image

Fahamu kuhusu vitamini K na kazi zake mwilini

vitamini k ni moja katika vitamini vinavyoitajika sana mwilini. Je unazijuwa athari za upungufu wa vitamini k mwilini?

VITAMIN K NA FAIDA ZAKE MWILINI

Vitamini K ni moja kati ya vitamini ambavyo miili yetu inavihitaji kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Endapo upungufu wa vitamini hivi utatokea basi madhara makubwa ya kiafya yatamkumba mtu. Katika makala hii nimekuandalia somo hili ambalo litakwenda kuangalia zaidi kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake.


 

YALIYOMO:

  1. Nini maana ya vitamini
  2. Vitamini K ni nini?
  3. Wapi nitapata vitamini K
  4. Ni zipi kazi za vitamin K
  5. Ni zipi athari za upungufu wa vitamini K
  6. Ni zipi athari za kuzidi kwa vitamin K


 

NINI MAANA YA VITAMINI?

Vitamini ni kampaudi ogania ambazo zinahitajika na mwili kwa ajili ya ukuaji wa mwili na utendaji wa michakato ya kibaiolojia ndani ya miili (metabolism), na ni viruubisho ambavyo havitengenezwi ndani ya miili yetu. Vitamini vipo katika makundi makuu mawili ambayo ni fat soluble na water soluble. Pia makundi ya vitamini ni A, B, C, D na K.


 

Fat soluble ni titamini ambavyo mwili unaweza kuvihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadaye vitamini hivi ni kama A, D, E na K. Hii ina maana hatuhitaji tule vyakula vyenye vitamin hivi kila siku. Watwer soluble ni vitamini ambavyo mwili hauwezi kuvihifadhi mwilini hivyo baada ya kula chakula mwili hufyonza kiasi cha vitamini hivi na kuvitumia. Hivyo tunahitajika tule vyakula vyenye vitamini hivi kila siku. Vitamini hivi ni kama D na C.


 

VITAMIN K NI NINI?

Hivi ni vitamini katika kundi la fat soluble ambavyo vimetokana na kampaundi za naphthoquinone. Vitamin hivi vimeitwa K, hii K asili yake ni neno la lugha ya Danish kutoka neno koagulation neno hili ukilileta kwenye lugha ya kiingereza unapata coagulation yaani kuganda. Hasa hapa kunazungumziwa kuganda kwa damu. Kwani vitamin K huhitajika mwilini katika kusaidia mchakato wa kuganda kwa damu pindi mtu anapopata jeraha.


 

Kwa mara ya kwanza vitamin K vimeanza kuletwa kwenye maandishi na mwanasayansi wa Danish mwaka 1929 Bwana Henrik Dam pindi alipokuwa akifanya tafiti juu ya kazi za Cholesterol kwenye mwili. Wataalamu wa lishe wameigawa vitamin K katika makundi ya K1 na K2. hivi vya K1 kitaalamu huitwa phytonadione huweza kupatikana kwenye mboga za majani na hivi vya K2 kitaalamu huitwa menaquinone hupatikana kwenye nyama, mayai na maziwa.

 

VYAKULA VYA VITAMIN K

Kama ulivyosoma hapo juu kuwa vitani K vipo katika makundi kma Vitamin K1 na vitamin K2 na pia umeona kwa ufupi vyanzo vya kila vitamini K. Sasa hapa nitakuorodheshea tena vyanzo vya vitamin K

Vitamin K1:

Vitamini hivi unaweza kuvipata kwenye mboga za majani za rangi ya kijani kama

  1. Mchicha
  2. Kabichi
  3. Spinach
  4. Kisamvu
  5. Mboga nyinginezo za majani
  6. Mapalachichi
  7. Zabibu
  8. Na matunda mengineyo


 

Vitamin K2

Hivi unaweza kuvipata kwenye;-

  1. Nyama
  2. Mayai
  3. Siagi
  4. Maziwa
  5. Na vyakula vinginevyo vya mfanano na hivi

 

KAZI ZA VITAMIN K MWILINI

Kama tulivyokwisha kuona maana ya K kweye vitamini K, sasa hebu tuone baadhi tu ya kazi za Vitamin hivi.

  1. Husaidia katika kuganda kwa damu
  2. Husaidia katika afya ya ubongo
  3. Husaidia katika kulinda afya ya mifupa
  4. Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo
  5. Husaidia katika uthibiti wa matumizi ya madini ya calcium (chumvi) mwilini


 

  1. Kuganda kwa damu:

Hii ndiyo kazi kuu ya vitamin K, ni kuwa pindi unapopata jeraha lolote ambalo litapelekea damu kutoka, basi ili kuhakikisha damu haitoki zaidi katika jeraha lile,na hatimaye damu hukata, kazi hii yote hufanya na vitamin K hasahasa hapa tunazungumzia K1. vitamini K hutumika katika kutengeneza prothrombin, factors VII, IX, pamoja na X, kwa pamoja huitwa cloting factor na ndizo ambazo huhusika katika kusimamisha damu isiendelee kutoka kwenye jeraha. Upungufu wa vitamin K unaweza kusababisha damu kutokuganda ama utoka hata kama hakuna jeraha.


 

  1. Husaidia katika Afya ya Mifupa

Kuna ugonjwa unatambulika kama osteoporosis haya ni maradhi ya mifupa kuwa midhaifu, kuuma na kuweza kupasuka kwa urahisi sana. Mara nyingi maradhi haya yanawapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 50, lakini pia unaweza kuwapata watu wenye chini ya hapo.

Wataalamu wa afya wanahusianisha upungufu wa vitamin K na kupata maradhi haya. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamin K husaidia katika kuboresha afya ya mifupa, kuthibiti ujazo na tungamo la mifupa pia kuzuia mipasuko kwenye mifupa. Hatahivyo tafiti zaidi zinahitajika kuthibitisha zaidi.


 

  1. Afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu;

Tafiti zinahusisha uwezo wa kukumbuka na vitamin k. baadhi ya tafiti zilizofanywa zinaonyesha kuwa watu wenye umri wa zaidi ya 70 huwa uwezo wao wa kukumbuka unapungua, ila kwa wale ambao wana vitami K vya kutosha kwenye damu zao uwezo wao wa kukumbuka unakuwa mkubwa. Na hapa pia tunazungumzia sana vitamin K1.


 

  1. Kuboresha na kulinda afya ya moyo

Vitamin K husaidia katika kushusha presha ya damu kwa kuzuia kuganda kwa madini ndani ya mishipa ya damu. Hali hii huweza kusaidia moyo uweze kusukuma damu bila ya matatizo yeyote. Tafiti zinaonyesha kuwa kuwa na vitami K vya kutosha huzuia ama kupunguza athari za kupata stroke yaani kupalalaizi.


 

  1. Hulinda mwili dhidi ya kukuwa kwa seli za sartani.

Baadhi ya waandishi wanaeleza kuwa vitamin K huweza kusaidia kuondosha ama kulinda mwili zidi ya kupata vimbe za saratani. Lakini bado hakuna ushahidi wa kisayansi wa kutosheleza kuthibitisha madai haya.

 

ATHARI ZA VITAMIN K

Ijapokuwa vitamin K vinafida kubwa ndani ya miili yetu kama tulivyoona hapo juu. Basi pia itambulike kuwa vitamin K vikizidi zaidi ndani ya miili yetu vinaweza kusababisha madhara ya kiafya kama;-


 

Kama vitamin K itakuwa ni nyingi ndani ya mwili inaweza kupelekea athari kwenye figo. Pia inaweza kuhatarisha afya ya ini kama itatumika kwa kiwango kikubwa zaidi. Inaweza kuhatarisha ugandaji wa damu kwenye ini. Ni K vinaweza kushusha kiwango cha sukari hivyo kwa wenye kisukari itakuwa ni vyema akiwa chini ya uangalizi wa daktari kama anatumia dozi ya vitamin K.

 

UPUNGUFU WA VITAMIN K

Kama tulivyoona kazi za vitamin K katika miili yetu sasa hebu tuone ni zipi Athari za upungufu wa vitamin hivi ndani ya miili yetu

  1. Kuchelewa kuganda ama kusimama kwa damu katika jeraha ama kidonda
  2. Kutokwa na damu hata kama hakuna jeraha
  3. Ni rahisi kupata maradhi ya saratani (cancer)
  4. Ni rahisi kupata maradhi ya moyo
  5. Kupunguza hadira na misongo ya mawazo
  6. Kutoweza kuthibiti kumbukumbu
  7. Kuchoka kwa mifupa.

 

Mwisho

Vitamini K unaweza kuvipata kwa njia ya chakula ama kwa kumeza vidonge. Kwa wale ambao wana upungufu na vitamin unaweza kununua vidonge vya vitamin kwa kufuata maelekezo ya daktari. Usiwache kuwa nasi kwa kupata makala nyingine zaidi za afya hapa kwetu.

 

 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1632


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Huduma ya kwanza kwa mtu aliyekula sumu
Post hii inahusu zaidi kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyekula chakula chenye sumu, kula sumu ni kitendo Cha kula kitu chochote kama dawa,pombe, kemikali na chakula kichafu. Soma Zaidi...

Upungufu wa vyakula vya madini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula vya madini Soma Zaidi...

Zijue kazi za chanjo ya DTP au DPT (Donda Koo,Pepopunda, na kifaduro))
Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya DTP au DPT ambayo Inazuia magonjwa ya Donda Koo, Pepopunda na kifaduro. Soma Zaidi...

Huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYUKI
Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Soma Zaidi...

Imani potofu juu ya chanjo.
Post hii inahusu zaidi Imani potofu juu ya chanjo kwa watoto na akina Mama, ni baadhi ya Imani waliyonayo watu juu ya chanjo. Soma Zaidi...

Upungufu wa damu mwilini
Post inaenda kuzungumzia kuhusiana na upungufu wa damu mwilini ambapo tutaona SABABU na dalili zake lakin upungufu wa damu mwilini hujulikana Kama ANEMIA. Soma Zaidi...

Njia za kujikinga na vidonda vya tumbo
Kama unahitaji kujuwa namna ya kuweza kujikinga na vidonda vya tumbo, basi makala hii ni kwa ajili yako. Hapa utaweza kuzijuwa hatuwa zote za kujikinga na kupata vidonda vya tumbo. Soma Zaidi...

Sababu za kumwosha Mgonjwa mwili mzima.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kumwosha Mgonjwa mwili mzima,ni sababu ambazo umsaidie mgonjwa ili aweze kupata nafuu mapema na kumsaidia kama tutakavyoona hapo chini Soma Zaidi...

Njia za kushusha presha
Post hii inakwenda kukujulisha njia za kushusha presha iliyopanda. Soma Zaidi...

Madhara ya chakula kutosagwa vizuri tumboni.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni, haya ni madhara ambayo utokea kwa sababu ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni. Soma Zaidi...

Jifunze jinsi ya kumsaidia mwenye kifafa
Kifafa hakiambukizi na ugonjwa wa ubongo lakini kifafa pia hakiathiri akili au ubongo Ila kikiwa kifafa Cha kudumu na Cha nguvu ndio huweza kuadhiri. Pia Kuna kifafa Cha mimba na kifafa Cha kawaida.kifafa Cha mimba ndio kinahatari Sana kuliko Cha Kawaid Soma Zaidi...