Post hii inahusu zaidi sababu za ugumba kwa wanawake, ni sababu ambazo upelekea wanawake wengi kuwa wagumba ukizingatia kuwa wanazaliwa wakiwa na uwezo kabisa wa kupata watoto lakini kwa sababu mbalimbali za kimazingira wanakoswa watoto, zifuatazo ni saba
Sababu za ugumba kwa wanawake.
1. Kwanza kabisa ugumba ni hali inayotokea ambapo mwanamke na mwanaume wanaishi kwa mwaka mmoja kwa kujamiiana pasipokutumia aina yoyote ya uzazi wa mpango lakini hawapati mtoto kwa kipindi cha mwaka huo mzima, kuna aina mbili za ugumba.Aina ya kwanza ni pale ambapo mwanaume na mwanamke wanapata moto mmoja na baadae hawapati kabisa na ya pili ni kwamba hawapati mtoto hata mmoja. Zifuatazo ni sababu za ugumba kwa mwanamke.
2. Kuaribika kwa mirija ambayo inasaidia katika mifumo mizima ya kusafirisha yai, kwa mwanamke kuna baadhi ya mirija ambayo usababisha kusafirisha yai wakati wa utungaji wa mimba, mirija hiyo ikiharibiwa ushindwa kupokea yai na kulifikisha sehemu usika, sababu za kuaribika kwa mirija inaweza kuwa ni maambukizi kwenye mirija hiyo au ni kwa sababu ya upasuaji kwa hiyo yai ushindwa kusafiri kutoka kwenye ovari mpaka kwenye follapian kwa ajili ya kurutubishwa.
3. Sababu nyingine ni kuwepo kwa matatizo kwenye mfuko wa uzazi, mfuko wa uzazi kawaida unapaswa kuwa na mazingira mazuri kwa ajili ya kumtunza mtoto, kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye mfumo wa uzazi pamoja na kuwepo kwa uvimbe mtoto hawezi kukua kwenye mfumo wa uzazi kwa hiyo kutibu maambukizi mapema ni vizuri ili kuepukana na tatizo hili la kukosa mtoto.
4.kuwepo kwa acid nyingi kwenye uke. Tunajua wazi kubwa kwenye uke kuna acidi ambayo inapaswa kutunza sehemu hiyo ila acidi ikiwa nyingi huwa inaua mbegu za kiume kwa hiyo acidi ya kwenye uke inapaswa kuwa nne na nusu kwa pH ikizidi hapo inaua mbegu kwa hiyo pakitokea tatizo la ugumba ni vizuri kupima kiwango cha acidi kwenye uke ili kupunguza tatizo la ugumba.
5. Kuwepo kwa ute mzito kwenye uke na cervix, tujue wazi kubwa kwenye uke kwa kawaida huwa kuna ute, ikitokea uke huo kubwa mzito usababisha mbegu kushindwa kupita na kulifikia yai kwa ajili ya kurutubishwa kwa hiyo tunapaswa kuangalia na tatizo la ute endapo kama kuna tatizo la ugumba na kuweza kutumia dawa za kurainisha ute na mbegu zinaweza kupita kwa urahisi.
6. Kuwepo kwa maambukizi kwenye via vya uzazi, tukumbuke kubwa via vya uzazi ni pamoja na uke, cervix na tumbo la uzazi hizi sehemu zikishambuliwa na Maambukizi ni vigumu kupata uja uzito. Hasa maambukizi yatokanayo na ngono zembe kwa hiyo tunapaswa kupima na kutibu mara moja Magonjwa haya ili kuweza kuondoa wimbi hili la ugumba kwa wanawake.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni
Soma Zaidi...Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume.
Soma Zaidi...Unaweza kutaka kujuwa je naweza kupata dalili za mimba baada ya siku nne toka ujauzito kutungwa? ama baada ya siku nne toka kushiriki tendo la ndoa. Makala hii itakwenda kujibu maswali haya na mengineyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala ya fangasi wa uumeni
Soma Zaidi...Inatakiwa angalau nafasivkati ya mtoto na mtoto wapishane miaka miwili.
Soma Zaidi...ukiwa na ujauzito unaweza kuona mabadiliko mengi katika mwili wako yakiwemo kutokwa na majimaji. je majimaji haya yana dalili gani kwenye ujauzito?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye Matiti kwa Mama mjamzito, hali hii utokea pale ambapo mama akibeba mimba Kuna mabadiliko kwenye Matiti kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba na dalili za siku hizo.
Soma Zaidi...Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto.
Soma Zaidi...