Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s)
(i) Allah(s.
Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s) Kutokana na Historia ya Nabii Yunusi(a.s) tunajifunza yafuatayo:
(i) Allah(s.w) ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu, hivyo waumini wamuelekee Allah kumuomba msamaha hata kama wamefanya kosa kubwa kiasi gani.
(ii) Toba inayokubaliwa pamoja na sharti nyingine ni ile inayoletwa kabla ya muda wa hukumu ya adhabu ya Allah (s.w) au kabla ya kufikwa na mauti:
Hawana toba wale ambao hufanya maovu mpaka mauti yamemhudhuria mmoja wao, (hapo) akasema: “Hakika mimi sasa natubu.” Wala (hawana toba) wale ambao wanakufa katika hali ya ukafiri. Hao tumewaandalia adhabu iumizayo. (4:18)
(iii) Katika kazi ya Da’awah (kulingania Uislamu) tusiwakatie tamaa watu bali tuendelee nao kwa kubadilisha mbinu mpaka mwisho wa uhai wetu au mpaka Allah(s.w) apitishe hukumu yake. Tumuige Nabii Nuhu(a.s) kwa subira (alilingania kwa miaka 950) na tusirudie kosa la kukosa subira la Nabii Yunus(a.s).
(iv) Matendo mema na ucha-Mungu, huwa ni sababu ya dua na toba ya mja kuwa kabuli mbele ya Allah(s.w).
“Basi isingelikuwa ya kwamba yeye (Yunus) alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanamuabudu (Allah(s.w) vilivyo) bila shaka angalikaa tumboni mwaka (huyo samaki) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe)”. (37:143-144)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Nasaba ya Mtume Muhammad S.A.W na familia yake.
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 1
Soma Zaidi...HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...Vita vya Al Fijar na sababu zake
Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar.
Soma Zaidi...Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...