Post hii inahusu zaidi dawa ya ampicillin, ni mojawapo ya dawa za kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mwili wa binadamu ba pia ni dawa ambayo IPO kwenye kundi la penicillin kundi hili kwa kitaa huitwa broad spectrum penicillin
1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kwamba hii ni dawa ambayo usaidia kutibu maambukizi ya bakteria na pia ni dawa ambayo imo kwenye makundi ya penicillin kama tulivyoona hapo kwenye utangulizi na pia dawa hii inaweza kusaidia pia kupambana na bakteria ambao utoa asidi Ili kuweza kuzuia kazi ya dawa, kama dawa husika haipo ampicillin inaweza kutumika.
2. Kwa kawaida ampicillin usaidia katika matibabu ya maambukizi ya bakteria kwenye Koo,sikio,mkojo na pia usaidia katika matibabu ya nimonia, dawa hii huwa na container lake kila container Ina milligrams mia mbili hamsini na na nyingine huwa na miigram mia tano na pia milligrams utolewa kulingana na wataalamu wa afya na pia dawa hii utolewa kila baada ya masaa sita , kabla ya kutumia dawa hii ni vizuri kutumiwa dakika thelathini kabla ya kula chakula.
3. Dawa pia IPO kwenye mfumo wa unga au poda na huwa na maji maalumu yametengwa kwa ajili ya kuchanganya poda hiyo na maji, maji hayo kwa kitaamu huiitwa water for injection, kwa hiyo dawa hiyo uchanganywa na maji na utikiswa na kuhakikisha kwamba poda haionekani tena na pia mgonjwa uweza kupewa dawa hiyo, kwa upande wa dozi utegemea umri na uzito wa mgonjwa. Pia dawa hiyo inawezekana kutolewa kwenye paja au Tako na pia kwenye mishipa ya damu.
Tunapaswa kufahamu kwamba mchanganyiko wa dawa inayopitia kwenye damu na kwenye paja au Tako ni tofauti kwa sababu ya kwenye mishipa inaenda Moja kwa moja kwenye damu kwa hiyo tunaongeza maji zaidi ya Ile inayopitia kwenye nyama ( Tako na paja).
4. Kwa wakati mwingine kuna syrup hizi ni kwa upande hasa wa watoto, mchanganyiko ni kutumia milligrams mia ishilini na tano kwenye mills tano na pia mtoto anapewa, mara nyingi hizi dawa zinakuja zimechanganywa Moja kwa moja na chupa Huwa na maagizo namna ya kutumia, kwa hiyo wazazi wa mtoto uweza kupewa maagizo na jinsi ya kumpatia mtoto dawa hiyo.
5. Dawa hii ya ampicillin na yenyewe Ina tabia kama dawa zote au makundi ya penicillin kwa hiyo kila mtu anaweza kutumia dawa hii ila kwa wale ambao Wana aleji na ampicillin hawapaswi kutumia dawa hii na pia wale wenye aleji ya penicillin hawapaswi kutumia kwa sababu dawa hii imo miongoni mwa makundi ya penicillin na pia kwa wale wenye tatizo la upungufu wa damu wanapaswa kuitumia kwa taahadhari au waitumie kwenye uangalizi maalumu Ili wasije kuleta tatizo kubwa zaidi kwa sababu dawa hii Ina tabia ya kupunguza damu hasa kwa watumiaji wa mara kwa mara.
6. Vile vile dawa hii Ina maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kujitokeza wakati wa kuitumia maudhi hayo ni pamoja na maumivu kwenye joint, kichefuchefu na kutapika, maumivu ya tumbo , kizunguzungu na upungu wa damu au kama Kuna mtu ana kidonda au sehemu inayotoa damu anaweza kuendelea kutoa damu kwa mda mrefu wakati akiwa anatumia dawa hii. Kwa hiyo haya maudhi madogo madogo yakitokea ni kawaida wakati wa kutumia dawa hii ila yakiongezeka na kuleta madhara zaidi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya na kubadilishiwaa dawa.
7. Pia ni vizuri kutumia dawa hii kwa ushauri wa wataalamu wa afya sio kutumia dawa hii kiholela kwa sababu matokeo yake yanaweza kuwa mabaya hasa kwa watu wenye damu kidogo wakitumia dawa hii wakiwa nyumbani wanaweza kuleta tatizo juu ya tatizo na pia kwa wale wenye sickle cell yaani wenye matatizo ya kuishiwa damu wanapaswa kuitumia dawa hii wakiwa kwenye uangalizi maalumu au wapime wingi wa damu kabla ya kutumia ai tatizo kama litakuwa kubwa zaidi na kuleta madhara ni Bora wabadilidhiwe na kupewa dawa ambazo hazitaleta madhara kwao.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi dawa hydrocortisone kwa kutuliza aleji au mzio, kwa kawaida Kuna mda mtu anapotumia dawa Fulani anakuwa na mabadiliko mbalimbali kama vile kifua kubana , viupele na mambo kama hayo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya kupambana na bakteria, hili kundi la fluoroquinolones lina dawa kuu mbili ambazo ni ciprofloxin na ofloxacin.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya potassium sparing katika matibabu ya magonjwa ya moyo.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako.
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya haloperidol katika matibabu ya magonjwa ya akili, ni mojawapo ya dawa ambayo utumiwa na wagonjwa ambao wamechananyikiwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya Mebendazole kama Dawa ya kutibu Minyoo, ni dawa inayotumiwa na watu wengi pale wanapokuwa na minyoo, walio wengi wamefanikiwa kupona kwa kutumia Dawa hii.
Soma Zaidi...hapa utajifunza dalili za fangasi, dawa ya fangasi na aina za fangasi, pia nitakujuza njia za kukabiliana na fangasi
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya carvedilo katika matibabu ya magonjwa, ni mojawapo ya dawa kwenye kundi la beta blockers na pia uhusika katika matibabu ya magonjwa ya moyo kama nyingine.
Soma Zaidi...