FAHAMU KUHUSU MAPACHA WANAOFANANA


image


Post hii inahusu zaidi watoto mapacha wanaofanana,ni watoto wanaozaliwa wakiwa wanaofanana kwa sura na hata group la damu huwa ni Moja.


Mapacha wanaofanana.

Ni mapacha ambao uzaliwa kutokana na yai Moja,kwa kwaida tunafahamu kwamba yai likitoka urutubishwa na mbegu na baadae mtoto anaweza kuzaliwa,ila Kuna Kipindi ambapo yai Moja likitolewa mbegu urutubishwa na baadae yai hilo upasuka na kutoa mtoto Zaidi ya mmoja na watoto hao kwa kawaida kwenye sehemu Moja na makuzi yao huwa ni kwa pamoja,kwa hiyo watoto hao ufanana sana kwa sura na pia huwa na kundi Moja la damu na wakati mwingine ni vigumu kuwatofatisha.

 

Kwa hiyo hawa watoto mapacha wanaofanana hawatokani na sababu za urithi kwa kuthani kwamba kama ukoo Fulani una mapacha wanaofanana ni lazima na watoto wengine kwenye ukoo huo huo kupata watoto mapacha wanaofanana,ila kwa mapacha wasiofanana inawezekana kwa hiyo ni mambo ya kibiologia na sio sababu za ki urithi,kwa hiyo watu wanapaswa kupata elimu kwa sababu Kuna watu wanatumia mbinu Ili kuweza kupata mapacha wanaofanana.

 

Kuna hadithi au simulizi mbalimbali ambazo usemwa na watu mbalimbali kuhusu mapacha wanaofanana kwamba akiugua mmoja na mwingine anaugua hata kama wako sehemu tofauti, kwa hiyo hii haijafanyiwa utafiti kuona kama ni kweli au vipi. Kwa hiyo kwa wale ambao wanapigana na kutumia mbinu mbalimbali Ili kuweza kupata mapacha wanaofanana ni vigumu kwa sababu wengine wanatumia hata na dawa mbalimbali Ili kupata mapacha wanaofanana ila kwa wasiofanana inawezekana,lakini kwa wanaofanana kwa kutumia dawa ni vigumu.

 

Kwa hiyo jamii inapaswa kuelimishwa na kuachana na matumizi ya dawa mbalimbali ambazo usadiki kwamba ukizitumia utapata mapacha wanaofanana.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    





Je una umaswali, maoni ama mapendekezo?
Download App yetu kuwasiliana nasi




Post Nyingine


image Fahamu kuhusu mapacha wanaofanana
Post hii inahusu zaidi watoto mapacha wanaofanana,ni watoto wanaozaliwa wakiwa wanaofanana kwa sura na hata group la damu huwa ni Moja. Soma Zaidi...