HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYOKA
Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu.
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYOKA
Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu. Ni vigumu kuwatofautisha wenye sumu na wasio na sumu kwani wakati mwengine wanafanana sifa. Wataalamu wameweka njia kadhaa za kuweza kuwajuwa weenye sumu. Nyoka mwenye sumu ana sifa zifuatazo
1.kichwa chake kipo katika pembe tatu
2.Rangi zake zinameremeta sana
3.Mboni ya Macho yao yamefanana na macho ya paka
4.Wanapoogelea kwenye maji miili yao inaelea juu
Tmbua kuwa sifa hizi hata nyoka wasio na sumu wamaweza kuwa nazo. Kuwa makini na kaa mbali na nyoka wa aina yeyote kama huna ujuzi na utambuzi huu. Mtu aliyengatwa na nyka mwenye sumu ataonyesha dalili zifuatazo:-
1.Uchovu
2.Kizunguzungu
3.Anaweza kuzimia
4.Kichefuchefu
5.Kuharisha
6.Kutapika
7.Mapigo ya moyo kuongezeka kwa kasi
8.Misuli kukosa uweze wa kutanuka na kusinyaa
9.Kuvimba eneo alipong’atwa.
Ukiona mtu ameng’atwa na nyoka na akaonyesha dalili hizi, wahi kuomba msaada ili awahishwe ituo cha afya kwa haraka. Hakikisha unampatia huduma ya kwanza ili kupunguza athari za kusambaa kwa sumu mwilini. Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka inaweza kuwa kwa nama zifuata zo:-
1.mtulize mgonjwa nafsi yake, mpe maneno matamu na ya kutuliza. Hii itasaidia moyo kupunguza kazi ya kusambaza damu mwilini, hivyo sumu haita sambaa kwa kasi.
2.Muweke mgonjwa chini, na katu usimtembeze, mlaze chini kwa namna ambayo sehemu alipong’atwa itakuwa chini. Kwa mfano kama ameng’atwa mguuni, unaweza kumuwekea kitu kichwani akaegemea kwa mto ili sehemu ya mguuni iwe chini.
3.Ondoa mengo ya nyoka kwa uangalifu na katu usimishe eneo alilongatwa na nyoka.
4.Kama mgonjwa ana kizunguzungu, ama baridi mfunike kwa nguo ili kumuongezea joto
5.Chukuwa maelezo kuhusu aina ya nyoka, hii itasaidia wataalamu wa afya kujuwa tiba sahihi.
6.Osha eneo kwa kupitishia maji kwa juu na katu usisugue ama kuminya jeraha.
Usifanye vitu hivi:
1.Usinyonye sumu kwa mdomo wako
2.Usimpe mgonjwa chakula wala maji
3.Usimtembeze mgojwa
4.Usitumie barafu sehemu yenye jeraha
5.Usifunge kwenye jeraha eti kuzuia mzunguo wa damu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 ai web app 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Ratiba ya chanjo ya polio
Posti hii inahusu zaidi namna chanjo ya polio inavyotolewa na ratiba zake yaani kuanzia siku ya kwanza mpaka pale mtoto anapomaliza chanjo hii kwa hiyo tuone ratiba ya chanjo ya polio.
Soma Zaidi...Umuhimu wa kupumzika kiafya
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kupumzika kiafya, kwa kawaida mwili na viungo vingine vya mwili uweza kufanya kazi zaidi pale mtu akiwa amepumzika.
Soma Zaidi...Njia za kufuata unapohudumia watu waliopata ajali
Post hii inahusu zaidi namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa watu waliopata ajali. Ajali ni tukio lisilotarajiwa ambalo kinaweza kumkuta mtu yeyote, tunapotoa huduma ya kwanza tnazingatia rangi ambazo huwakilisha jinsi watu walivyoumia.
Soma Zaidi...Mambo yanayochangia Ili dawa kuingia kwenye damu vizuri
Post hii inahusu zaidi mambo yanayochangia Ili dawa iingie vizuri kwenye damu, na mambo yanayoweza kusababisha dawa kuingia au kutoingia vizuri kwenye damu.
Soma Zaidi...Kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi
Somo Hili linakwenda kukueleza sababu za kwanini mbu hawezi kuambukiza ukimwi
Soma Zaidi...Njia za kuingiza chanjo mwilini
Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...