Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuhakiki Kama u-mjamzito
JE NITAHAKIKISHA VIPI KAMA NINA UJAUZITO?
Hili ni swali la msingi kabisa, maana unaweza kuwa na dalii za ujauzitio lakini si ujauzito, ama unaweza kuwa ujauzito lakini ukipima huoni kitu. Sasa nini tufanye. Njia pekee ya kuhakiki kama ni ujauzito ama sio ni kupima. Unaweza kutumia kipimo cha mkojo ukiwa nyumbani ama kwenda kupima hospitali.
Kama utatumia kipimo cha mkojo fika duka la dawa na hakikisha unapewa kipimo kilichokuwa hakiku expire. Pata maelekezo kutoka kwa uuzaji kama ni mara yako ya kwanza. Pia maelekezo utaweza kuyakuta kwenye hiko kipimo ila lugha inaweza usielewe. Kipimo hili kinafanya kazi kwa kuangalia uwepo wa kemikali ambazo huzaliwa wakati wa ujauzito. Endapo zitakuwepo kipimo kitaonyesha kuwa ni mjamzito.
Sasa ni muda gani unafaha kupima?Ni vyema kupia wiki mbili baada ya kukosa hedhi. Endapo utapima wiki moja baada ya kukosa hedhi ama utapima mapema zaidi kuna uwezekano kuwa hutapata majibu kama ni mjamzito. Hivyo inashauriwa sana kusubiri baada ya wiki mbili toka kukosa hedhi ndipo upime. Kama utakwenda kupima hospitali haina shida hata ukiwahi maana zipo njia nyingi wanaweza kutumia.
Nina dalili za uajauzito lakini nikipima sina?Hili ni katika maswali ambayo wanawake wengi wamekuwa wakiuliza. Inatokea anazo dalili zote za ujauzito lakini akipima hakuna kitu. Kuna sababu nyingi juu ya swala hili. Kabla ya kuendelea na somo hili zaidi, wacha nikufahamishe kuwa, yafuatayo yanaweza kusababisha usione ujauzito kwenye kipimo:-
1.Kama umepima mapema kabisa2.Kama kipimo ni kibovu3.Kama umekosea namna ya kupima4.Kama huna ujauzito5.Homoni za ujauzito hazipo za kutosha kwenye mkojo.
Hizi ni katika sababu tu zinazotokea hasa wakati wa kupima. Sasa wacha tuingie katika somo hili kitaalamu zaidi. Ni kwa nini unaweza kupata dalili za uajauzitio zilizotaja hapo juu lakini ukipima huna hata ujauzito?. nitaangalia hoja kuu tano za kutokea kwa hali hizi kama ifuatavyo:-
1.Kukosa HedhiKukosa hedhi ni dalili ya ujauzito, lakini haimaanishi kuwa ni lazima utakuwa mjamzito. Kwani mwanamke anaweza kukosa hedhi kwa moja ya sababu zifuatazo:-A.Uwiyano usiosawa wa homoni (hormene imbalance)B.MadawaC.Maradhi katika ovariD.Magonjwa kama ya PIDE.Misongo ya mawazoF.VyakulaG.Njia za uzazi wa mpango
2.Kuuma kujaa na kuvimba kwa matiti. Hii inaweza kuwa ni dalili ya ujauzito.akini pia hali hii inaweza kusababishwa na mambo kadhaa ambayo yanaweza yakakufanya uhisi ni mjamzito.kwa mfano:-A.Kuwepo kwa uvimbe kwa ndani (breast sore)B.Kuwepo kwa shida katika tishu za matiti (fibrocystic breast tissue)C.Kwa wakati mwingine mazoezi makali yanaweza kusababisha hali hii.D.Uvutaji wa sigaraE.Pia uwiyano mbaya wa homoni (hormone imbalany)
3.Maumivu ya kichwa na kichefuchefu yanaweza kusababishwa pia na sababu nyingine. Ijapokuwa inakadiriwa kuwa asilimia 70 ya kichefuchefu ni ujauzito. Mengine yanayoweza kusababisha ni misongo ya mawazo, vyakula, maradhi na vidonda vya tumbo, sumu katika vyakula na mengineyo.
4.Maumivu ya tumbo na kutokwa na damu kidongo (cramping and spotting). dalili hizi zinawezakufana na sana na mwanzoni mwa hedhi, dalili hizi hazimaanishi moja kwa moja utakuwa na ujauzito. Kwani huwenda pia zikasababishwa na uwiyano mbaya wa homoni (hormone imbalance), matumizi ya baathi ya njia za uzazi wa mpango, matumizi ya madawa, misongo ya mawzo, mashambulizi ya bakteria mwilini (PID) na maradhi yanayojulikana kama uterine fibrinoid.
5.Uchovu, nadhani hapa sina haja ya kuzungumza sana maana kila mtu anafahamu kuwa uchovu unaweza kusbabishwa na mambo mengi sana kama mazoezi, kazi, maradhi mengine.
Hivyo kama unapata dalili za ujauzito na kila ukipima hakuna kitu vyema kufika kituo cha afya kwenda kucheki vyema huwenda kuna kitu hakiko sawa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inakwenda kukupa njia za kukusaidia kuacha punyeto.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku ya 7 Hadi ya 14
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatari za kutokwa na damu wakati wa ujauzito, hali hii utokea wakati wa ujauzito ambapo Kuna baadhi ya wajawazito utokwa na damu jambo ambalo hatupaswi kutarajia kwa sababu tunafahamu kabisa mama akishapata ujauzito na damu zinakom
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya uzito kwa mjamzito, hii ni hali ya kubadilika kwa uzito kwa Mama akiwa na Mimba
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji, ni madhara madogo madogo ambayo utokea kwa watumiaji wa matatizo ya kupumua.
Soma Zaidi...Zijuwe dalili 17 za mimba na mimba changa, kuanzia siku ya kwanza mpaka mwezi mmoja
Soma Zaidi...Kuzaliwa kabla ya wakati humpa mtoto muda mdogo wa kukua tumboni. Watoto waliozaliwa kabla ya wakati, hasa wale waliozaliwa mapema, mara nyingi huwa na matatizo magumu ya matibabu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za mimba kutoka, hili ni tatizo ambalo linawakumba wanawake wengi ambapo mimba utoka kabla ya kumfikisha mda wake, kwa kawaida Ili kawaida mimba nyingi utoka zikiwa na miezi chini ya Saba au wengine wanaweza kusema kwamba mim
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia Faida za Uzazi wa mpango kwa watoto, mama, wanandoa, na jamii au JUMUIYA.
Soma Zaidi...