Hadithi Ya 31: Upe Ulimwengu Kisogo Allaah Atakupenda

الحديث الحادي والثلاثون

"ازهد في الدنيا يحبك الله"

عَنْ أَبِي العَبّاسِ سَهلِ بْن سَعْدٍ السّاعِدِيِّ رضي الله عنه  قَالَ : جَاءَ رَجُلُ إِلى النَبِي صلى الله عليه   وسلم   فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ  . فَقَالَ: (( ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النّاسُ)).

  رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ  وَغَيْرُهُ بِأَسَانِيدَ حَسَنَةٍ. 

 


HADITHI YA 31 UPE ULIMWENGU KISOGO ALLAAH ATAKUPENDA

 

Kutoka kwa Abu Al-‘Abbaas Sahl bin Sa'ad As-Saa'idiy رضي الله عنه  ambaye alisema:

Mtu alikuja kwa Mtume صلى الله عليه وسلم  na akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, nielekeze kitendo ambacho  nikitenda  kitasababisha Mola kunipenda na watu kunipenda.  Akasema  (صلى الله عليه  وسلم  ) : Upe ulimwengu kisogo na Mwenyeezi Mungu atakupenda, na jiepushe na mali za watu na watu watakupenda.

Imesimuliwa na Ibn Maajah na wengineo kwa mtiririko mzuri wa mapokezi.*

*Hata hivyo wanachuoni wa Hadiyth wameeleza kuwa Hadiyth hii ni dhaifu kutokana na udhaifu wa sanad yake japo An-Nawawiy kaitumia na kasema ina sanad nzuri.