HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYUKI


Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Utamjuaje kama ana aleji na nyuki?. ni pale utakapomuona aliyeng’atwa na nyuki akivimba mwili, na anaweza pia kupoteza fahamu. Pia hali hizi zinategemea ni kiasi gani cha nyuki wamemg’ata mtu.



Utakapomuona mtu ameng’atwa na nyuki usimkimbie, kwanza msaidie, kuhakikisha kuwa nyuki hawamng’ati tena. Unaweza kuchukuwa blanketi ama shuka uakmfunika vyema. Hakikisha na wewe umefunika pua, mgomo na masikio. Kama nyuki wanaendelea kuja mmwagie maji mgonjwa ili kupoteza harufu ya nyuki.



Hakikisha kabla hujaanza kutoa huduma ya kwanza, kwanza unaangalia hali ya aliyeng’atwa, kama hali ni ya kawaida na hahitaji kwenda hospitali. Kama anahitaji kwenda hospitali haraka wasiliana na kituo kilicho jirani ama tafuta msaada, kwa watu walio karibu. Hakikisha maamuzi haya hayaathiri hali ya mgonjwa. Ili kumpa huduma ya kwanza aliyeng’atwa na nyuki:-


1.kwa upole tumia kitu chenye wembamba kisha toa miiba ya nyuki kwenye ngozi ya mgonjwa. Katu usitukie kucha zako, maana zitaipasua miipa na sumu itaingia ndani na katu hutaweza kuitoa tena.


2.Unaweza kutuia kisu, ama kituchenye ncha, ila hakikisha kuwa miiba ya nyuki haikatiki kwa ndani. Kwa mfano unapotumia kiwembe kuna uwezekano mkubwa ukaikata miib kwa ndani.


3.Muweke mgonjwa mahali pa ubaridi kama inawezekana


4.Osha maeneo aliyong’atwa kwa sabuni na maji


5.Unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu.


6.Zipo dawa kama losheni (calamine lotion) ila ni maalumu kwa aliyeng’atwa na nyuki, kama zipo mgonjwa apakwe.


7.Hakikisha unamtuliza moyo mgonjwa.


8.Kama hali ni mbaya bado mgonjwa apelekwe kituo cha afya.