Somo hili linakufundisha maana ya HTML, kwa nini inatumika, na jinsi ya kuandaa simu au kompyuta yako kwa ajili ya kuanza kutengeneza tovuti. Pia tutatengeneza ukurasa wetu wa kwanza wa HTML hatua kwa hatua.
HTML ni lugha ya msingi inayotumika kutengenezea kurasa za tovuti na blogu. Bila HTML hakuna website inayoonekana duniani. Unaweza kutengeneza tovuti kwa kutumia HTML pekee, kisha ukaboresha baadaye kwa kutumia CSS na JavaScript.
Katika somo hili, tunaanza kwa kukuweka tayari ili uweze kuandika code zako bila shida—iwe unatumia simu au kompyuta.
HTML ni ufupisho wa:
Hypertext
Markup
Language
Ni lugha ya kimataifa inayotumiwa kutengeneza kurasa za tovuti (website pages). HTML haihitaji umiliki wa vifaa ghali; unaweza kuanza hata kwa kutumia simu yako ya mkononi.
Ikiwa una ndoto za kuanzisha blog, tovuti ya biashara au portfolio, basi uko mahali sahihi. Mafunzo haya yatakufundisha kuanzia hatua ya mwanzo kabisa hadi kutengeneza tovuti inayoweza kwenda live.
Ili uweze kufanikiwa kwenye kozi hii, unahitaji:
Simu ya smartphone au kompyuta
Uwezo wa kusoma na kuandika
Utayari wa kujifunza
Umakini na ujanja
Kufanya mazoezi kila baada ya somo
Kozi ya msingi (Basics) itachukua wiki moja, kisha tutaendelea na hatua ya pili.
Kwa watumiaji wa simu, utatumia app inayoitwa Acode (badala ya TrebEdit kwa sababu Acode ni nyepesi na ya kisasa).
Pakua app ya Acode kwenye Play Store:
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.foxdebug.acodefree
Fungua Acode
Bofya icon ya “folder” kisha tengeneza folder jipya
Lipe jina mfano: html-project
Ndani ya hilo folder, tengeneza folder lingine liitwe images
Rudi kwenye folder la html-project
Bonyeza alama ya “+” kutenge">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tunakwenda kugawanya tag za HTML, pia nitakwenda kukuletea tag 70 za HTML
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuweka style mbalimbali kwenye ukurasa wa html
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunz ajinsi ya kutengeneza cheti kwa kutumia html na css.
Soma Zaidi...Katika somo somo hili utajifunza maana ya code, tag na mpangilio wa faili la HTML
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na saratani
Soma Zaidi...Katika somo hili nitakuletea orodhabya tag 25 za html ambazo hugumiwa katikabuandishi.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz ahatuwa kwa hatuwa jinsi ya Kuunganisha HTML na CSS au JavaScript
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuweka menyu kwenye faili la html na kuweka rangi ya background. Pia utajifunza kufanya ukurasa uwe responsive yaani uendani na ukubwa wa kifaa.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza sehemu muhimu katika faili la HTML kama vile tag, attribute na element
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu sehemu kuu za faili la HTML
Soma Zaidi...