Hstora ya Nab Ishaqa katika quran

Katika post hii tutakwenda kujifunza historia ya Mtume Ishaqa

IS-HAQ(A.S.) NA YA‘AQUUB(A.S.)

 

Is-haq(a.s) ni mtoto wa pili wa Nabii Ibrahiim(a.s), mama yake akiwa Sarah. Habari njema ya kumzaa Is-haq ilimjia Nabii Ibrahim(a.s.) mara tu baada ya kufuzu mtihani wa kumchinja mwanae mkubwa, Ismail(a.s). Alipongezwa kwa kubashiriwa kuzaliwa kwa Is-haq(a.s.):


 

Amani kwa Ibrahim. Hivi ndivyo tunavyowalipa watendao mema. Bila shaka yeye alikuwa miongoni mwa waja wetu walioamini (kweli kweli).Tena tukambashiria (kumzaa) Is-haq, Nabii miongoni mwa watu wema (kabisa). (37:109-112).


 

Maelezo ya kuzaliwa Is-haq na hatimaye Ya‘aquub(a.s.) yanapatikana katika kisa cha Malaika waliompa Nabii Ibrahiimu habari za kuangamizwa watu waovu wa Nabii Lut(a.s) na zile za yeye kupata mtoto katika uzee wake.


 


Na mkewe (Ibrahim - bibi Sarah) alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukampa habari njema ya (kuwa watazaa mtoto wamwite) Is-haq na baada ya I’shaq (watapata mjukuu wamwite) Yaaquub.(11:71)


 


(Mkewe Ibrahim) akasema: “Ee mimi we! Nitazaa na hali mimi ni mkongwe, na huyu mume wangu ni mzee sana? Hakika hili ni jambo la ajabu.”(11:72)


 

Wakasema (wale Malaika): Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye anayestahiki kusifiwa na kutukuzwa.” (11:73)

 

Shukurani za Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Allah(s.w)

Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Is- haqa(a.s), Nabii Ibrahim(a.s.) alimshukuru Allah(s.w) kwa maneno yafuatayo:

“Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipa juu ya uzee (wangu watoto wawili hawa):- Ismail na Is-haqa. Hakika Mola wangu ni mwenye kusikia maombi (ya waja wake)” (14:39).

Is-haqa alipofikia utu uzima naye alipewa Utume na akaruzukiwa mtoto - Ya‘aquub(a.s) naye pia akapewa Utume.


 

.............Tulimpa Is-haqa na Ya‘akub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.Na tukawapa rehema zetu na tukawafanyia sifa za kweli tukufu(za kusifiwa na viumbe). (19:49-50).


 

Na tukawajaalia kuwa maimamu wanaoongoza kwa amri yetu, na tukawapelekea wahyi wa kuzifanya kheri na kusimamisha Sala na kutoa Zaka. Na walikuwa kwetu ni wenye kutunyenyekea. (21:73).


 

Aya tulizozinukuu zaweka wazi kuwa Is-haqa na mwanawe Ya’aquub, walikuwa Mitume na viongozi wa kusimamia utekelezaji wa sheria za Allah(s.w).


 

Mafunzo Yatokanayo na Historia Nabii Is-haqa na Ya’aquub(a.s)

(i) Kutenda mema kunampatia muumini faida kubwa hapa duniani na huko akhera.

(ii) Tunatakiwa tuwachague kuwa viongozi wetu wa jamii wale waliotuzidi katika matendo mema.

(iii) Ni wajibu wa Waumini kumshukuru Allah(s.w) baada ya kupata ushindi, kufaulu au kupata mafanikio yoyote yale katika mchakato wa maisha.

 

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: visa vya Mitume Main: Dini File: Download PDF Views 412

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Historia ya Mtume Al-yasa’a

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Mtume Al-yasa'a

Soma Zaidi...
Historia ya Nabii Shu'aib

atika makala hii utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Shu'aib katika Quran

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Ibrahimu

Katika post hii utakwenda kujifunza historia ya Mtume Ibrahim katika quran

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Swaleh (Salih)

Katika post hii utakwenda kujifunza historia ya Mtume Swalehe katikaQuran

Soma Zaidi...
Historia ya Mtume Lut

Katika somo hili utakwenda kujifunza historia yaMtume Lut kutoka katika Quran

Soma Zaidi...
Historia ya Nabii Musa

atika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Musa

Soma Zaidi...
Hstora ya Nabii Ilyasa

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Ilyasa

Soma Zaidi...
Historia ya Nabii Idrisa

Katika somohili utakwenda kujifunza historia ya Nabii Idrisa (amani iwe juu yake)

Soma Zaidi...
Historia ya Nabii Ayyuub

Katika somo hiliutakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii ayyuub

Soma Zaidi...
hHistoria ya Nabii Dhul-kifl

Katika makala hii tutakwenda kujifunza kuhusu historia ya Nabii Dhul-kifl

Soma Zaidi...