Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa
.HUDUMA YA KWANZ AKWA ALIYEPALIWA AMA KUKWAMWA NA KUTU KOONI
Mtu aliyepaliwa ama kukwamwa na kitu kooni huwa anashindwa kuzungumza ama kupumua. Hali hii ikiendelea kwa muda inaweza kumsababishi amadhara makubwa hata kifo. Ubongo unaweza kufa ndani ya dakika chache sana kama ukikosa hewa ya oksijeni. Kama ukimkuta mtu amepaliwa ama kukamwa na kitu kooni na anashindwa kupumua unatakiwa umpe huduma ya kwanza:
Mtu anaweza kukwamwa ama kupaliwa na chakula, ama kitu kigumu kama kumeza pesa, jiwe barafu na kadhalika. Pia anaweza kupaliwa na maji, asali ama kimiminika chochote na kuzuia njia ya hewa. Hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Kama kupaliwa ni kwa kawaida amnapo mtu atakuwa na uwezo wa kukohoa, kulia, kuzungumza na kuhema, tambua kuwa anaweza kurudi katika hali ya kawaida hata bila ya kupata huduma ya kwanza. Ili kumsaidia mtu huyu kurudi haraka katika hali ya kawaida
1.Mwambie aendelee kuhohoa zaidi hii itasaidia kuondoa kilichokwama
2.Mwambe ajaribu kutema kicho kilichomkaba ama kilicho mkwama ama kusababisha kupaliwa
3.Katu usuthubutu kuingiza vidole vyeko kwenye koo lake eti kujaribu kukitoa kilicho mkaba
Kupaliwa kwa namna nyingine iliyo mbaya ni pale mtu anaposhindwa kusema, kukohoa, kulia ama kuhema. Bila ya huduma ya kwanza mtu huyu anaweza kuzimia na hatimaye kupoteza maisha. Huduma ya kwanza kwa mtu huyu ni:-
1.Muinamiche kifua chake kwa mbele, hii itasaidia kitu kilichomkaba kisiende ndani sana
2.Simama nyuma yake pembeni kidogo, weka mkono wako mmoja kwenye kifua chake na mgono wako mwingine anza kumpiga ngumi kwenye mgongo wake kati ya bega na bega, usawa na kifua kwa nyuma.
3.Angalia kama kilichomkaba kimeondoka
4.Kama hakijaondoka mpige tena kwa nguvu mapigo matano kama ni mtoto mminye kwa nguvu kwenye tumbo lake fanya hivi mara tano. Usifanye hivi kwa mtoto mdogo.
5.Kama hali inaendelea umpeleke kituo cha afya cha karibu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 ai web app 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIKAZWA NA MISULI
Kukaza kwa misuli lunaweza kutokea muda wowote ila mara nyingi hutokea pindi mtu anapofanya mazoezi, amnapoogelea ama anapofanya kazi.
Soma Zaidi...Huduma ya Kwanza kwa aliyeungua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua
Soma Zaidi...Chanjo zinazotolewa nchini Tanzania
Posti hii inahusu zaidi chanjo ambazo utolewa nchini Tanzania, ni chanjo ambazo uzuia Magonjwa ambayo yako katika sehemu mbalimbali za nchi.
Soma Zaidi...Dalili za unyanyasaji wa kimwili
Unyanyasaji wa kimwili. Unyanyasaji wa watoto kimwili hutokea wakati mtoto amejeruhiwa kimwili kimakusudi. Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa watoto kingono ni shughuli yoyote ya kingono na mtoto, kama vile kumpapasa, kushikana mdomo na sehemu
Soma Zaidi...Mambo yanayosababisha kupona kwa vidonda.
Posti hii inahusu mambo yanayochangia katika kupona kwa kidonda, ni mambo ambayo yapo kwa mgonjwa mwenyewe kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Zijue sehemu za mwili zinazochomwa chanjo.
Posti hii inahusu zaidi sehemu ambazo zinapaswa kudungwa chanjo, hizi ni sehemu zile zilizopendekezwa kwa ajili ya kuchoma chanjo kwa kadiri ya kazi ya chanjo.
Soma Zaidi...