20.
20. Kuepukana na Kulaani Ovyo
Kulaani ovyo kumekatazwa katika Uislamu. Mtu anapolaani wengine anakuwa amejisahau kuwa naye ni mkosaji. Mtume (s.a.w) ametukataza kulaani ovyo katika Hadithi zifuatazo:
Ibn ‘Umar (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Si sawa kwa Muumini kuwa mkubwa wa kulaani”. Na katika upokezi mwingine, Mtume amesema, “Si stahiki ya Muumini kuwa mkubwa wa kulaani”. (Tirm idh).
Abu Dard (r.a) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allah akisema: “Watu wenye mazoea ya kulaani hawatakuwa mashahidi wala wenye kushufaia katika siku ya Kiyama ”. (Muslim).
Ibn Abbas (ra) ameeleza kuwa upepo ulipeperusha nguo ya mtu. Kwa hiyo aliulaani (upepo). Mtume wa Allah (saw) alisema ; “Usiulaani kwa sababu umeamrishwa ufanye hivyo na kwa sababu laana inakurudia mwenye kulaani kitu kisichostahiki kulaaniwa (kisicho na hatia). (Tirmidh na Abu-Daud).
Muislamu anatakiwa ajiepushe na tabia ya kulaani na badala yake awe mwingi wa kuwasamehe wenye kumkosea na kuwatakia msamaha kwa Allah (s.w) ili naye asamehewe dhambi zake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukugundisha maana ya hadathi pamoja na kutaja aina za hadathi
Soma Zaidi...Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa orodha ya vitu vilivyo najisi.
Soma Zaidi...kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah.
Soma Zaidi...