Huduma ya Kwanza kwa mwenye kizunguzungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu mwenye kizunguzungu
HUDUMA YA KWANZA KWA MWENYE KIZUNGUZUNGU
Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa. Kizunguzungu kinaweza kuwa ni dalili ya tatizo flani kwenye afya ya mtu. Maradhi mengi yanahusiana na kizunguzungu, hivyo baada ya huduma ya kwanza na mgonjwa akawa hajambo ni vyema aende kituo cha afya akajuwe chanzo cha kizunguzungu:
Mtu mwenye kizunguzungu anaweza kujipa huduma ya kwanza mwenyewe. Vinginevyo anaweza pia kupata maelekezo kutoka kwa mtu aliye karibu naye kwani siku zote mgonjwa anakosa uwezo wa kujimilikia hasa kujipa huduma ya kwanza.
1.Kwanza mwenye kizunguzungu anatakiwa akae chini
2.Kama alikuwa akitembea ama alikuwa akifanya shuhuli yeyote anatakiwa aache na akae chini kabisa na wala asichchumae.
3.Akaechini kipolepole na katu asiharakishe
4.Kama kukaa chini hakutoshi ni vyema alale, kama anaona kama dunia inazunguka asilale kichalichali.
5.Kama anakiu mpe maji ya kutosha anywe
6.Akae sehemu iliyotuia, isiyo na fujo wala mwanga mkali wa taa ama jua
7.Ni vyema kama atapata usingizi walau kidogo
8.Kizunguzungu kikiondoka kwanza akae chini kipolepole na anapotaka kusimama asimame kipolepole na katu asitumie kitu ili kimsaidie kusimama kama fimbo
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 web hosting 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Ijue rangi za mkojo na maana zake katika mwili kuhsu afya yako
Posti hii inahusu zaidi rangi za mkojo na maana zake, hizi ni rangi ambazo uweza kutokea kwenye mkojo wa mtu mmoja na mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa magonjwa, chakula,na mtindo wa maisha inawezekana unywaji wa maji au kutokunywa maji.
Soma Zaidi...HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA KWIKWI
Kwikwi sio hatari sana kwa afya, lakini inaweza kuwa hatari zaidi kwa mu aliyefanyiwa upasuaji kwenye tumbo.
Soma Zaidi...Njia za kuzuia kiungulia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuzuia kiungulia
Soma Zaidi...Huduma ya Kwanza kwa aliyekazwa na misuli
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekazwa na misuli
Soma Zaidi...Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...