Katika somohili utakwenda kujifunza historia ya Nabii Idrisa (amani iwe juu yake)
Katika Quran
Mtume aliyemfuatia Nabii Adam(a.s) katika Mitume 25 waliotajwa katika Qur-an ni Idrisa(a.s).
Nabii Idrisa(a.s) ametajwa kwa ufupi katika Qur-an
“Na mtaje Idrisa katika Kitabu (hiki). Bila shaka yeye alikuwa mkweli sana (na) Nabii. Na tulimuinua daraja ya juu kabisa.” (19:56-57).
Na (mtaje) Ismail, na Idrisa na Dhul-kifli wote walikuwa miongoni mwa wanaosubiri.” (21:85)
Katika aya hizi Nabii Idrisa(a.s) ametajwa kuwa alikuwa Nabii wa Allah(s.w) aliyepea katika ukweli na subira na Allah akamnyanyua daraja ya juu kabisa kutokana na sifa zake hizo. Hatuna taarifa zaidi ya harakati za Nabii Idrisa(a.s) katika kuhuisha Uislamu na kuusimamisha katika jamii yake, bali itoshe tu kuwa mwanaharakati anayefanya kazi ya Mitume wa Allah ya kusimamisha Uislamu katika jamii hanabudi kujipamba na tabia ya ukweli na subira.
Inasemekana kuwa nabii Idrisa:-
1. Ndiye mtu wa kwanza kuandika
2. Ndiye mtume wa kwanza kutoa darsa
3. Ndiye mtu wa kwanza kushona nguo
Idris alizaliwa huko Babeli, mji ulioko katika eneo la sasa la Iraq. Kabla ya kupokea Ufunuo. Idris alipokuwa mkubwa, Mungu alimtunuku Unabii. Wakati wa maisha yake, watu wote hawakuwa bado Waislamu. Baadaye, Idris aliacha mji wake wa Babeli kwa sababu idadi kubwa ya watu walitenda dhambi nyingi hata baada ya kuwaonya. Baadhi ya watu wake waliondoka na Idris. Ilikuwa vigumu kwao kuacha makazi yao.
Wanahistora waslamu wanasimulia kuwa Idris alifanywa nabii akiwa na umri wa miaka 40, sawa na umri ambao Muhammad alianza kutoa unabii, na aliishi wakati ambapo watu walikuwa wameanza kuabudu moto. Tafsiri zinapanua juu ya maisha ya Idris, na kusema kwamba nabii aligawanya muda wake katika sehemu mbili. Kwa siku tatu za wiki, Idris angehubiri kwa watu wake na kwa siku nne angejishughulisha tu na ibada ya Mungu. Wanahistora kama al-Tabari, walimpa Idris sifa ya kuwa na hekima na maarifa makubwa.
Tafsiri zinasimulia kwamba Idris alikuwa miongoni mwa "watu wa kwanza kutumia kalamu pamoja na kuwa mmoja wa watu wa kwanza kuangalia mwendo wa nyota na kuweka uzito na vipimo vya kisayansi." Ibn Arabi alimuelezea Idris kama "nabii wa wanafalsafa" na kazi kadhaa zilihusishwa naye. Baadhi ya wanazuoni waliandika tafsiri juu ya kazi hizi zinazodaiwa kuwa zake, wakati huo huo Idris pia alipewa sifa ya uvumbuzi kadhaa, ikiwa ni pamoja na sanaa ya kutengeneza mavazi.
Mfasiri Ibn Ishaq alisimulia kwamba alikuwa mtu wa kwanza kuandika kwa kalamu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika makala hii utakwenda kujifunzahistoria ya Mtume Hud katika Quran
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza historia yaMtume Lut kutoka katika Quran
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Mtume Al-yasa'a
Soma Zaidi...ata post h utawenda ujfunza hstora ya Nabii Adam ulngana na Quran navyoeleza
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Historia ya Nabii Isa
Soma Zaidi...atika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Shu'aib katika Quran
Soma Zaidi...Katika somo hili utawenda ujfunz ahstoraya Nabii Ya'qub na familia yake
Soma Zaidi...atika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Musa
Soma Zaidi...KKatika somohili utakwenda kujifunzahistoriaya Mtume Ismail Mtoto wa Nabii Ibrahim
Soma Zaidi...Katika makala hii tutakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Dhul-kifl
Soma Zaidi...