Navigation Menu



Histora ya Nabi Zakariya

Katika somo hili utakwenda ujfunza kuhusu hslistoria ya Nabi Zakariya

HISTORIA YA MTUME ZAKARIA(A.S) 
Nabii Zakaria(a.s) ni miongoni mwa mitume wa Bani Israil (Mayahud) na anatokana na kizazi cha Nabii Sulaiman(a.s). Alikuwa mwangalizi mkuu wa nyumba ya Ibada na alikuwa anapta riziki yake kwa kazi ya useremala.


 


Zakaria(a.s) Kumlea Marymam na Kuomba Mtoto Mwema Zakaria(a.s) alichaguliwa na ukoo kumlea Maryamu, mama yake Nabii Issa(a.s). Alimlea vyema katika malezi ya kiislamu.

Katika kumlea Marymu, Zakaria(a.s) siku moja alishangaa kumkuta Maryam binti Imraan na vyakula mezani ambavyo hakumpa yeye, ikabidi amuulize:-

“.........Ewe Maryam! unapta wapi hivi ? Akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu” (3:37)


 

Jibu hili la Maryamu lilimsisimua na kumuhamasisha Mzee Zakaria kiasi cha kumfanya naye amuelekee Mola wake na kumuomba mtoto mwema atakaye mrithi katika ucha-mungu na kusimamisha Dini ya Allah(s.w) katika jamii. Zakaria(a.s) alimuelekea Mola wake na kulalama.

 

Akasema: “Mola wagu. Bila shaka mifupa yangu imekuwa dhaifu na kichwa kinawaka (kinan’gara) kwa mvi,wala sikuwa mweye bahati mbaya (mwenye kukhasirika) Mola wangu, kwa kukuomba wewe. Na hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu(kuharibu Dini). Na mke wangu ni tasa. Basi nipe mrithi (anijie) kutoka kwako. Atakaye nirithi na kuwa na kuwarithi(wazee wake wengine)kizazi cha Ya‘aquub. Na umfanye, Mola wangu mwenye kukuridhisha”(19:4-6)


 

Yahya(a.s) Jibu la Dua ya Mzee Zakaria(a.s)

Dua ya Zakaria(a.s) ilijibiwa kwa kubashiriwa kupata mtoto, Yahya (Akaambiwa): “Ewe Zakaria! Tunakupa habari njema ya (kuwa utazaa)mtoto, jina lake ni Yahya: Hatujafanya kabla yake aliye na jina namna hilo.” (19:7)


 

Yahya(a.s) Kupewa Utume


Alizaliwa mtoto Yahya na kupewa utume akingali mtoto na akainukia kuwa mtu mwema kwa wazazi wake na kwa walimwengu wote kwa ujumla. Alijitoa muhanga kwa ajili ya kulingania Dini ya Allah(s.w).


 


“Ewe Yahya! kishike kitabu (hiki unachopewa) kwa hima kubwa.” Na tulimpa hikima angali mtoto. Na (tukamfanya ni) huruma kutoka kwetu, na utakaso na akawa mcha-Mungu. Na mwema kwa wazazi wake wala hakuwa jeuri ,asi. Na amani ilikuwa juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyokufa na siku atakayofufuliwa hai.(19:12-15)

Nabii Zakaria na Yahya(a.s),wote waliuliwa na Mayahud.

 

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Zakaria(a.s) na Yahya(a.s)

Kutokana na Historia ya Nabii Zakaria (a.s) na Yahya (a.s)
tunajifunza yafuatayo:

(i) Tuwe makini katika kulea watoto wetu hasa mabinti – Binti akileleka vizuri atakuwa ni chimbuko la malezi bora katika jamii.


 

(ii) Tusichoke kumuomba Allah(s.w) jambo lolote la msingi tunalohitajia kwa ajili ya kusimamisha Uislamu na kuendeleza wema katika jamii – Hapana linaloshindikana kwa Allah(s.w).


 

(iii) Waumini wanaharakati wa kusimamisha Uislamu katika jamii, waombe watoto wema watakaorithi harakati za Kiislamu na kuziendeleza kwa ari na hima zaidi.


 

(iv) Ili watoto wetu waweze kuwa wanaharakati wazuri, hatunabudi sisi wenyewe kuwa mfano mwema wa kuigwa kama alivyokuwa mzee Zakaria(a.s) na kisha tuwafunz kwa kina elimu sahini ya Uislamu inayotokana na Qur-an na Sunnah na tuwape kwa upana elimu ya mazingira.


 

(v) toto anayependeka mbele ya Allah(s.w) ni yule anayewafanyia wema wazazi wake kisha kuifanyia wema jamii. Mtu hawezi kuwa mwema kwa jamii yake endapo ameshindwa kuwatendea wema wazazi wake waliomzaa na kumlea kwa taabu.


 

(vi) Kila mtoto anazaliwa katika amani, (katika Uislamu). Atabakia kuwa katika amani mpaka kufa kwake
na kufufuliwa kwake endapo tutamlea Kiislamu naye akaendelea kubakia kuwa Muislamu mtendaji mwenye kufanya jitihada za makusudi za kusimamisha Uislamu katika jamii baada ya baleghe yake mpaka kufa kwake.

 

 

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-06-27 16:56:30 Topic: visa vya Mitume Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 323


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Historia ya Nabii Shu'aib
atika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Shu'aib katika Quran Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Ibrahimu
Katika post hii utakwenda kujifunza historia ya Mtume Ibrahim katika quran Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Al-yasa’a
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Mtume Al-yasa'a Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Lut
Katika somo hili utakwenda kujifunza historia yaMtume Lut kutoka katika Quran Soma Zaidi...

hHistoria ya Nabii Dhul-kifl
Katika makala hii tutakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Dhul-kifl Soma Zaidi...

Hstoria ya Nabii Yusuf
Katika makala hii utakwenda ujfunzakuhusu historiaya Nabii Yufuf katika Quran Soma Zaidi...

Historiaya Nabii Isa
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Historia ya Nabii Isa Soma Zaidi...

Hstora ya Nabii Adam
ata post h utawenda ujfunza hstora ya Nabii Adam ulngana na Quran navyoeleza Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Ismail katika quran
KKatika somohili utakwenda kujifunzahistoriaya Mtume Ismail Mtoto wa Nabii Ibrahim Soma Zaidi...

Hstoria ya Nabi Daud
Katika somo hili utawenda ujifunza uhusu historia ya Mtume Daud Soma Zaidi...