image

HTML - somo la 7: Vitu vya kuzingatia unapoandika HTML

Katika somo hili utajifunza sehemu muhimu katika faili la HTML kama vile tag, attribute na element

HTML  NI NINI?

HTML ni katika lugha za kikompyuta iliyopo katika kundi la markup language. Tofauti na watu wengi wanavyodhani kuwa HTML ni programming language. Hii si sahihi, kwa kuwa HTML imekosa sifa ya kuwa logic hivyo haiwezi kuwa programming language. HTML ni kifupisho cha HyperText Markup language. Lugha nyingine zilizo katika kundi hili ni pamoja na css amyao tutakuja kuisoma kwenye muendelezo wa mafunzo haya?

 

Karibia tovuti zote zinakuwa na HTML. Hivyo HTML ni moja katika lugha zinazotumika kwa wingi katika kutengeneza kurasa za wavuti (web pages). tovuti ya kwanza kuanzishwa duniani ilitoshelezwa na HTML . cheki link hii kufunguwa website ya kwanza duniani World first website http://info.cern.ch/hypertext/WWW/TheProject.html

 

 

HISTORIA FUPI YA HTML:

HTML kwa mara ya kwanza ilianzishwa na Tim Berners-Lee, Robert Cailliau na wengineo mwaka 1989. maana halisi ya hypertext ni kuwa faili linaruhusu kuwa na link (kiungo) ambayo unaweza kuhama kutoka ukurasa mmoja kwenda mwengie. Na maana ya Markup Language ni ile hali ya ambayo maandishi kuchakatwa na kuonekana katika mpangilio mzuri. Kufanya hivi unatakiwa utumie tag na attributes. Kutoka miaka hiyo mpaka sasa html imetolewa katika matoleo mengi na sasa tupo katika toleo la 5 yaani html5.

 

MPANGILIO WA FAILI LA HTML.

Faili la HTML lina sehemu kuu tatu ambazo ni:-

1. Kutaja aina ya faili.

2. Head

3. Body

 

Ukiangalia code hizo hapo juu mwanzoni kabisa kumeanza na code hii <!DOCTYPE html> hii ndio sehemu kuu ya kwanza ya faili la HTML na kazi yake ni kutambulisha aina ya faili. Hapo mwanzo ilikuwa inatajwa na toleo la HTML lakini kwa sasa si lazima na huchukuliwa kuwa I html5.

 

Kisha sehemu ya pili ni head ambayo imeanza na <head> na kumaliziwa na </head>. ndani ya tag hizi mbili ndipo zinakaa taarifa muhimu zinazolihusu faili hilo. Nyingi katika taarifa hizi hazionekani na mtumiaji wa tovuti hiyo. Taarifa hizi ni kama link, icon, na title. Kwa kiasi kikubwa taarifa znazopatikana hapa ni zile zinazoitwa metadata ni taarifa ambazo hazipo kwa ajili ya msomaji ama mtumiaji wa website husika, hizi zipo kwa ajili ya ingini pekuzi na kufanyia SEO. HIVYO KWENYE <head> kuna metadata na taarifa nyingine.

 

Kisha baada ya head inafata <body na mweisho imemaliziwa na </body>. hapa ndipo ambapo utaweka taarifa zote unazozitakazikae kwenye faili lako. Yaani maudhui ya huo ukurasa yanakaa hapa. Na watumiaji wa website hiyo watasoma maudhui hayo.

 

 

VITU VINAVYOUNDA FAILI LA HTML

Faili la HTML linaundwa kwa vitu vikuu viwili ambavyo ni TAG na ATTIBUTE. Hata hivyo unatakiwa ujuwe kuwa tag na attribute kwa pamoja huunda Element. Hivyo kabla hatujaenda mbele zaidi tutaona maa na ya hivi vitu vitatu.

 

 

<!DOCTYPE html>

<html>

<head>

<title>My First Webpage</title>

<meta charset="UTF-8">

<meta name="description" content="This is my first website">

</head>

<body>

<h1>Welcome to my webpage</h1>

<p>Welcome to my brand new website.</p>

<a href="http://www.google.com">Google</a>

</body>

</html>

 

 

 

TAG

Katika HTML tag hufafanuliwa kama seti ya herufi zinazounda amri iliyoumbizwa kwa ukurasa wa Wavuti. Tag ni kama chombo cha kubebea code za HTML. Code zote huandikwa kwa tag. Hapo zamani code zote katika kutengeneza ukurasa wa wavuti zilitumia tag, ijaokuwa siku hizi baadhi ya sehemu akuna haja ya kutumia tag.

 

Tag hutumika katika html kwa ajili ya kuanzia kuandika elment, na kawaida tag zinakuwa na za kufungulia ambazo huanzwa na < kisha inakuwa na ya kufungia ambayo huazwa na </. mfano  wa tag ni kama huu <h1>hello</h1> hapo <h1> ni tag ya kufungulia na </h1> ni tag ya kufungia. 

 

Katika code zilizoonyeshwa hapo juu  mifano ya tag za kufungua ni <html>, <head>, <tittle>, <meta>, <body>, <h1>, <p> na <a>. mifano ya tag za kufunga ni </head>, </title>, </h1>, </p">...



Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 249


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Jinsi ya kutengeneza cheti kwa kutumia HTML
Katika post hii utakwenda kujifunz ajinsi ya kutengeneza cheti kwa kutumia html na css. Soma Zaidi...

HTML - somo la 9: Jinsi ya kutumia tag za HTML katika uandishi wa maudhui
Katika somo hili utakwenda kuona jinsi ya kuzitumia tag balimbali za html Soma Zaidi...

haloo word
all haloo Soma Zaidi...

HTML - somo la 13: Jinsi ya kugawa ukurasa wa HTML
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kugawanya ukurasa wa HTML katika column Soma Zaidi...

HATML - somo la 4: Jinsi ya kutumia tag za html
Katka somo hi utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia tag za html ili kupangilia muonekano wa maudhui Soma Zaidi...

HTML - somo la 3: Tags za HTML zinazotumiwa katika uandishi
Katika somo hili nitakuletea orodhabya tag 25 za html ambazo hugumiwa katikabuandishi. Soma Zaidi...

HTML - somo la 8: Mgawanyiko wa Tag za HTML na kazi zake
Katika somo hili tunakwenda kugawanya tag za HTML, pia nitakwenda kukuletea tag 70 za HTML Soma Zaidi...

HTML - somo la 16: Jinsi ya ku host website bure
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku host website yako bila malipo Soma Zaidi...

HTML- somo la 2: Kazi za HTML, code na tag kwenye website.
Katika somo somo hili utajifunza maana ya code, tag na mpangilio wa faili la HTML Soma Zaidi...

HTML - somo la 14: Hatua za kutengeneza website
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza website hatuwa kwa hatuwa Soma Zaidi...

HTML-somo la 5: Jinsi ya kupangilia munekano wa maudhui kwenye website
Katika somo hili utajifunza Kuweka picha Kuweka rangi Kuweka linki Kupangilia position na alignment ya maandishi Kuongeza ukubwa wa herufi Kukoment Soma Zaidi...

HTML - somo la 7: Vitu vya kuzingatia unapoandika HTML
Katika somo hili utajifunza sehemu muhimu katika faili la HTML kama vile tag, attribute na element Soma Zaidi...