Fahamu dawa ya ibuprofen katika kutuliza maumivu

Post hii inahusu zaidi dawa ibuprofen katika kutuliza maumivu, ni aina mojawapo ya dawa na yenyewe ufanya kazi kama aspirin na paracetamol

Dawa ya ibuprofen katika kutuliza maumivu .

1. Ibuprofen ni dawa ambayo ufanya kazi ya kutuliza maumivu, ni dawa ambayo ufanya kazi ya kuzuia prostagland ambayo usambaza ujumbe kutoka sehemu Moja kwenda nyingine na kama Kuna maumivu sehemu na yenyewe yanaweza kusambaa lakini kwa kazi ya ibuprofen maumivu hayawezi kusambaa kutoka sehemu Moja kwenda nyingine.

 

2. Na pia dawa hii usaidia kutuliza maumivu baada ya upasuaji, kwa sababu baada ya upasuaji maumivu huwa makali lakini kwa sababu ya kazi ya ibuprofen maumivu yanaweza kupungua kwa kufuata utaratibu wa dawa yenyewe 

 

3. Dawa hii Iko kwenye mfumo wa vidonge kwa hiyo upitia mdomoni wakati wa kutumia na pia Ili kuepuka kuleta madhara kwenye utumbo ni vizuri kutumiwa baada ya kula au wakati wa kula Ili mradi pawepo chochote tumboni.

 

4. Dose yake kwa kawaida ni milligrams mia nne kwa kila masaa manane na ni lazima kufuata maagizo ya wataalamu wa afya kwa hiyo hiyo dawa isitumiwe kiholela Bali kwa utaratibu wa wataalamu wa afya.

 

5. Pia wasiopaswa kutumia dawa hii ni wake wenye aleji na dawa hii ndio hawapaswi kutumia . Pia Kuna maudhi madogo madogo yatokanayo na dawa hii kama vile kichefuchefu na kutapika, kuharisha na maumivu ya tumbo pamoja na maumivu ya kichwa.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/17/Saturday - 03:27:34 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 578


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-