Post hii inahusu zaidi huduma ambayo Mama anapaswa kutolewa pindi mimba inapotishia kutoka huduma hii utolewa kulingana na Dalili tulizoziona zinazohusiana na mimba kutishia kutoka.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kujikumbushia kidogo kuhusu mimba Inayotishia kutoka , mimba ya aina hii utokea pale ambapo mjamzito utokwa na damu kidogo kidogo zinaweza kuwa kama za hedhi ila zinaweza kuwa kidogo lakini ni za mwendelezo au za mara kwa mara na hazikati na pengine Mama anakuwa Hana maumivu hata kidogo au pengine maumivu yanakuwepo ila ni kwa kiasi kidogo sana kwa hiyo mama baada ya kuona hayo anapaswa kuwahi hospital Ili kupata matibabu na kuokoa mimba isitoke. Kwa mjamzito wa namna hii tunapaswa kumpatia huduma zifuatazo.
2. Kwa kwaida Mama akiwa katika hali hii mara nyingi huwa na wasiwasi kwa hiyo anapaswa kutiwa moyo na kumhakikishia usalama na kumwambia ni shida gani iliyompata pia mama anapaswa kulala kitandani kwa wiki Moja bila kutembea huko na huku bila sababu , mjamzito anashauliwa kulala kwa Sababu kama Kuna sehemu yoyote imeachia ni rahisi kabisa kujirudia na kuwa kawaida kabisa na pia mjamzito kama amefuata mashariti haya kitu cha kwanza kabisa damu ambazo zilikuwa zinatoka zinakoma na kama mjamzito amefuata mashariti anakuwa vizuri ndani ya wiki Moja ,na pia mama kama ameambiwa kulala anapaswa kuelezwa wazi kwa nini amelala na pia aambiwe wazi kwamba akikosea mashariti anaweza kupoteza mtoto.
3. Pia Mama anapaswa kushauliwa au kuambiwa kabisa kuachana na tendo la ndoa anapopatwa na tatizo la namna hii,
Mama anapaswa kuachana na tendo la ndoa kwa sababu inawezekana kwenye sehemu ya mlango wa kizazi Kuna sehemu iliyolegea kwa hiyo mama akiendelea kufanya tendo la ndoa anasababisha sehemu Ile kulegea na kuendelea kuleta matatizo zaidi au kwa wakati mwingine baba akitoa mbegu na mbegu hizo mara nyingi Zina kichocheo ambacho kikichanganyika na kichocheo cha uchungu cha mama uweza kuanzisha uchungu na kusababisha mlango wa kizazi kufunguka na mtoto anaweza kutoka, kwa hiyo Mama mwenye tatizo hili anapaswa kuacha tendo la ndoa mpaka hapo atakapomaliza kujifungua. Pia na baba anapaswa kuelezwa wazi hali ya mke wake.
4. Pia kwa Kipindi hiki kwa sababu mama anaweza kuwa na mawazo au kwa sababu ya kulala kwa mda mrefu anaweza kukosa usingizi na kuwa na kishawishi cha kutembea akiwa amejificha na kusababisha madhara zaidi kwa hiyo ni vizuri mjamzito akionekana na wasiwasi na kutotulia apewe dawa za usingizi, na pia pengine mimba inawezekana kutishia kutoka kwa sababu ya kukosekana kwa baadhi ya vichocheo ambavyo usaidia kukua kwa mimba kwa hiyo mama anapaswa kupewa vichocheo mbalimbali,kwa kitaamu huiitwa progesterone hasa hasa kama Kuna ushaidi kwamba imepungua kwenye mwili wa mama
5. Ikitokea damu ikaacha kutoka hiyo ni dalili kubwa ya kwamba tatizo limepona na mama anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani lakina kwamashariti makubwa kati ya mtoa huduma za afya, mama na ndugu wa karibu hasa mme wake , kwa hiyo mama atapaswa kurudi klinic mara kwa mara Ili kuendelea kuangalia afya ya mama na mtoto, na kabla mama hajaondoka anapaswa kabisa kuangalia kama damu imeacha kutoka na watoa huduma wajihajikishie kwa sababu Kuna akina Mama ambao wamechoka kuishi hospital, na akina Mama wanapaswa kuwa wakweli na wawazi kuhusu afya zao na za watoto pia.
6. Pia tatizo likipona ni vizuri kutoa elimu ya kutosha kwa mama na ndugu Ili kuepuka Mila potofu ambazo zinaweza kuleta matatizo zaidi
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Mimba inaweza kutoka kutokana na maradhi, majeraha ama misukosuko mimgine. Kutoka kwa mimva haimaanishi ndio mwisho wa kizazi.
Soma Zaidi...Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoa mapema kabla ya mwenza kuridhika.
Soma Zaidi...Utajifunza sababu za maumivu ya uume na uke wakati wa tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa na matibabu yake.
Soma Zaidi...Post huu inahusu zaidi utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito, ni chakula anachopaswa kutumia na ambavyo hapaswi kutumia kwa Mama mjamzito mzito, kwa sababu Mama mjamzito anapaswa kuwa makini katika matumizi ya chakula ili kuweza kuongeza vitu muhimu mwil
Soma Zaidi...Ni kweli kuwa kutema mate mara kwa mara inaweza kuwa ni dlili za ujauzito. Lakini itambulije kuwa pekee sio kithibitishi cha ujauzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo anaweza kuzipata mwenye Ugonjwa wa tezi dume, sio Dalili zote mtu anaweza kuzipata kwa sababu dalili kama hizi zinaweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mathara yanayosababisha Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke
Soma Zaidi...SIKU YA KUPATA UJAUZITO Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote.
Soma Zaidi...