Karun na Hamana waliishi zama za Mtume Musa(a.
Karun na Hamana waliishi zama za Mtume Musa(a.s) na walikuwa viongozi waandamizi wa Firaun. Walikuwa ni watu maarufu katika jamii yao na walikuwa mstari wa mbele katika kumpinga Mtume Musa(a.s).
“Na kwa yakini tulimtuma Musa pamoja na miujiza yetu na hoja (dalili) zilizo dhahiri. (Tulimpeleka) kwa Firauni na Hamana na Karun, wakasema: “(Huyu ni) Mchawi, muongo mkubwa” (40:23-24).
Katika aya nyingine Mwenyezi Mungu anatufahamisha kuwa aliwaangamiza Firaun, Hamana na Qarun kwa sababu waliyakanusha mafundisho ya Mtume Musa na wakatakabari:
Na (vile vile) Qarun na Firauni na Hamana (waliangamizwa); na hakika aliwajia Musa kwa miujiza waziwazi, lakini walijivuna katika ardhi, lakini hawakuweza kumshinda Mwenyezi Mungu. Basi kila mmoja tulimtesa kwa sababu ya dhambi zake. Miongoni mwao wako tuliowapelekea kimbunga cha changarawe; na miongoni mwao wako waliotolewa roho kwa ukulele mkubwa, na miongoni mwao wako tuliowadidimiza ardhini na miongoni mwao wako tuliowagharikisha na hakuwa Mwenyezi Mungu Mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu (wenyewe) nafsi zao” (29:39-40).
Qarun alijaaliwa kuwa na mali nyingi sana. Lakini alilisahau lengo la maisha akatakabari. Watu walio karibu naye walimnasihi lakini hakuzinduka. Alijivuna na kuona kuwa utajiri aliokuwa nao kaupata kwa juhudi na elimu yake. Alisahau kuwa hiyo ni neema kutoka kwa Allah(s.w).
Hakika Qarun alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa hazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu (kuzichukua). Walimwambia watu wake: “Usijione (usijigambe), hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanaojigamba” (28:76).
Akasema: “Hakika nimepewa haya kwa sababu ya ilimu niliyo nayo”. Je, hakujua ya kwamba Mwenyezi Mungu amewaangamiza kabla yake watu waliokuwa wenye nguvu zaidi kuliko yeye na wenye mkusanyo mwingi zaidi (kuliko wake yeye)?” (28:78).
Kwa kutakabari kwake huko, Qarun aliangamizwa kwa kudidimizwa ardhini yeye na nyumba yake.
“Basi tukamdidimiza yeye (Qarun) na nyumba yake ardhini, wala hapakuwa na kundi lolote la kumsaidia kinyume na Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa walioweza kujisaidia” (28:81).
Yapo mafunzo mengi kutokana na maisha ya Qarun. Funzo la kwanza ni kuwa kama utajiri hautatumiwa vyema, waweza kuzaa maovu yafuatayo:
(i) Humfanya mwenye mali kujisahau na kutakabari.
(ii) Humfanya mwenye mali kuwasahau wenye shida na wahitaji. Hali hii huzaa jamii ya wenye mali ambao hula na kusaza wakati wengine hubaki ombaomba wasio na msaada wowote.
Funzo la pili linalolandana na maisha ya Qaruni ni kuwa mali, cheo na mamlaka ya mtu hayawezi kumsaidia chochote Mwenyezi Mungu anapopitisha hukumu yake. Qaruni alitamba kwa mali yake, lakini hukumu ya Allah(s.w) ilipofika alididimizwa yeye na mali yake ardhini.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1057
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Kitabu cha Afya
NAMNA MTUME(S.A.W) ALIVYOSIMAMISHA DOLA YA KIISLAMU MADINAH
Safari ya Mtume(s. Soma Zaidi...
Kuanzishwa kwa vitenge vya ulinza na Usalama, na usalama wa taifa
Soma Zaidi...
tarekh11
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Soma Zaidi...
Kwanini mwanadamu hawezi kuunda dini sahihi
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija. Soma Zaidi...
Kulingania watu wake na Miujiza Aliyoonyesha Nabii Isa(a.s)
Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyewawezesha Mitume na Manabii kufanya miujiza. Soma Zaidi...
tarekh 4
KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBOTukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Soma Zaidi...
Hija ya kuaga kwa mtume, na hutuba ya mwisho aliyotowa mtume katika hija
Mwaka mmoja baada ya msafara wa Tabuuk Bara Arab zima ilikuwa chini ya Dola ya Kiislamu. Soma Zaidi...
HISTORIA YA MTUME DAUD(A.S).
Nabii Daudi(a. Soma Zaidi...
Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba
Mtume (s. Soma Zaidi...