Navigation Menu



Historia ya Mtume Hud katika Quran

Katika makala hii utakwenda kujifunzahistoria ya Mtume Hud katika Quran

HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD

Baada ya Nuhu(a.s) Mtume aliyemfuatia ni Nabii Hud(a.s). Hud(a.s) alitumwa na Mola wake kuwalingania kabila (taifa) la ‘Ad. Kabila la ‘Ad lilikuwa likijulikana kama ‘Ad-al-ram au ‘Ad-Ula. ‘Ad walikuwa wakiishi kusini ya Bara Arab, eneo la kati ya Oman hadi Hadharamut na Yemen. Akina ‘Ad waliongoza katika teknologia ya kujenga majumba marefu katika makazi yao:


 

“Je, hukuona jinsi Mola wako alivyowafanya ‘Ad? Iram (waliokuwa)wanamajumba mar efu mar efu. Ambao hawakuumbwa mfano wao katika miji. (89:6-8)


 

Baada ya muda kupita, ‘Ad waliacha mafundisho sahihi ya Nabii Nuhu(a.s) ya kumpwekesha Allah(s.w) na wakarejea tena kwenye kuabudia masanamu wakiongozwa na wakuu wa jamii. Ndipo, Hud(a.s) akatumwa na Mola wake kuhuisha tena Uislamu.


 

“Na kwa ‘Ad (tulimpeleka) ndugu yao Hud akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Allah, nyinyi hamna Mungu ila yeye. Basi hamuogopi?” (7:65)


 

 

Mbinu za Hud(a.s) Katika Kufikisha Ujumbe

 

Katika kulingania Uislamu kwa watu wake, Hud(a.s) alitumia mbinu zifuatazo:


 

Kwanza alijieleza kwa uwazi na kuwanasihi watu wake:

“Akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi sio mpumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola wa walimwengu. Nakufikishieni ujumbe wa Mola wangu. Na mimi kwenu ni (mtu) nasihi muaminifu.(7:67-68)


 


Mnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayotoka kwa Mola wenu kwa (ulimi wa) mtu aliye mmoja katika nyinyi ili akuonyeni? (Muabuduni Mwenyezi Mungu) na mkumbuke alivyokufanyeni Khalifa baada ya watu wa Nuhu.Na akakuzidisheni sana katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufaulu.” (7:69)


 

Pili aliwapa hoja kwanini wanalazimika kumuamini Allah na kumuabudu ipasavyo.


 


Mcheni yule ambaye amekupeni haya mnayoyajua.” “Amekupeni (chungu ya) wanyama na watoto wanaume.” “Na mabustani na chemchem, (mito).” (26:132-134)


 

Tatu, aliwabashiria kupata malipo mema hapa hapa ulimwe nguni endapo watamcha Allah(s.w) ipasavyo:


 

“Enyi watu wangu! Ombeni msamaha kwa Mola wenu (kwa mabaya yenu yaliyopita) kisha mtubie kwake, atakuleteeni mawingu yateremshayo mvua tele, na atakuzidishieni nguvu juu ya nguvu zenu (mlizonazo). Wala msikengeuke kuwa waovu.” (11:52)


 

Nne, aliwahofisha watu wake na adhabu kali ya Allah(s.w)
iwapo watamuasi.


 

“Na kama mtarudi nyuma (hainidhurishi kitu); nimekwisha kukufikishieni niliyotumwa nayo kwenu; na Mola wangu atawafanya makhalifa (wakazi wa mahali hapa) watu wengine wasiokuwa nyinyi; wala nyinyi hamtaweza kumdhuru hata kidogo. Hakika Mola wangu ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.” (11:57)


 

“(Wakumbushe) alipowaambia ndugu yao Hud.‘Je, hamtamu ogopa (Mwenyezi Mungu hata nikikutajieni adhabu yot itakayokufikieni kwa mabaya yenu mnayoyafanya)? Bila shaka mimi kwenu ni Mtume muaminifu.” (26:124-125).


 

Tano,aliwafahamisha kwa uwazi watu wake kuwa hakutarajia kupata malipo ya Utume wake kutoa kwao.


 

“Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira juu ya haya. Haukuwa ujira wangu ila kwa yule aliyeniumba. Basi hamyatii akilini (haya ninayokuambieni)?” (11:51).


 

“Wala sikutakieni juu yake ujira, ujira wangu haupo ila kwa
Mola wa walimwengu wote.” (26:127)

 

Wapinzani wa Ujumbe wa Hud(a.s)

 

Waliomuamini Mtume Hud(a.s) walikuwa watu wachache na wengi walipinga ujumbe wake. Waliongozwa na Wakuu wa jamii.


 

“Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, sisi tunakuona umo katika upumbavu na tunakuona u miongoni mwa waongo.” (7:66).


 

Katika kuupinga ujumbe wa Mtume Hud (a.s), makafiri walitoa hoja zifuatazo:


 

Kwanza,walidai kuwa hawako tayari kuacha kuabudu yale waliyokuwa wakiabudu wazee wao.


 


Wakasema: “Je! umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na tuache waliyokuwa wakiabudu baba zetu? Basi tuletee unayotuahidi ikiwa ni miongoni mwa wasemao kweli.” (7:70).


 

Pili,walidai kuwa Hud(a.s) alikuwa mzushi kama wazushi wengine waliotokea katika zama mbali mbali na hasa pale alipowaambia watu watafufuliwa baada ya kufa na kulipwa kwa yale waliyoyafanya hapa duniani.


 

“Hayakuwa haya (ya kuja watu kusema kuwa wao ni Mitume) ila ni tabia ya watu wa (tangu) kale. Wala sisi hatutaadhibiwa (kama unavyodai na walivyodai hao).” (26:137-138)


 

“Je anakuahidini ya kwamba mtakapokufa na mkawa udongo na mifupa, kuwa mtatolewa, (mtafufuliwa)?” Hayawi hayo mnayoahidiwa.(23:35-36).


 

Hakuwa huyu (anayejiita Mtume) ila ni mtu anayemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi si wenye kumuamini. “(23:38)


 

Tatu,walidai kuwa Hud (a.s) alikuwa mpumbavu au mjinga.

“Wakasema wakuu waliokufuru katika kaumu yake, “Sisi tunakuona umo katika upumbavu na tunakuona u miongoni mwa waongo”. (7:66).


 

Nne, walidai kuwa hakuwa Mtume kwa kuwa alikuwa mtu ana yekula na kunywa kama wao:


 


Na wakubwa katika watu wake waliokufuru na kukadhibisha makutano ya akhera, na tuliwatajirisha katika maisha ya dunia, walisema: “Hakuwa huyu ila ni mtu kama nyinyi, anakula katika vile mnavyokula na anakunywa katika vile mnavyokunywa.” (23:33)

 

Msimamo wa Nabii Hud(a.s) Dhidi ya Makafiri wa Kaumu Yake


Pamoja na kwamba alipingwa na nguvu za Dola ya makafiri wa kaumu yake, Mtume Hud(a.s), hakutetereka katika msimamo wake wa kutangaza Ufalme wa Allah(s.w) na kufikisha ujumbe wake. Hakutetereka kwa sababu alitegemea ulinzi wa yule aliyemtuma, mwenye uwezo juu ya kila kitu kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


 

“..........Akasema (Hud) mimi namshuhudia Mwenyezi Mungu, nanyi shuhudieni ya kwamba mimi niko mbali na hao mnaowashirikisha (na Mwenyezi Mungu) mkaacha (kumuabudu)


 

yeye (pekee). Basi nyote nifanyieni hila (za kunidhuru) kisha msinipe muhula wowote”.(11:54-55).


 

Mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu. Hakuna kiumbe chochote isipokuwa (Mwenyezi Mungu) anamsanifu atakavyo. Bila shaka Mola wangu yuko juu ya njia iliyonyooka.(11:56)




 

Na kama mkirudi nyuma (hainidhurishi kitu); nimekwisha kukufikishieni niliyotumwa nayo kwenu; na Mola wangu atawafanya Makhalifa (wakazi wa mahala hapa) watu wengine wasiokuwa nyinyi wala nyinyi hamtaweza kumdhuru hata kidogo. Hakika Mola wangu ni mwenye kuhifadhi kila kitu.”. (11:57)


 

Ushindi wa Nabii Hud(a.s) Juu ya Makafiri

 

Makafiri walivyozidi kutakabari na kuzidisha fisadi katika ardhi ikiwa ni pamoja na kutaka kumdhuru Nabii Hud(a.s) na wale walioamini pamoja naye, Allah(s.w) alipitisha hukumu yake ya kuwahilikisha makafiri na kuwanusuru waumini kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


 

Ilipofika amri yetu ya (kuangamizwa) tulimuokoa Hud pamoja na wale walioamini pamoja naye kwa rehema itokayo kwetu. Na tukawaokoa katika adhabu ngumu.(11:58)


 


Na hao ndio ‘Ad. Walikanusha aya za Mola wao, na wakawaasi
Mitume yake na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi.(11:59)


 

Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na siku ya kiyama. Sikilizeni hakika ‘Ad walimkufuru Mola wao. Wakaangamizwa hao
‘Ad kaumu ya Hud.” (11:60)

Jeshi la Allah(s.w) lililotumika dhidi ya makafiri katika jamii ya akina ‘Ad ni upepo mkali uliovuma mfululizo kwa siku nane (mausiku Sabaa na michana minane) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


 

Basi walipoliona wingu likiyaelekea mabonde yao, walisema: “Wingu hili la kutunyeshea mvua.” (Wakaambiwa) “Bali haya ni ile mliyokuwa mkitaka ije kwa upesi, (adhabu ya Mwenyezi Mungu). Ni upepo ambao ndani yake iko adhabu iumizayo.” “Unaoangamiza kila kitu kwa amri ya Mola wake.” Basi wakawa si wenye kuonekana tena ila nyumba zao tu (ndizo zilizosalia). Hivyo ndivyo tuwalipavyo watu waovu. (46:24-25)


 


Na bila shaka tuliwastawisha katika yale tusiyokustawisheni nyinyi, na tuliwapa masikio na macho na nyoyo; lakini masikio yao na macho yao na nyoyo zao hazikuwafaa chochote walipokuwa wakikanusha Aya za Mwenyezi Mungu, na yakawazunguka yale waliyoyafanyia mzaha. (46:26)


 


Na katika (habari za), Adi (ziko alama kadhalika). (Kumbusha) Tulipowapelekea upepo wa papazi uangamizao. Haukuacha chochote ulichokijia ila ulikifanya kama kamba mbovu. (51:41-42)


 


Walikadhibisha kina Adi (nao); basi ilikuwaje adhabu Yangu na maonyo Yangu! Hakika tuliwapelekea upepo mkali katika siku ya nuhsi iendeleayo (kwao mpaka leo). Ukiwang’oa watu (katika ardhi kisha unawabwata chini, wamelala, wamekufa) kana kwamba ni magogo ya mitende iliyong’olewa. Basi ilikuwaje adhabu Yangu na maonyo Yangu! (54:18-21).


 

Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu; Mwenye hikima. (48:7)

 

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Hud(a.s)

(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s.w) na lengo la binaadamu hapa ulimwenguni.


 

(ii) Kutomchelea yeyote katika kufanyakazi ya kulingania
Uislamu na kuusimamisha katika jamii.


 

(iii) Katika kufanyakazi ya kuhuisha Uislamu katika jamii tutarajie malipo kutoka kwa Allah(s.w) peke yake.


 

(iv) Katika kufanya kazi ya kulingania na kusimamisha Uislamu katika jamii tumtegemee Allah(s.w) peke yake.


 

(v) Waislamu wakijizatiti ipasavyo, watawashinda makafiri.
Pamoja na nguvu kubwa walizonazo.

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-06-25 20:58:46 Topic: visa vya Mitume Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 316


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Historiaya Nabii Isa
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Historia ya Nabii Isa Soma Zaidi...

Hstora ya Nabii Adam
ata post h utawenda ujfunza hstora ya Nabii Adam ulngana na Quran navyoeleza Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Ayyuub
Katika somo hiliutakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii ayyuub Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Idrisa
Katika somohili utakwenda kujifunza historia ya Nabii Idrisa (amani iwe juu yake) Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Shu'aib
atika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Shu'aib katika Quran Soma Zaidi...

hHistoria ya Nabii Dhul-kifl
Katika makala hii tutakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Dhul-kifl Soma Zaidi...

Histora ya Nabi Zakariya
Katika somo hili utakwenda ujfunza kuhusu hslistoria ya Nabi Zakariya Soma Zaidi...

Historia ya Nabii Ismail katika quran
KKatika somohili utakwenda kujifunzahistoriaya Mtume Ismail Mtoto wa Nabii Ibrahim Soma Zaidi...

Historia ya Mtume Ibrahimu
Katika post hii utakwenda kujifunza historia ya Mtume Ibrahim katika quran Soma Zaidi...

Hstora ya Nabii Yahya
Katika somo hili uatkwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Yahya Soma Zaidi...