Ifahamu dawa ya kupunguza maumivu

Post hii inahusu dawa ya aspirin katika kupunguza maumivu,ni dawa ambayo upunguz maumivu ya Kawaida, kushusha homa na pia usaidia kwenye magonjwa ya moyo hasa kuzuia stroke kama imetokea mda ndani ya masaa ishilini na manne

Ifahamu dawa ya aspirin katika kupunguza maumivu.

1. Dawa hii ni mojawapo ya madawa ambayo yamechaguliwa kupunguza maumivu ya Kawaida na  kama tulivyoona hapo mbeleni Ina saidia pia katika magonjwa ya moyo, kwa hiyo hii dawa inatumika na watu mbalimbali ila Kuna watu ambao hawapaswi kutumia dawa hii nao ni watu wenye ugonjwa wa kubanwa na kifua kwa kitaamu ugonjwa huu huiitwa Asthma au katika kutumia wagonjwa hao wanapaswa kuwa makini au kutumia dawa hii kwa uangalizi zaidi na wataalamu wa afya,

 

2. Vile vile sio wagonjwa wa asthma peke yao ambao hawapaswi kutumia dawa hii pia na wale wenye aleji na dawa hii ya aspirin, Kuna wale wanaotumia wakabanwa na kifua, wengine wakawa na ma upele na mambo kama hayo hao watu wa aina hii hawapaswi kutumia dawa ya aspirin. Pia Kuna wale watu ambao Wana magonjwa ya Figo na hao hawapaswi kutumia dawa hii ya aspirin kwa sababu usababisha madhara zaidi kwa hiyo kwa wenye matatizo na dawa hii wanapaswa kutumia dawa kwa kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.

 

3. Pia wengine ambao hawapaswi kutumia dawa ya aspirin ni watoto wote chini ya miaka kumi na minane na pia akina Mama wanaonyonyesha Hawapaswi kutumia dawa hii kwa sababu hii dwa inaweza kuwa chanzo cha ugonjwa ambao kwa kitaamu huiitwa Reyes syndrome huu ni ugonjwa unaowapata akina Mama na watoto chini ya miaka kumi na sita , kwa hiyo akina Mama wanaonyonyesha na watoto chini ya miaka kumi na sita watafutiwe dawa nyingine za maumivu Ili kuepuka madhara mengine.

 

4.pia watu wenye tatizo la vidonda vya tumbo na wenyewe hawapaswi kutumia dawa hii ya maumivu aina ya aspirin, na wale wenye tatizo la kutoka na damu hasa kwa kitaamu huiitwa haemophilia na wenyewe hawapaswi kutumia dawa hii ya maumivu. na pia dawa hii  uingilia kwenye mfumo wa uchujaji wa mkono ambapo inaweza kusababisha mkojo husichujwe vizuri ndio maana kwa wagonjwa wa Figo ni marufuku kutumia dawa hii labda kwa ruhusa ya wataalamu wa afya , kwa hiyo kwa wahusika ni vizuri kabisa kuzingatia hayo.

 

5. Matokeo ya dawa hii ya aspirin , kwa watumiaji wa dawa hii ya aspirin wanaweza kupata matokeo mbalimbali kama haya kuwepo kwa magonjwa ya Figo kwa watumiaji hali hii ikitokea ni kuacha dawa mara Moja,pia kuwepo kwa matatizo kwenye nefron yanaani kwenye mfumo mzima wa kuchuja mkojo kwa watumiaji wa dawa hii ya aspirin wakipata shida hiyo ni vizuri kabisa kuacha dawa hiyo,pia Kuna uwezekano wa kusikia kwa shida, kichefuchefu na kutapika, na Pia kwa matumizi ya dawa mda mrefu usaidia kuzuia kubalance kiwango cha asidi na base mwilini.

 

6.kwa sababu dawa hii huwa inapunguza maumivu Kuna wakati mwingine ikitumiwa sana na mgonjwa anaweza kuwa na homa sana kwa sababu ya kuharibika au kuvurugika kwa sehemu mbalimbali kama vile Figona ini homa inaweze pia kuongeza hali ya kuharibika kwa mifumo mingine ya mwili ambayo Kwa kitaamu huiitwa metabolic rate kitendo cha kuharibika kwa metabolic rate  au kuongezeka kwa metabolic rate usababisha kuwepo kwa virusi kwenye ini na kusababisha maambukizi kwenye ini kwa hiyo wenye magonjwa ya ini na Figo wasitumie dawa hii ila kwa ushauri wa wataalamu wa afya.

 

7. Dawa hii huwa kwenye mfumo wa vidonge na umezwa kwa kutumia maji na baada ya kula kushiba kwa sababu ikimezwa bila kushiba uweza kusababisha vidonda vya tumbo hasa kwa watumiaji wa mda mrefu na milligrams ambazo zinatumika ni kiasi cha 300  milligrams mpaka mia tisa milligrams kwa masaa masaa sita, na maximum dozi ni 4kilogram hii dozi , pia dozi upangwa kwa kadri ya uzito, umri wa kila mgonjwa kwa hiyo ni vizuri kutumia dawa hii kwa kadri ya maagizo ya wataalamu wa afya.

 

8. Kwa sababu dawa hii Ina matokeo mengi kwa wagonjwa ambao wanatumia pia ambao hawapaswi kutumia ni wengi kama vile wenye vidonda vya tumbo, wenyewe athma , akina Mama wanaonyonyesha na watoto chini ya miaka kumi na sita,wenye magonjwa ya Figo, magonjwa ya nefron, wenye magonjwa ya ini, kwa hiyo dawa hii isitumiwe kiholela holela kwa sababu Ina madhart mengi katika matumizi na inaweza kuleta matatizo mengine zaidi ni vizuri kupata ushauri wa wataalamu wa afya katika matumizi ya dawa hii.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Dawa Main: Afya File: Download PDF Views 1050

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Fahamu kuhusu dawa za kutibu minyoo

Post hii inahusu zaidi dawa mbalimbali za kutibu minyoo, tunafahamu kabisa minyoo ni ugonjwa ambao uwapata watu mbalimbali hasa watoto.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya parental Artusnate dawa ya kutibu malaria sugu

Post hii inahusu zaidi dawa ya Parental Artusnate ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa malaria sugu kama tutakavyoona hapo baadaye.

Soma Zaidi...
Dawa za kutibu ugonjwa wa macho

Somo Hili linakwenda kukuletea dawa za kutibu ugonjwa wa macho

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa ya Theophylline katika kutibi mfumo wa upumuaji

Post hii inahusu zaidi dawa ya theophylline ni dawa inayofanya kazi kwenye mfumo wa upumuaji.

Soma Zaidi...
Ijue dawa ya cephalosporin katika kupambana na bakteria

Post hii inahusu zaidi dawa ya cephalosporin katika kupambana na bakteria, ni mojawapo ya kundi kati ya makundi ya kupambana na bakteria ambalo ufanya Kazi kama penicillin.

Soma Zaidi...
Dawa ya kuzuia kuathirika kwa watu walio hatarini kupata VVU

Somo hili linakwenda kukuletea dawa ya kuzuia kuathirika kwa watu walio hatarini kupata VVU

Soma Zaidi...
Imani potofu kuhusu madawa ya hospitalini

Post hii inahusu zaidi imani potofu kuhusu madawa yanayotolewa hospitalini, ni imani waliyonayo Watu hasa Watu wa bi vijijini na hata wa mjini nao wameanza kutumia madawa ya miti shamba kwa wingi.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa za kifua kikuu

Post hii inahusu dawa za kifua kikuu ni dawa ambazo utumika kutibu kifua kikuu, kwanza kabisa kabla ya kuanza kufahamu dawa hizo ni vizuri kabisa kufahamu kifua kikuu nini hili kuweza pia kufahamu dawa zake.

Soma Zaidi...
Miungurumo haiishi tumboni nikishika upande wa kushoto wa tumbo kuna maumivu kwa mbali je mm nitumie dawa gan kuondoa tatizo hilo

Kukawa na gesi tumboni kunaweza kuwa ni dalili ya shida kwenye afya, hasa katika mfumo wa chakula. Hali itakuwa sio nzuri endapo utakosea hamu ya kula na kuhisivkushiba muda wowote.

Soma Zaidi...
Dawa ya fangasi uumeni

kama unasumbuliwa na fangasi uumeni, nitakujuza dawa yake, sababu za fangasi uumeni, matibabu yake na njia za kuwaepuka

Soma Zaidi...