image

Historia ya Mtume Swaleh (Salih)

Katika post hii utakwenda kujifunza historia ya Mtume Swalehe katikaQuran

HISTORIA YA NABII SALIH(A.S)

Utangulizi:

Thamud walikuwa ni muungano wa kikabila katika eneo la kaskazini-magharibi mwa Rasi ya Uarabuni, waliotajwa katika vyanzo vya Waashuri wakati wa utawala wa Sargon II. Jina la kabila hili linaendelea kuonekana katika hati hadi karne ya nne BK, lakini kufikia karne ya sita walikuwa wanachukuliwa kama kundi lililokuwa limetoweka zamani .

Kulingana na Quran, mji ambao Saleh alitumwa ulikuwa unaitwa Al-Hijr, ambao unalingana na mji wa Wana-Nabatea wa Hegra . Mji huo ulipata umaarufu karibu na karne ya 1 BK kama eneo muhimu katika biashara ya msafara wa kanda hiyo . Karibu na mji huo kulikuwa na makaburi makubwa yaliyochongwa kwenye miamba, yaliyotumiwa na wanachama wa makundi mbalimbali ya kidini . Katika wakati usiojulikana wa zamani, eneo hilo lilitelekezwa na labda likachukuliwa nafasi na Al-'Ula . Tangu enzi za Muhammad, eneo hilo limekuwa likijulikana kama Mada'in Salih, likiwa limepewa jina baada ya mtangulizi wake Salih .

Saleh hatatajwi katika maandiko yoyote ya kihistoria au katika maandiko yoyote ya kidini ya Kiyahudi au Kikristo yanayotangulia Quran, lakini simulizi ya kuangamizwa kwa Thamud inaweza kuwa ilijulikana sana katika Arabia ya kale. Jina la kabila hilo linatumika katika mashairi ya kale ya Kiarabu kama sitiari ya "udumavu wa mambo yote" .

 

Historiakatika Quran

Nabii Salih(a.s) alifuatia baada ya Hud(a.s) na alitumwa kwa watu wa kabila (Taifa) la Thamud. Makazi yao yalikuwa kaskazini mwa Arabia sehemu iliyojulikana kama al-Hijr Mada’in Salih.

Thamud waliongoza katika teknolojia ya kuchonga majabali na kuyafanya majumba ya fahari kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:


 

......

“Na kumbukeni (Allah) alivyokufanyeni makhalifa baada ya ‘Ad na kukuwekeni vizuri katika ardhi; mnajenga majumba makubwa ya kifalme katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika majabali (yake).........” (7:74)

Baada ya muda kupita Thamud nao waliacha mafundisho ya Mtume Hud(a.s) kama walivyofanya akina ‘Ad hapo zamani, wakawa wanaabudia masanamu na kufisidi katika ardhi. Ndipo Allah(s.w) akamtuma Nabii Salih(a.s) kulingania Uislamu kwa wakazi wa Hijr.


 

Ujumbe wa Nabii Salih(a.s) kwa Watu Wake

 

Nabii Salih(a.s) aliwalingania watu wa kaumu yake, wamwamini Allah(s.w) na kumuabudu ipasavyo, watubie na waombe msamaha kwa dhambi zao:


 


“Na kwa Thamud tukampelekea ndugu yao, Salih, akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Allah; nyinyi hamna Mungu ila yeye. Yeye ndiye aliyekuumbeni katika ardhi, na akakukalisheni humo. Basi muombeni msamaha, kisha mrejee kwake. Hakika Mola wangu ni karibu (na waja wake) anapokea (maombi yao).” (11:61)

Nabii Salih aliendelea kuwalingania


 

“Mcheni Mwenyezi Mungu na nitiini.” “Wala msitii amri za wale maasi, (wenye kupindukia mipaka ya Mungu).” “Ambao wanafanya uharibifu tu katika ardhi wala hawaitengenezi.” (26:150-152)

 

Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu

 

Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a.s) naye kwa kuzingatia mazingira ya watu wake, alitumia mbinu zifuatazo katika kuulingania Uislamu:


 

Kwanza, alijieleza kwa uwazi kuwa yeye ni Mtume wa Allah(s.w)


 

“Bila shaka mimi kwenu ni Mtume mwaminifu.” (26:143)

Pili, aliwakumbusha watu wake neema za Allah(s.w) zilizo juu yao ili waone umuhimu wa kumshukuru na kumuabudu ipasavyo:


 


“Na kumbukeni (Mwenyezi Mungu) alivyokufanyeni makhalifa baada ya ‘Ad na kukuwekeni vizuri katika ardhi mnajenga majumba makubwa ya kifalme katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika majabali (yake). Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu, wala msifisidi katika ardhi kwa kufanya uharibifu.” (7:74)


 

“Je (mnafikiri kuwa) mtaachwa salama katika haya yaliyopo hapa (kwenu):” “Katika mabustani na chemchem, (mito).” “Na mimea na mitende yenye makole mazuri.” “Na mnachonga milimani majumba mkistarehe tu basi.” (26:146-149)


 

Tatu, aliwanasihi na kuwasisitiza watu wake wamche Allah(s.w)
na kumtii yeye badala ya kuwatii watu:


 

“Mcheni Allah na mtiini. Wala msitii amri za wale maasi (wenye kupindukia mipaka ya Allah). Ambao wanafanya uharibifu tu katika ardhi wala hawaitengenezi.” (26:150-152)

Nne,alisisitiza kutohitajia ujira kwa watu wake, kama walivyozoea kutoa ujira kwa viongozi wao kwa ajili ya manufaa na starehe zao binafsi.


 

“Wala sikutakini ujira juu yake, ujira wangu hauko ila kwa Mola wa walimwengu wote.” (26:145)

Tano, alionyesha muujiza wa jabali kuzaa ngamia jike kama dalili za Utume wake baada ya watu wake kumtaka afanye hivyo kwa uwezo wa Allah(s.w).


 

Akasema: “Enyi watu wangu! Mnaonaje, kama ninazo dalili zilizo wazi zitokazo kwa Mola wangu (za kunionyesha ukweli wa haya), naye amenipa rehema kutoka kwake, basi ni nani atakayeninusuru kwa Mwenyezi Mungu kama nikimuasi? Basi hamtanizidishia kwa hayo mnayonitakia ila khasara.(11:63)


 

Enyi watu wangu! Huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ni Ishara kwenu (mliyoitaka kwangu ili kuonyesha ukweli wa Utume wangu). Basi muacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu; wala msimguse kwa ubaya isije ikakuangamizeni adhabu iliyo karibu (na kukufikieni).” (11:64)

 

Wapinzani wa Ujumbe wa Nabii Salih(a.s)

 

Baada ya Nabii Salih(a.s) kufikisha ujumbe wa Allah(s.w) kwa ufasaha na kwa uwazi, watu wake waligawanyika makundi mawili.

Wachache wao waliamini, wengi katika hao wakiwa dhaifu.Wengi wao wakiongozwa na wakuu wa jamii walikufuru. Makafiri wa Kithamud waliukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.s) kwa sababu zifuatazo:


 

Kwanza, Walimuona Salih(a.s) kuwa ni mwongo, kuwa hapana cha kuwepo Allah wala adhabu kutoka kwake.

Wakasema wale waliotakabari “Sisi tunayakataa yale mnayoyaamini. Na wakamtumbua (wakamuua) yule ngamia na wakaasi amri ya Mola wao na wakasema: “Ee Salih! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume. (7:76-77)


 

Wakamchinja. Basi (Salih) akasema: “Stareheni katika mji wenu huu (muda wa) siku tatu (tu, kisha mtaadhibiwa); hiyo ni ahadi isiyokuwa ya uwongo.” (11:65)


 

Pili,hawakuwa tayari kuacha miungu ya Babu zao:

Wakasema: “Ewe Salih! Bila shaka ulikuwa unayetarajiwa (kheri) kwetu kabla ya haya (Sasa umeharibika). Oh! Unatukataza kuabudu waliowaabudu baba zetu? Na hakika sisi tumo katika shaka inayotusugua (katika nyoyo zetu) kwa haya unayotuitia.” (11:62)


 

Tatu, walimuona Salih(a.s) kama mtu aliyerogwa na wakamdai kuleta muujiza:

Wakasema “Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa (wakakosa akili).” “Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi; basi lete muujiza ikiwa ni miongoni mwa wasemao kweli.” (26:153-154)

 

Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao

 

Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.s), bali walidhihirisha jeuri yao kwa kumuua ngamia wa muujiza ili waione hiyo adhabu waliyoahidiwa (Rejea Qur-an 7:77). Baada ya kumuua ngamia walipewa siku tatu kama fursa ya mwisho ya kuamini na kutubia makosa yao. Badala ya kutubia kama vile haitoshi kwa kosa walilolifanya, walikula njama za kumuua Nabii Salih na wale walioamini pamoja naye.


 


Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya matata (kabisa) katika ardhi (hiyo) wala hawakusuluhisha (jambo ila kuharibu tu). Wakasema: “Apianeni kwa Mwenyezi Mungu (ya kwamba) tutamshambulia usiku yeye (Salih) na watu wake, kisha tutamwambia mrithi wake; Sisi hatukuona maangamio (yake wala) ya watu wake na bila shaka sisi ni wa kweli kwao.(27:48-49)


 

Basi wakapanga vitimbi (vyao); na sisi tukapanga mipango yetu
(tukapangua vitimbi vyao)na hali ya kuwa hawana habari. (27:50)

Kuangamizwa Makafiri na Kunusuriwa Waumini Mwisho wa siku ya tatu makafiri waliangamizwa na wakanusurika Salih(a.s) na wale walioamini pamoja naye kama tunavyojifunza katika Qur-an:


 

Basi ilipofika amri yetu, tukamuokoa Salih na wale walioamini pamoja naye kwa rehema Yetu; na (pia tukawaokoa) katika hizaya ya siku hiyo. Hakika Mola wako ndiye Mwenye nguvu (na) Mwenye kushinda.(11:66)


 

Na wale waliodhulumu (nafsi zao) uliwaangamiza ukelele (uliopigwa na Malaika); wakapambazukiwa wametulia tu (wamekufa) katika majumba yao. Kama kwamba hawakuwamo humo. Sikilizeni. Hakika Thamud walimkufuru Mola wao; basi Thamud wamepotelea mbali. (11:67-68)


 


Mtetemeko wa ardhi ukawanyakuwa (roho zao) na wakawa wamekufa humo katika miji yao. Basi (Salih) akawaacha (akenda zake), na huku anasema: “Enyi kaumu yangu! Nilikufikishieni ujumbe wa Mola wangu na nikakunasihini, lakini nyinyi hamwapendi wenye nasaha.” (7:78-79)


 

Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa jeshi la Allah(s.w) lililotumika kuwaangamiza makafiri wa Kithamud ni tetemeko la ardhi lililosababishwa na ukelele wa Malaika. Kumbuka:




 

“Na majeshi ya mbingu na ardhini ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, mwenye hikima.” (48:7)

 

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)

Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a.s).


 

Mafunzo ya ziada ni kuwa:

(i) Maendeleo ya sayansi na teknolojiahayana maana yoyote
ya amii kama hayatatumiwakwa ajili ya kusimamisha ukhalifa utakaotengeneza mazingira ya kuwepo kwa amani ya kweli.


 

(ii) Hivi leo maendeleo ya sayansi na teknolojia imekuwa ndio silaha ya kuendeleza dhuluma na maangamizi ya mamilioni kwa mamilioni ya watu wasio na hatia.


 

(iii) Pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia waliyonayo matwaghuti hivi leo,Waislamu wakijizatiti na kufanya subira watawashinda matwaghuti na kusimamisha ukhalifa kama ilivyokuwa kwa Nabii Hud(a.s) na Salih(a.s) kwa msaada wa Allah(s.w). Rejea Qur-an (8:59-60, 66)





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-06-26 08:58:20 Topic: visa vya Mitume Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 292


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Historia ya Nabii Idrisa
Katika somohili utakwenda kujifunza historia ya Nabii Idrisa (amani iwe juu yake) Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Musa
atika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Musa Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Swaleh (Salih)
Katika post hii utakwenda kujifunza historia ya Mtume Swalehe katikaQuran Soma Zaidi...

Hstora ya Nab Sulaman
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Sulaman Soma Zaidi...

Hstora ya Nabii Adam
ata post h utawenda ujfunza hstora ya Nabii Adam ulngana na Quran navyoeleza Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Ibrahimu
Katika post hii utakwenda kujifunza historia ya Mtume Ibrahim katika quran Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Ismail katika quran
KKatika somohili utakwenda kujifunzahistoriaya Mtume Ismail Mtoto wa Nabii Ibrahim Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Ya'qub
Katika somo hili utawenda ujfunz ahstoraya Nabii Ya'qub na familia yake Soma Zaidi...

Hstora ya Nabii Yunus
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Yunus Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Shu'aib
atika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Shu'aib katika Quran Soma Zaidi...

Historiaya Nabii Isa
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Historia ya Nabii Isa Soma Zaidi...

Histora ya Nabi Zakariya
Katika somo hili utakwenda ujfunza kuhusu hslistoria ya Nabi Zakariya Soma Zaidi...