Katika somo somo hili utajifunza maana ya code, tag na mpangilio wa faili la HTML
Karibi tena kwenye mafunzo ya HTML na hili ni somo la pili. Kama hujalipata somo la kwanza tumia linki itakayopatikana mwisho wa posti hii ili uweze kulipata somo la kwanza.
Somo la kwanza utalipata kwa link hii https://web.facebook.com/groups/androbongo/permalink/568341711186808/
HTML ni nini?
HTML ni kifupisho cha maneno Hypertext Markup language. Hii ni moja ya lugha za kikompyuta yaani computer language. Ni moja katka lugha za kikompyuta zilizo rahisi sana na ni rahisi kuelewa. Pia matumizi yake ni mara nyingi tumekuwa tukikutana nayo kwenye mitandao.
Je HTML ina kazi gani?
Kazi kuu ya HTML ni kutengeneza kurasa za website (tovuti) na blog. Kwa mfano ukurasa wa facebook wenyewe una mchanganyiko wa code za HT,L na lugha nyingine za kikompyuta. Siku hizi HTML inaweza kutumika hata katika kutengenezea App za simu na software za kompyuta (desktop App).
Je code ni nini?
Code ni maandishi yanayobeba maelekezo ambayo hupewa kompyuta maelekezo hayo ili iweze kufanya shughuli fulani. Lugha zote za kikompyuta hutumia code. Hivyo HTML kwa kuwa ni mojaya lugha za kikompyuta nayo hutumia code, kama ulivyoona kwenye somo lililotangulia.
Je HTML ni programming language.
Hapana HTML ni Markup Language, haiingii kwenye programming language kwa sababu sio logic.
HTML inafanyaje kazi kwenye blog ama website?
Je naweza kutengeneza blog ama website mwenyewe kwa kutumia HTML pekee?
Ndio unaweza kutengeneza website (tovuti) kwa html tu na ikawa live na watu wakaitembele. Ila kwa blog, sirahisi utahitajika uchanganye na lugha nyingine za kompyuta kama php ilikupata dynamic page yaani kurasa ambazo zinauwezo wa kufanyiwa update kama kupost, kukoment na kulike n.k
Ni nni ukomo wa mafunzo haya?
Ukomo wa mafunzo haya ni kukuwezesha kujifunza HTML, kwa simu yako, uweze kutengeneza website ama kurasa za mtandao kwa simu yako na kuziweka live yaani kuhost. Mafunzo haya yote ni bure na yatakuwa katika hatua kwa hatuwa. Hatuwa ya kwanza ndio hii imeanza na itachukuwa wiki moja. Kisha itafata ya pilie
Endelea na somo……..
TUANZE SOMO LETU HAPA:
Kwa kuwa umeshajifnza mambo adhaa. Pia umeweza kuandaa simu yako ili kuweza kuendana na somo. Sasa somo letu litaanzia pale ulipo ishia kwenye somo lililopita. Kwanza funguwa App yako TrebEdit, ingia menu kisha workplace kisha bofya jina la project uliotengenez jana. Kisha bofya, utakutana na faili lako la index.html. Bofya hilo faili hapo code za HTML zitafunguka. Kama tumekwenda pamoja, code ambazo ulipest katika somo lililotangulia ni hizi hapa chini:-
<!DOCTYPE html>
<html lang="en">
<head>
<meta charset="utf-8">
<title>Home Page</title>
</head>
<body>
<h1>Mafunzo ya HTML</h1>
<h2><u>Jifunze bure</u></h2>
<p>Haya ni mafunzo ya HTML kwa kutumia simu</p>
<br><br><br><h2>
<i>From <br>Bongoclass</i>
</body>
</html>
Kama unatumia PC kopi hizo code kisha pest kwenye notepad kisha sevu index.html
MPANGILIO WA FAILI LA HTML
1.Sehemu kuu mbili za ukurasa wa HTML
Faili la HTML lina sehemu kuu mbili ambazo ni <head> na <body>. Katika sehemu hii ya <head> ndipo ambapo panakaa taarifa muhimu kuhusu faili lako, ikiwepo kichwa cha habari ama maudhui au title hii huwakilishwa na <title>, pia katika sehemu hii ya <head> kukaa taarifa zingine kama icon, link, icon, muadndishi, muhutasari kuhusu maudhui na nyinginezo.
Taarifa hizi mara nyingi hazionekani kwa watumiaji wa mtandao huo, kwani hazibebi maudhui ila zinabeba mpangilio. Katika taarifa hizi chache kuonekana na watumiaji wa mtanda kwa mfano icon na title.
Sehemu ya pili ni <body>. sehemu hii ndio hubeba malengo ya ukurasa huo. Sehemu hii dio ambayo mtumiaji wa mtandao atakutana nayo na kuvinjari. Kama unataka kuandika ukurasa wa website unaohusu faida za hewa, basi maudhui yako utayaweka kwenye sehemu hii.
Ukiangalia kwa ukaribu code hi">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunza Kuweka picha Kuweka rangi Kuweka linki Kupangilia position na alignment ya maandishi Kuongeza ukubwa wa herufi Kukoment
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku host website yako bila malipo
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kugawanya ukurasa wa HTML katika column
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kijifunza kuhusu HTML attributes na jinsi ambavyo zinafanya kazi
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuweka style mbalimbali kwenye ukurasa wa html
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza website hatuwa kwa hatuwa
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz ahatuwa kwa hatuwa jinsi ya Kuunganisha HTML na CSS au JavaScript
Soma Zaidi...Katka somo hi utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia tag za html ili kupangilia muonekano wa maudhui
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunz ajinsi ya kutengeneza cheti kwa kutumia html na css.
Soma Zaidi...