Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu

Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu.

Aina za talaka, sharti zake na taratibu za kutaliki katika uislamu

Dhana ya Talaka

Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu.


- Talaka katika Uislamu si jambo linalopendeza bali linaruhusiwa tu pale inapobidi.
Ibn Umar (r.a) amesimulia kuwa, Mtume (s.a.w) amesema:

“Katika halali inayochukiza mbele ya Allah ni talaka” (Abu Daud)



- Hekima ya talaka ni kuwapa wawili wanaoachana fursa ya kwenda kuanzisha na kuendeleza maisha mengine ya familia kwa furaha na amani ili kufikia lengo.




Suluhu kati ya Mume na Mke Kabla ya Kutolewa Talaka

Ikitokea mume na mke wamegombana kabla ya kufikia hatua ya talaka, suluhu itafanyika kwa utaratibu ufuatao;


i. Mume na mke wafanye subra na kusuluhishana kwa kutakana radhi na kusameheana baina yao.
Rejea Qur’an (24:22), (42:40), (41:28)



ii. Mume na mke kuonyana na kukumbushana kurejea kwa Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w).


iii. Mume na mke watatengana kimalazi kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

Rejea Qur’an (2:226-227)

iv. Jamaa kwa upande wa mume na mke wakutane ili kuwasuluhisha.

Rejea Qur’an (4:35)



Haki za Kutaliki

- Katika Uislamu haki ya kutaliki iko kwa mume na mke au mahakama ya Kiislam.

- Mume humtamkia au kumwandikia mkewe “nimekuacha” na mke hudai talaka.

a) Haki ya mume kutoa talaka

- Mume amepewa nafasi ya kutaliki kwani ndiye anayetoa mahari, posa na ndiye kiongozi wa familia.


b) Haki ya mke kumuacha mumewe

- Kama tangu mwanzo, mume alikubaliana na mkewe kuwa huru kuvunja ndoa iwapo atamfanyia jambo lililo kinyume na sheria au asilolipenda.
- Kwa msingi huu, mke atadai talaka ya “Khul’u” au kwenda kwa Kadhi.



c) Kuvunja ndoa kwa makubaliano ya mume na mke

- Ikitokea mume na mke wakaamua kuachana kwa wema kwa talaka ya

“Mubaarat” itafaa kama haitavunja sheria au kupoteza haki ya mwingine.



d) Haki ya Mahakama ya Kiislamu kuvunja ndoa

- Wakati mwingine hata bila yak makubaliano ya mume na mke, mahakama ya Kiislamu ina haki ya kuvunja ndoa. Mfano wa talaka hii ni “Li’aan”.




Aina za Talaka

Kuna aina kuu mbili za talaka

a) Talaka rejea
b) Talaka isiyo rejewa



a) Aina za Talaka Rejea

- Ni aina ya talaka inayompa mume fursa ya kumrejea mkewe baada ya kumpa talaka katika kipindi cha twahara.
i. Talaka moja

Ni aina ya talaka ambapo mume humtamkia au kumuandikia mkewe

“nimekuacha” kwa talaka moja akiwa twahara.

ii. Talaka mbili

Ni aina ya talaka ambapo mume humuacha mara ya pili baada ya kumuacha kwa talaka moja kisha akamrejea katika twahara mbili tofauti.
Rejea Qur’an (2:229)



iii. Talaka ya ‘Ilaa

Ni aina ya talaka ambapo mume humtenga mkewe kwa zaidi ya miezi mine.

Rejea Qur’an (2:226)



iv. Talaka ya Zihaar

Ni aina ya talaka ambapo mume humsusa mkewe kwa kumfananisha na mama yake mzazi au maharim wake.
Kama hatatubia kabla ya kuisha miezi minne, mkewe atakuwa ameachika.

Rejea Qur’an (58:3-4)



v. Talaka ya Khul’u

Hii hupatikana kwa mke kudai talaka au kujivua katika ndoa kutokana na makubaliano tangu mwanzo katika mkataba wa ndoa.


Mke anayedai talaka, atalazimika kumrejeshea mume mahari aliyompa ili ajikomboe.
Rejea Qur’an (2:229)



vi. Talaka ya Mubaarat

Ni aina ya talaka ambapo mume na mke hukubaliana kuachana kwa wema baada ya kutofikia lengo la ndoa.


vii. Talaka kabla ya Jimai

Ni kuvunja mkataba wa ndoa kabla ya kufanya tendo la jimai (ndoa).

Talaka hii ina taratibu zifuatazo;

- Hapana kukaa eda kwa mwanamke aliyeachwa kabla ya tendoa la jimai.

- Kama mume ndiye aliyemuacha na ameshatoa mahari, hatadai chochote.

- Mume atalazimika kumpa mkewe kitoka nyumba kama ndiye aliyeamua kumuacha.
- Ikiwa mume alikuwa hajatoa mahari, atalazimika kutoa nusu ya mahari.

- Kama mke ndiye aliyedai talaka atamrudishia mumewe mahari aliyompa

Rejea Qur’an (2:236-237)



b) Aina ya Talaka Zisizorejewa

- Ni aina ya isiyompa mume fursa ya kumrejea mkewe baada ya kumuacha kwa talaka mbili ila mpaka aolewe na mume mwingine kisha aachike kisheria.
i. Talaka tatu (Tahliil)

Ni talaka ambayo mume humuacha mkewe baada ya kumrejea kutoka talaka mbili alizomuacha na kumrejea hapo awali.
Rejea Qur’an (2:230), (65:1)



ii. Talaka ya Li’aan

Ni talaka inayopatikana baada ya mume au mke kumshika ugoni mwenzake bila ya kuwa na mashahidi wanne.


Kila mmoja ataishuhudilia nafsi yake kwa kula kiapo mara tano mbele ya kadhi na baada ya hapo ndoa itavunjika na kutorejeana tena.
Rejea Qur’an (24:6-9)



Taratibu na Sharti za Kutaliki Kiislamu

i. Talaka hutolewa kwa matamshi au maandishi kuwa “nimekuacha” au maneno yenye maana mfano wake.


ii. Talaka itamkwe au itolewe mke akiwa katika kipindi cha twahara na wasiwe wamefanywa tendo la ndoa ndani ya twahara hiyo.

iii. Utoaji wa talaka ushuhudiwe na mashahidi wawili waadilifu.

iv. Mke aliyetalikiwa hukaa nyumbani kwa mumewe mpaka eda iishe ambapo hutengana tu kimalazi.

v. Kama mume na mke wataamua kurejeana kabla ya eda kwisha, watarejeana kwa wema kwa kumuahidi Allah (s.w) kuwa wataishi kwa wema.

vi. Baada ya eda kwisha, mume na mke watalazimika kuachana kwa wema kama anavyoamrisha Allah (s.w).

vii. Si halali kwa mume aliyetoa talaka kuchukua au kudai chochote katika vile alivyompa mkewe.

viii. Mume aliyemuacha mkewe, analazimika kumpa mtaliki wake kitoka nyumba.

Rejea Qur’an (2:236)

ix. Mke aliyeomba talaka anawajibika kujikomboa kwa kumrudishia mtalaka wake mahari aliyompa, na mume akisamehe hapana ubaya.



                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 10558

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Faida na umuhimu wa ndoa katika jamii

Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi

Soma Zaidi...
Swala ya witiri na faida zake, na jinsi ya kuiswali

Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya witiri na faida zake kwa mwenye kuiswali.

Soma Zaidi...
Baada ya kumzika maiti nini kifanyike kumsaidia marehemu

Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu

Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii.

Soma Zaidi...
Nguzo za udhu ni sita

Post hii itakufundisha kuhusu nguzo kuu sita za udhu.

Soma Zaidi...
Ni upibutaratibu wa kuingia eda na kutoka eda

Katika uislamu hakuna sheria ya mwanamke kuingizwa eda na kutolewa eda kama ilivyozoeleka. Endelea na post hii ujifunze zaidi

Soma Zaidi...