Dawa ya Rifampicin na kazi zake

Dawa ya Rifampicin na kazi zake

Posti hii inahusu zaidi Dawa ya Rifampicin na kazi zake, hii ni dawa mojawapo inayotibu kifua kikuu kati ya Dawa zilizoteuliwa kutibu ugonjwa wa kifua kikuu.

Dawa ya Rifampicin na kazi zake.

1.Dawa ya Rifampicin ni dawa ambayo utumika katika kipindi cha kwanza na cha pili katika vipindi vikuu viwili vya matibabu ya kifua kikuu, hii dawa usaidia kuuua bakteria wanaosababisha kifua kikuu na pia kuzuia protein ya bakteria isizalishwe kwa hiyo bakteria hao hawawezi kuishi na kuzaliana kwa sababu ya kuwepo kwa dawa ya Rifampicin.

 

2.Pia hii dawa usaidia kuua bakteria anayeitwa TB bacill  na pia dawa hiii uweza kuua bakteria ambao wameshaene kwenye mwili wa binadamu na pia uua bakteria wale ambao wamekaa mda mrefu kwenye mwili wa binadamu, kwa hiyo tunaona faida kubwa ya dawa hii tunapaswa kuitumia kwa maelekezo ya wataalamu wa afya, pia dawa hii haiwezi kutumika ikiwa yenyewe bali huwa na mchanganyiko wa madawa mengine.

 

3.Dawa hii ya Rifampicin utumiwa na watu wenye kifua kikuu lakini sio wote wenye kifua kikuu wanaweza kutumia kwa sababu mbalimbali kwa mfano wale wanaotumia uzazi wa mpango na wana Ugonjwa wa kifua kikuu wanapaswa kuona madaktari ili waweze kupata njia za uzazi wa mpango hambazo haziingilian na dawa ya Rifampicin kwa sababu kuna njia za uzazi wa mpango ukizitumia pamoja na dawa ya Rifampicin dawa hii uweza kumaliza dawa za njia ya mpango nguvu na mtu akapata mimba.

 

4.Pamoja na kutumia njia hii kuna maudhi mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza katika kutumia dawa hizi ni kama kichefuchefu, kutapika na hata kuharisha kwa wagonjwa wengine, na maumivu ya kichwa yanaweza kutokea pia pamoja na homa, kwa hiyo hizi Dalili zikitokea mgonjwa hasiogope ni kawaida ila kwa wanaoanza maudhi haya yakiendelea wanapaswa kwenda hospitalini ili kuangalia labda kuna tatizo fulani.

 

5.Kwa kubwa ugonjwa huu unatibika tunapaswa kuwapeleka wagonjwa wetu hospitali ikiwa wataonesha Dalili za kifua kikuu ambazo ni pamoja na homa za mara kwa mara, kupungua uzito , kukohoa kwa wiki mbili na kukonda hizi ni baadhi ya Dalili tunapaswa kuwahi mapema kwa sababu Ugonjwa huu usambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kama mgonjwa hajatumia dawa akishatumia dawa kwa wiki mbili hawezi kuambukiza wengine.

 

6.Kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwa jamii ili kuwaleta wagonjwa wao hospitalini wasiwafiche na kuna imani potovu ambayo utokea kubwa mgonjwa wa kifua kikuu ufuchwa ndani wakidai kuwa ana Maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi kumbe ni kifua kikuu kwa sababu ya kufanana kwa baadhi ya Dalili, kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa ili kuweza kutokomeza kabisa janga hili

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Dawa Main: Post File: Download PDF Views: 4219

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zinazofanana:

Fahamu dawa ya kuzuia enzymes zinazotengenezwa na bakteria

Post hii inahusu zaidi dawa ya cloxacillin ambayo Iko kwenye kundi mojawapo la penicillin ambalo uzuia enzymes zinazotengenezwa na bakteria.

Soma Zaidi...
Ni dawa gani hatari kwa mjamzito?

Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako.

Soma Zaidi...
Tiba mbadala za vidonda vya tumbo

Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala za vidonda vya tumbo

Soma Zaidi...
Matumizi ya dawa ya vidonda vya tumbo

Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
dawa ya kutibu infection kwenye kizazi nisaidie doctor

Je unasumbuliwa na maambukizi na mashambulizi ya virusi na bakteria kwenye sehemu za siri ama via vya uzazi?. Posti hii inakwenda kuupa ushauri.

Soma Zaidi...
Miungurumo haiishi tumboni nikishika upande wa kushoto wa tumbo kuna maumivu kwa mbali je mm nitumie dawa gan kuondoa tatizo hilo

Kukawa na gesi tumboni kunaweza kuwa ni dalili ya shida kwenye afya, hasa katika mfumo wa chakula. Hali itakuwa sio nzuri endapo utakosea hamu ya kula na kuhisivkushiba muda wowote.

Soma Zaidi...