image

Historia ya Nabii Shu'aib

atika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Shu'aib katika Quran

HISTORIA YA NABII SHU’AYB(A.S)

Nabii Shu’ayb(a.s) alitumwa kwa watu wa Madian waliokuwa wakikaa pande za pwani ya Shamu (Syria). Watu hawa walikuwa wafanyabiashara wakubwa wa zama hizo. Mji wao ulikuwa katika njia kuu (Highway) ya misafara ya biashara kutoka sehemu mbali mbali za Mashariki ya kati kuelekea pwani ya bahari ya Mediterranean.


 

Tabia ya watu wa Madian


Wamadian pamoja na kuwa wafanyabiashara mashuhuri walikuwa na tabia ya kupunja vipimo wakati wa kuuza. Pia walikuwa wababe wakifanya uharibifu katika ardhi, walikuwa majambazi wakipora na kunyang’anya watu mali zao. Vile vile walikuwa washirikina na kuzuia watu kufuata Dini ya Allah(s.w).

 

Ujumbe wa Nabii Shu’ayb kwa Watu Wake


Nabii Shu’ayb(a.s) kama walivyofanya Mitume waliomtangulia aliwanasihi watu wake kumwamini na kumuabudu Allah(s.w) ipasavyo katika maisha yao ya kila siku na kusimamisha uadilifu katika jamii.


 


Na kwa watu wa Madian (tulimpeleka) ndugu yao, Shuaibu. Akasema: “Enyi watu wangu! Mwabuduni Mwenyezi Mungu, nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Msipunguze kipimo (cha vibaba) wala (cha) mizani. Mimi nakuoneni mumo katika hali njema (basi msiiharibu kwa kufanya dhulma).Nami nakukhofieni adhabu ya siku (kubwa) hiyo itakayokuzungukeni.” (11:84)


 

Nabii Shu’ayb(a.s) aliendelea kuwaasa watu wake:

“Wala msikae katika kila njia kuogopesha (watu) na kuwazuilia na Dini ya Mwenyezi Mungu (wale) wenye kuamini, na kutaka kuipotosha Na kumbukeni mlipokuwa wachache, Naye akakufanyeni kuwa wengi (sasa).Na tazamneni jinsi ulivyokuwa mwisho wa waharibifu.” (7:86)HISTORIA YA NABII

 

Mbinu Alizozitumia Nabii Shu’ayb(a.s) Katika Kufikisha Ujumbe Wake


Katika kuwafikishia ujumbe watu wake,Nabii Shu’ayb alifanya yafuatayo:


 

Kwanza, kuwafahamisha watu wake kwa uwazi kuwa yeye ni
Mtume wa Allah(s.w) aliye mfano wa kuigwa:


 


Akasema: “Enyi watu wangu! Mnaonaje kama ninayo dalili inayotokana na Mola wangu na ameniruzuku riziki njema (ya Utume) kutoka kwake (nitaacha haya, nishike upotofu wenu)? Wala sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayokukatazeni. Sitaki ila kutengeneza, kiasi ninavyoweza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu (Mwenyewe). Kwake ninategemea, na Kwake naelekea.” (11:88)


 

Pili, aliwahofisha adhabu kali ya Allah(s.w) iwapo watakataa kumwamini na kumfuata.

Na kwa Madiani (tulimtuma) ndugu yao, (Nabii) Shu’ayb, naye akasema: “Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu na iogopeni siku ya akhera wala msende katika ardhi mkifisidi.” (29:36)


 

Tatu,aliwatahadharisha watu wake na adhabu ya Allah(s.w)
iliyowafika kaumu zilizopita za akina ‘Ad, Thamud na kaumu Lut.


 

“Na enyi watu wangu! Kukhalifiana nami kusikupelekeeni yakakusibuni kama yaliyowasibu watu wa Nuh au watu wa Saleh na watu wa Luti si mbali nanyi.” (Karibuni hivi wameangamizwa; na nchi zao ziko karibu na nyinyi pia). (11:89)


 

Nne, aliwatumainisha watu wa Madian kuwa endapo wataomba msamaha kwa Allah(s.w) na kutubu juu ya makosa yao, Allah(s.w) atawasamehe na kuwaepusha na balaa lililowafika watu wa kaumu za Mitume waliotangulia.


 

“Na ombeni msamaha kwa Mola wenu (kwa yaliyopita), kisha tubuni kwake . Hakika Mola wangu ni Mwenye kurehemu na Mwenye kuwapenda (waja Wake).” (11:90)


 

Tano, aliwaonyesha msimamo na utegemezi wake juu ya
Allah(s.w).

“Na enyi watu wangu! Fanyeni (mtakayo) kwa tamkini yenu; na mimi pia ninafanya (yangu kwa tamkini yangu). Karibuni hivi mtajua ni nani itakayemfikia adhabu ifedheheshayo na ni nani aliye muongo. Na ngojeeni; mimi pia ninangoja pamoja nanyi.” (11:93)


 

“Bila shaka tumemtungia Mwenyezi Mungu uwongo ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Mwenyezi Mungu kutuokoa nayo. Wala haiwi kwetu sisi kurejea mila hiyo. Lakini akitaka (jambo) Mwenyezi Mungu, Mola wetu, (huwa). Mola wetu amekienea kila kitu kwa ilimu yake. Kwa Mwenyezi Mungu tunategemea. Mola wetu! Hukumu baina yetu na baina ya wenzetu (hawa) kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanaohukumu.” (7:89)

 

Vitimbi vya Wapinzani Dhidi ya Ujumbe wa Nabii Shu’ayb(a.s)

Kama ilivyokuwa katika kaumu zilizotangulia, waliomuamini Shu’ayb(a.s) na kufuata nasaha zake walikuwa watu wachache tu katika jamii yake. Wengi wao walikaidi mafundisho ya Mtume wao wakiongozwa na wakuu wa jamii. Katika kumkanusha Mtume wao walitumia mbinu mbali mbali.


 

Kwanza, walitumia vitisho
Wakuu waliotakabari katika kaumu yake wakasema: “Ewe Shu’ayb! Tutakutoa wewe na wale walioamini pamoja nawe katika mji wetu, au mrejee katika mila yetu.” Akasema: “Je, ingawa tunaichukia?” (7:88)


 

Pili, walitumia mbinu ya kuwakatisha watu tamaa

Na wakuu waliokufuru katika kaumu yake wakasema: “Kama nyinyi mkimfuata Shu’ayb, hapo bila shaka mtakuwa wenye kukhasirika.” (7:90)


 

Tatu,walimdhihaki Mtume wao.

Wakasema: Ewe Shuaibu! Swala zako zinakuamrisha tuyaache yaliyokuwa wakiyaabudu baba zetu au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Bila shaka wewe ni mwenye akili na mnyoofu (11:87)


 

Nne, walitumia mbinu ya kumdhalilisha.

Wakasema: “Ewe Shu’ayb! Hatufahamu mengi katika hayo unayoyasema. Na sisi tunakuona mdhalilifu kwetu. Lau kuwa si jamaa zako tungekupiga mawe, wala wewe si mtu mtukufu kwetu! (ila tunachunga hishima ya jamaa zako tu).” (11:91)

 

Kuangamizwa Waovu na Kuokolewa Waumini


Baada ya kuonywa wasionyeke, Allah(s.w) aliwaangamiza kama walivyoangamizwa akina Ad, Thamud, n.k.


 

Basi mtetemeko wa ardhi uliwatoa roho zao, wakawa wasiojimudu, (wamekufa) humo mjini mwao. Wale waliomkadhibisha Shu’ayb wakawa kama kwamba hawakuwako (mahala hapo). Wale waliomkadhibisha Shu’ayb ndio waliokuwa wenye khasara. (7:91-92)


 

Na ilipokuja amri yetu, tulimuokoa Shu’ayb na wale walioamini pamoja naye kwa rehema yetu. Na wale waliodhulumu ukelele (wa adhabu) ulinyakuwa roho zao. Wakawa majumbani mwao wametulia tu (wamekufa).(11:94)


 


Kama kwamba hawakuwamo humo. Sikilizeni. Wameangamia (watu wa) Madiana kama walivyoangamia (kina) Thamudu. (11:95)

Kwa mujibu wa aya hizi, watu wa Madian waliangamizwa kwa ukelele ukifuatiwa na tetemeko la ardhi. Tukikumbuka kuwa:


 

Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu; Mwenye hikima. (48:7)

 

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Shu’ayb(a.s).


 

Kutokana na kisa cha Nabii Shu’ayb(a.s) tunajifunza yafuatayo:


 

(i) Waislamu tunadhima ya kusimamisha uchumi halali katika jamii pamoja na kuamrisha mema na kukataza maovu kwa ujumla.


 

(ii) Tusimchelee yeyote katika harakati za kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii.


 

(iii) Tukisimama kidete kuifuata na kuisimamisha Dini ya Allah (s.w)katika jamii Allah(s.w) atatunusuru na kuthubutisha miguu yetu juu ya makafiri.


 

(iv) Waislamu wakijizatiti kusimamisha Uislamu katika jamii watawashinda makafiri pamoja na nguvu kubwa za kiuchumi na kijeshi walizonazo.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-06-27 13:53:00 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 34


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 02
Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu
Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Sulaiman(a.s)
Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a. Soma Zaidi...

Jifunze historia ya uislamu toka mitume na manabii, kuja kwa makhalifa na maimamu hadi leo
Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUJENGWA UPYA KWA AL-KA'BAH (NYUMBA TUKUFU YA ALLAH)
KUJENGWA UPYA KWA AL-KA’ABAHItambulike kuwa Al-ka’abah ndio mjengo wa kwanza kujengwa duniani. Soma Zaidi...

tarekh 5
KUZALIWA KWA MTUME (S. Soma Zaidi...

Nasaba ya Mtume Muhammad S.A.W na familia yake.
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 1 Soma Zaidi...

Historia ya Luqman mtu aliyesifika kuwa na Hikma
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma. Soma Zaidi...

KIKAO CHA KUMFUKUZA MTUME MUHAMMAD KUTOKA MAKKAH (MAKA), KIKAO ALICHOHUDHURIA IBLISI
KIKAO CHAKALIWA KUJADILI HATMA YA MUHAMMAD KATIKA MJI WA MAKAHiki ni kikao kizito hakijapata kutokea toka muhammad katika ji wa maka. Soma Zaidi...

Uendeshaji wa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nasaha za Lut(a.s) kwa Watu Wake
Nabii Lut(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII NUHU
Soma Zaidi...