image

Uanzishwaji wa Makundi mbalimbali ya Harakati za Kuhuisha Uislamu Ulimwenguni

8.

Uanzishwaji wa Makundi mbalimbali ya Harakati za Kuhuisha Uislamu Ulimwenguni


8.2. Uanzishwaji wa Makundi mbalimbali ya Harakati za Kuhuisha Uislamu Ulimwenguni



Umar bin Abdul Aziz

- Wakati wa utawala wa banu Umayyah, aliibuka Umar bin Abdul Aziz mwaka wa 99 A.H (717 A.D).
- Umar bin Abdul Aziz alipendekezwa kuchukua uongozi wa Ukhalifa nje na matarajio kwa vile hakuwa katika ukoo wa kifalme.
- Kutokana na uadilifu wake Umar bin Abdul Aziz, baadhi ya wanazuoni wa

Kiislamu wanamemhesabu kama Khalifa wa tano wa Dola ya Kiislamu.



Mambo aliyoyafanya Umar bin Abdul Aziz katika muda wa uongozi wake:

i. Alijenga mfumo wa maisha kwa misingi ya uadilifu, haki na usawa. ii. Aliwaondoa magavana wote waliokuwa katili na jeuri kwa raia.
iii. Alirejesha na kuimarisha Baitul-Mali ya Dola katika ukusanyaji na utumiaji wa rasilimali kwa uadilifu mpaka maskini na wanaohitajia walikosekana.

iv. Alitoa amri na kusimamia marekebisho ya vipimo ili raia wasipunjwe katika kuuza na kununua.
v. Aligawa kwa raia ardhi na rasilimali zote zilizotengwa kwa dhulma na upendeleleo kwa ajili ya wakubwa.
vi. Alikuwa karibu sana raia katika kutatua matatizo, kupokea na kufanyia kazi maoni na mapendekezo yao juu ya uongozi wake.
vii. Hakutenganisha dini na serikali, bali alisimamia kusimamishwa swala, kutolewa zakat, kuamrisha mema na kukataza maovu.
viii. Aliandika waraka na kuusambaza nchi nzima ili kujenga udugu na mapenzi ya kweli baina raia wake na kuondoa mishikamano ya kijahili, kiukoo na kimila.
ix. Alisimamia kwa ukaribu sana ukusanyaji na utumiaji wa zakat, kodi na michango mbali mbali katika Dola.
x. Aliwaamuru askari wa kiislamu kuchunga miiko ya vita iliyowekwa na Allah (s.w) na Mtume Muhammad (s.a.w).



Makundi mbalimbali ya harakati za kuhuisha Kiislamu katika Karne ya 20 A.D

a) Kikundi cha Badee-U-Zaman Said Nusri, Uturuki.

- Badee-U-Zaman ni mkurd aliyezaliwa mji wa Hizan, Uturuki mwaka 1873 A.D.

- Alitumia ujana wake kusoma Qur’an, Sheria, Falsafa, Historia, Geografia, Lugha kadhaa za kigeni, Hisabati na Baiolojia.

- Alikuwa Mcha-Mungu aliyeendesha maisha yake kwa mujibu wa Qur’an na

Sunnah bila kujali hatari yeyote ya maadui itakayomkabili.

- Aliweka mipango ya kuanzisha chuo kikuu cha Zuhra mfano wa chuo cha Al- Azhar, Misr kitakachofundisha Uislamu na elimu ya sayansi ya jamii.
- Alianzisha chama cha upinzani kiitwacho “Ittikadil-Muhammad”

kilichopambana na chama tawala cha “Kamati ya Umoja na Maendeleo”.

- Aliandika na kusambaza makala zilizohusu chama chake na kuwaonya

waislamu dhidi ya Kufuata mifumo ya maisha kinyume na Qur’an na Sunnah.

- Alikamatwa mara kadhaa na kutiwa jela (kizuizini) ikiwa ni pamoja kuhukumiwa kifo na wafuasi wake 15 na zaidi lakini baadaye aliachiwa huru.

- Akiwa jela aliandika makala alyoiita “Risalat-Nuur” na kuipenyeza mitaani kinyemela.
- Aliwaasa wabunge wa Uturuki kuishi maisha ya Kiislamu na kuepukana na mila na tamaduni za ukafiri.
- Alishutumiwa na viongozi wa serikali kuwa na njama ya kuipindua serikali

kwa kufundisha Qur’an bila kibali chao.

- Mwisho, Badee-U-Zaman alirejeshwa jela ambapo kesi yake ilipigwa kalenda hatimaye umauti ulimkuta akiwa jela akiwa na umri wa miaka 86.




Mafunzo yatokanayo na Harakati za Badee-U-Zaman

i. Ujasiri na uvumilivu katika kuendea kila jambo gumu la kheri bila kujali madhara yanayoweza kumfika.
ii. Subira na kushikamana na malengo licha ya kufikwa na misukosuko, mateso na vitisho mbali mbali kutoka kwa maadui.
iii. Ni wajibu kwa kila mwanaharakati wa Kiislamu kujali sana katika kutafuta na kufanyia kazi elimu na maarifa, hasa elimu sahihi ya mwongozo.
iv. Tabia na mwenendo mwema ni jambo la msingi sana katika kuendesha harakati za Uislamu katika jamii zetu.
v. Maadui wa Uislamu na waislamu siku zote hawatakata tamaa katika kuupiga vita Uislamu na waislamu hadi Qiyama kisimame.




b) Kikundi cha Ikh-wan Muslimiina, Misr (1906-1949 A.D)

Kuanzishwa kwake na hali ya maisha ya Misr:

- Kiliasisiwa na shahiid, Hassan Al-Bannah mwaka 1928 A.D akiwa na umri wa miaka 22 baada ya kupata stashahada ya elimu, kikiwa na watu 6
- Kikundi hiki kilikuwa na lengo la kusimamisha Uislamu Misr ambapo sheria za

Allah (s.w) zitatawala maisha ya jamii.

- Hali ya maisha ya Wamisr ilijengeka katika dhana ya secularism (kutenganisha dini na serikali), kuzagaa zinaa, madanguro, disco na kila aina ya uchafu.
- Umagharibi ulitapakaa na Uislamu ulibakia kuwa suala la mtu binafsi, sio la kijamii.

- Hassan Al-Bannah katika kupelekea kuanzisha kundi hili, aligundua kuwa;

i. Mahubiri ya Mashekhe misikitini hayatoshi katika kuelimisha na kufikisha ujumbe wa Uislamu katika jamii.
ii. Mashekhe walio wengi wanashindwa kupambana na wanaojiita

“secularists” (wasiofuata dini) na “mordenists” (wasomi wa kisasa).

iii. Mashekhe wengi wananunuliwa na kuhongwa kirahisi na serikali.



Muundo wa Ikh-wan Muslimiin:

- Kilianza na watu 6 mwaka 1928 A.D na kila mwanaharakati aliyejiunga nacho alipatiwa mafunzo maalum.
- Kupatikana wanaharakati kulifanyika kwa umakini na uangalifu mkubwa sana katika kukilea na kukilinda kikundi.
- Wanaharakati walipanda daraja kulingana na kiwango cha juhudi na baada ya

kufuzu mafunzo maalum na kula kiapo cha utii (Bai’at).



Mbinu za Harakati za Ikh-wan Muslimiin:

- Kujenga imani madhubuti juu ya Uislamu kwa kutoa elimu sahihi ya Uislamu.

- Kutoa mafunzo maalum ya kiharakati ya Kiucha-Mungu na kujiandaa kijeshi.

- Kubuni shughuli mbali mbali za kudumu za kimaendeleo za kibinafsi na kijamii kama vile; kujenga mashule, vyuo, miradi mbali mbali, n.k.




Athari na Matokeo ya Harakati za Ikh-wan Muslimiin:

- Harakati za kuelimisha umma juu ya Uislamu zilikua na kuenea kupitia darsa, mihadhara, mawadha misikitini na uandishi.
- Mwaka 1936 harakati zilikomaa na hatimaye mwaka 1948 serikali ilipiga marufuku chama cha Ikh-wan Muslimiin.
- Licha ya hivyo, serikali iliamua kuwaweka ndani wafuasi wa Ikh-wan na kufilisi mali na rasilimali zao.
- Mwaka 1949, Hassan Al-Bannah aliuliwa kwa kupigwa risasi na uongozi wa Ikh-wan Muslimiin ukawa chini ya Hassan Ismail Hudaybi.

- Mwaka 1964, serikali chini ya utawala wa Jamal Abdul-Nasser ilizingizia njama za kumuua Jamal Abdul-Nasser na kutoa mapendekezo yafuatayo;
i. Somo la Maarifa ya Uislamu liondolewe katika mtaala mashuleni na kuundwe mtaala mwingine wa maadili ya kijamaa (socialism).
ii. Ukomunisti upewe fursa ya kuvuruga imani ya Uislamu na kupiga vita vyama na taasisi zote za Kiislamu.
iii. Waislamu wenye msimamo mkali na hata wale wasiojinasibisha kikundi Ikh-wan Muslimiin wapigwe vita.

iv. Vifungo na adhabu kali viwaandame Ikh-wan Muslimiin na wasipewe fursa yeyote.
- Hivyo, matokeo ya mapendekezo haya yalikuwa kama ifuatavyo;

1. Hassan Ismail Hudaybi alichapwa kwa mnyororo mpaka akafa;

2. Mnamo 29/8/1966 viongozi wa tatu akiwemo shahiid Sayyid Qutb walihikumiwa kunyongwa;
3. Muhammad Qutb na dada yake Amina Qutb walitiwa jela;

4. Bibi Zainab Al-Ghazal, Amirat wa Umoja wa wanawake wa Kiislamu aliteswa na kutiwa kwa miaka kadhaa.


- Hadi leo hii, nchi nyingi zenye harakati za Kiislamu zinaathari ya Ikh-wan

Muslimiin.



c) Ikhw-wan Muslimiin Sudan Mwanzo wa Harakati:

- Harakati za kikundi hichi zilianza miaka ya 1950 katika chuo kikuu cha

Khartoum na kuenea vyuo vingine hadi mashuleni.

- Wanafunzi wanaharakati walijifunza nadharia ya Kikomunisti ili kuonesha madhaifu yake dhidi ya mafundisho ya Uislamu. Muundo na Harakati zake:

- Muundo wa harakati zake unafanana na ule wa Ikh-wan Muslimiin wa Misr.

- Kati ya mwaka 1970 na 1973 wanaharakati walikabiliwa na mateso makubwa yakiwemo; vifungo, kazi ngumu, kufilisiwa mali zao na kuishi uhamishoni.

- Waliamua kuingia serikalini badala ya kupambana nayo wakiwa nje, ili kupata kila mipango na taarifa inayoweza kusudiwa kuwadhuru.
- Waliwaelimisha na kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kusimamisha sheria za Kiislamu.
- Kutokana na nguvu ya Ikh-wan ndani ya serikali, rais wa Sudan Jafar Nimeir alitangaza serikali ya Kiislamu kinafiki.
- Ikh-wan walitumia vyombo vya dola kuutangaza Uislamu, ijapokuwa rais aliandaa mkakati wa kuwatia ndani viongozi wa Ikh-wan lakini hakufanikiwa.
- Hatimaye nguvu ya Ikh-wan ilizaa matunda na kuipindua serikali ya rais Jafar.



Mafanikio ya kikundi cha Ikh-wan cha Sudan:

- Kikundi kilianzisha chama kilichojulikana kwa jina la “National Islamic Front

(NIF)” kilichokuwa na nguvu na kusikilizwa na serikali.

- Kundi lilifanikiwa kuanzisha makampuni na mabenki makubwa ya Kiislamu ndani na nje ya Sudan.
- Takriban theluthi ya uchumi wa nchi ni mali za wanaharakati wa Ikh-wan

Muslimiin.



d) Kikundi cha Jamiatil-Islamy, Pakistani

Kuanzishwa kwake:

- Kilianzishwa na Sayyid Abdul A’la Maudud aliyezaliwa mwaka 1903 A.D huko

Aurangabad, Pakistani.

- Abdul A’la Maudud alipata elimu yake ya mwongozo na mazingira katika madrasa za masheikh majumbani.
Muundo wa Harakati na Mafanikio ya Jamiatil-Islamy:

- Abdul-A’la Maududi alianza uandishi wa habari katika magazeti ya “Taj” na

“Al-Jamiat” na kuanzisha gazeti lake lililoitwa “Tarjumah Ul-Qur’an”

- Mwaka 1932 Maudud aliandika Kitabu kiitwacho “Katika Kuufahamu

Uislamu” (Towards Understanding Islam).

- Mwaka 1953, Maudud aliandika Kitabu kiitwacho “Tatizo la Kadian” (The

Kadian Problem) kilichoonesha kuwa kadiani si dhehebu la Kiislamu.

- Alifanya kazi serikalini lakini alikataa kulipwa mshahara kwa kuhofia kudhibitiwa katika harakati zake.
- Mwaka 1953, Maudud alitiwa jela na kuhukumiwa kifo ingawa aliachiwa huru kwa amri ya mahakama kuu.
- Mwaka 1962, Maudud aliandika vitabu vijulikanacho kama “Uislamu na Kudhibiti Uzazi” (Islam and Birth Control) na “Haki za wanawake katika Uislamu” (Islamic Proud and The Status of Women in Islam)
- Jamiatil Islamy iliongozwa na amir akiwa kama msimamizi mkuu wa program za Jumuiya chini ya usaidizi wa Baraza Kuu (Central Council).
- Viongozi walichaguliwa kwa misingi ya Ucha-Mungu na kupatiwa mafunzo maalum ya kiharakati.
- Jumuiya ilijishughulisha kutoa huduma na kujenga vituo vya elimu, afya na mambo mbali mbali ya kiuchumi na kijamii.




Mafunzo yatokanayo na vikundi mbalimbali vya harakati za Kuhuisha Uislamu:

i. Harakati za Kiislamu ili zifikie matunda yake ni wajibu kufanya na vijana wasomi na wacha-Mungu.
ii. Misukosuko katika harakati za kuuhuisha Uislamu ni ishara ya kupatikana mafanikio.
iii. Ni wajibu wa wanaharakati wa Kiislamu kutumia mbinu za harakati za kuulingania Uislamu kulingana na zama na mazingira.
iv. Kazi kubwa na ya msingi katika kuhuisha Uislamu ni kuielimisha jamii elimu sahihi ya mwongozo pamoja na ya mazingira.
v. Hatuna budi kuwa waangalifu katika kuanzisha vikundi vya harakati, wanakundi sharti wapatikane kwa kupitia mafunzo maalum.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 500


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Uendeshaji na Kupanuka kwa Dola ya Kiislamu Kipindi cha Makhalifa Waongofu
Soma Zaidi...

Nabii Ibrahiim(a.s) Kumlingania Uislamu Baba Yake
Baada ya NabiiIbrahiim(a. Soma Zaidi...

MAMA YAKE MTUME MUHAMMAD (S.A.W) ANAMLEA MTUME MUHAMAD AKIWA NA UMRI WA MIAKA MINNE (4)
KULELEWA NA MAMA YAKE ALIPOFIKA MIAKA MINNEMtume (s. Soma Zaidi...

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Hud(a.s)
(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s. Soma Zaidi...

Vita vya Badr: Chanzo na sababu za vita vya Badr, Mafunzo ya Vita Vya Badr
Vita vya Badri. Soma Zaidi...

Wapinzani wa Ujumbe wa Hud(a.s)
Waliomuamini Mtume Hud(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII IBRAHIM
Soma Zaidi...

Vitimbi vya Makafiri Dhidi ya Nabii Salih(a.s) na Waumini na kuangamizwa kwao
Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a. Soma Zaidi...

Shukurani za Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Allah(s.w)
Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Is- haqa(a. Soma Zaidi...

Muhutasari wa sifa za wanafiki
Kwa kuzingatia aya zote tulizozipitia juu ya wanafikitunaweza kutoa majumuisho ya sifa za wanafiki kama ifuatavyo:- (1)Hutenda kinyume cha imani wanaodai kuwa nayo. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII HUD(A.S) NA WATU WA 'AD
Baada ya Nuhu(a. Soma Zaidi...

Kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...