Matibabu ya ugonjwa wa uti wa mgongo

Posti hii inahusu zaidi matibabu kwa mgonjwa wa uti wa mgongo, kwa kawaida tunajua kuwa homa hii ya uti wa mgongo usababisha na wadudu mbalimbali kama vile bakteria, virus, fungasi, sumu mbalimbali kama vile madini ya lead na arseni, na vitu kama vile Mag

Matibabu ya ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.

1. Kwa kuwa sababu za Ugonjwa huu ni nyingi kwa hiyo tunatibu kadri ya kisababishi, kama mdudu aliyesababisha ni kirusi kwa kawaida huwa hakuna dawa maalumu kwa ajili ya kirusi, kwa kawaida uanza na kuisha chenyewe kwa baadhi ya wagonjwa ila tunatibu kwa kulingana na dalili inayojitokeza,kwa hiyo ni vizuri kabisa kujua chanzo cha homa ya uti wa mgongo ni nini ili tuweze kujua matibabu maalum.

 

2. Kwa kawaida Ugonjwa huu uathiri sana sehemu za ubongo ni vizuri kabisa mgonjwa kutibiwa kwenye mazingira ya ukimya na kuhakikisha hakuna kitu chochote ambacho kinatumia nguvu ili mgonjwa aweze kufikilia zaidi kwa hiyo ni vizuri kabisa kumtenga Mgonjwa na kuepuka tabia ya kuzungumza naye bila sababu, tunafanya hivyo ili kuweza kupumzisha ubongo ambao umeathirika ili kuweza kurudi kwenye hali ya kawaida.

 

3. Kwa sababu ya visababishi mbalimbali mgonjwa anaweza kutibiwa kwa kutibu dalili kwa mfano kama ana homa anapaswa kupewa dawa za kutuliza homa, kama ana degedege anapewa dawa za degedege, na kama hawezi kula anapewa mpira wa kuweza kumrishia  chakula na kawa hawezi kwenda haja kubwa  na ndogo anawekewa mpira wa kuweza kupitisha mkojo na pia mgonjwa anapaswa kukaa katika hali ya usafi mda wote.

 

4. Na pengine visababishi vinaweza kuwana dawa za moja kwa moja kwa mfano kama aliyesababisha ni bakteria la zima Mgonjwa atapewa antibiotics kama vile chloramphenicol, benzyl penicillin,certriaxone, ampicillin,cefotaxime na kama  ni fungasi tunampatia anti fungasi , kama ana degedege tunampatia dawa hizo, kwa hiyo tunapokuwa tunamtibu mgonjwa huyu tunapaswa kuwa makini ili kuweza kuepuka Maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Dawa Main: Afya File: Download PDF Views 2420

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 web hosting    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Penicillin dawa ya kutibu maambukizi ya bakteria mwilini

Post hii Inahusu zaidi dawa za kutibu maambukizi yoyote Yale yanayosababishwa na bakteria dawa hizi kwa kitaamu huiitwa antibiotics Kuna dawa mbalimbali zinazotibu maambukizi ya bakteria leo tutaanza na dawa ambayo inaitwa penicillin.

Soma Zaidi...
Dawa za fangasi ukeni

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za fangasi ukeni

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu dawa za kutibu minyoo

Post hii inahusu zaidi dawa mbalimbali za kutibu minyoo, tunafahamu kabisa minyoo ni ugonjwa ambao uwapata watu mbalimbali hasa watoto.

Soma Zaidi...
dawa ya kutibu infection kwenye kizazi nisaidie doctor

Je unasumbuliwa na maambukizi na mashambulizi ya virusi na bakteria kwenye sehemu za siri ama via vya uzazi?. Posti hii inakwenda kuupa ushauri.

Soma Zaidi...
Dawa ya kutibu minyoo

Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote

Soma Zaidi...
Matumizi ya dawa ya vidonda vya tumbo

Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Dawa za kutibu ugonjwa wa macho

Somo Hili linakwenda kukuletea dawa za kutibu ugonjwa wa macho

Soma Zaidi...
Matibabu ya Fangasi ukeni na dawa za fangasi wanaoshambulia uke.

Fangasi wanaweza kushambulia uke, kwa juu kwenye mashhav ya uke ama kwa ndani. Hali hii inaweza kusababisha miwasho na maumivu pia. Inaweza kusababisha michubuko na kutofurahia tendo la ndoa. Makala hii inakwenda kukujuza dawa na matibabu ya fangasi ukeni

Soma Zaidi...
Dawa ya kutibu maumivu ya jino

Utaijuwa Dawa ya maumivu ya jino, sababu za maumivu ya jino na njia za kujikinga na maumivu ya jino

Soma Zaidi...
Ifahamu dawa ya kutibu kifua kikuu

Post hii inahusu zaidi dawa ya Rifampin kama dawa mojawapo ya kutibu kifua kikuu.

Soma Zaidi...