Hadithi Ya 32: Kusiwe Na Kudhuriana Wala Kulipiza Dhara

الحديث الثاني والثلاثون "لا ضرر ولا ضرار" عَنْ أَبىِ سَعيدٍ سَعْدِ بْن مَالكِ بْن سِنَانٍ الْخُدريِّ رضي الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه   وسلم    قَالَ :(( لاَ ضَرَرَ وَلاَ ضِرَارَ )) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَالدَّارَقُطْنِيّ، وَغَيْرُهُمَا مُسْنَدًا. وَرَوَاهُ مَالِكٌ فِي "الْمُوَطَّإِ مُرْسَلاً عَنْ عَمْرِو بْنِ يَحْيَى عَنْ أَبِيهِ عَنْ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم  مُرْسَلًا، فَأَسْقَطَ أَبَا سَعِيدٍ، وَلَهُ طُرُقٌ يُقَوِّي بَعْضُهَا بَعْضًا. 


KUSIWE NA KUDHURIANA WALA KULIPIZA DHARA

 

Kutoka kwa Abu Sa'iid Sa'ad Ibn Malik Ibn Sinaan Al-Khudhri رضي الله عنه  ambaye alisema  kuwa Mtumeصلى الله عليه وسلم  kasema:

Kusiwe na kudhuriana wala kulipa dhara.

 

Imesimuliwa na Ibn Maajah, Daaraqutni na wengineo na ina kiwango cha 'Musnad' 

 

Vile vile imesimuliwa na Malik katika (kitabu) Al-Muwatta kama 'Mursal'

Inayo mtiririko wa mapokezi kutoka kwa 'Amr Ibn Yahya, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mtumeصلى الله عليه وسلم  hata ukimuacha Abu Sa'id bado inayo mtiririko wa mapokezi unayoiunga mkono.