image

Hali ambazo akiwa nazo mwenye kuomba dua dua yake hujibiwa

Post hii inakwenda kukifundisha nibhali zipi ukiwa nazo, basi dua yako kuhubaliwa kwa urahisi.


HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA.
1.Dua ya kumuombea aliye mbali. Chukulia mfano una ndugu yako yupo nchi nyingine ama mji mwingine kisha ukamkumbuka na ukataka kumuombea dua, basi dua hii itajibiwa tu. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua iliyo nyepesi (na haraka ) kujibiwa ni dua ya mtu kumuombea aliye mbali” (amepokea Abuu Daud na Tirmidh kwa isnad sahihi). Pia amesimulia Abuu Dardaa رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “dua ya mtu muislamu ni yenye kujibiwa anapomuombea ndugu yake aliye mbali. Juu ya kichwa chake kuna Malaika anaitikia ‘aamiin’ na wewe upate mfano wa wake”. (amepokea Ahmd na Muslim).

2.Dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa. Hali za watu watatu hawa wakiomba dua Allah atajibu dua zao bila ya shaka. Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema ‏ "‏ ثَلاَثُ دَعَوَاتٍ يُسْتَجَابُ لَهُنَّ لاَ شَكَّ فِيهِنَّ دَعْوَةُ الْمَظْلُومِ وَدَعْوَةُ الْمُسَافِرِ وَدَعْوَةُ الْوَالِدِ لِوَلَدِهِ

3.“dua za watu watatu (hawa) ni zenye kujibiwa na hakuna shaka juu ya hili: dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa”. (amepokea Abuu Daud, Ahmad na Tirmidh kwa sanad sahihi).

4.Dua ya mwenye swaum (funga), imamu muadilifu, na mwenye kudhulumiwa. Watu hawa dua zao zitajibiwa tu, kingozi muadilifu, mtu aliyekuwa kwenye funga na kabla hajafuturu na mtu aliyedhulumiwa. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم watu watatu dua zao hazirudi: mwenye funga mpaka afutauru, imamu muadilifu (kiongozi muadilifu), na mwenye kudhulumiwa.…….” (amepokea tirmidh kwa isnad sahihi). Soma zaid

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1063


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Hadithi Ya 22: Je, Nikiswali Swalah Za Fardhi, Nikafunga Ramadhaan
Soma Zaidi...

DUA BAADA YA TAHIYATU, NA KUTOA SALAMU KWENYE SWALA
13. Soma Zaidi...

kuwa na ikhlas
Ikhlas ni kufanya kila jambo jema kwa ajili ya Allah (s. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 27: Uadilifu Ni Tabia Nzuri
Soma Zaidi...

KUINGIA KWA WAGENI
Download kitabu Hiki Bofya hapa KUINGIA KWA WAGENI Amina na Sadie walimuonea huruma wakamuomba Zubeid amruhusu abakie. Soma Zaidi...

DUA 94 - 114
DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 94. Soma Zaidi...

Hadithi ya tatu:ukarimu na kusaidiana
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hadithi Ya 25: Wenye Mali Wameondoka Na Fungu (jaza) Kubwa
Soma Zaidi...

DUA 120
Soma Zaidi...

Dua sehemu 03
Zijuwe njia ambazo Allah hujibu Dua yako. Tambua kama umejibiwa dua yako au bodo, soma darsa za dua hapa. Soma Zaidi...

Namna ya kumuosha maiti hatua kwa hatua, nguzo na sunnah za josho la maiti
1. Soma Zaidi...

Dua Sehemu ya 01
Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua? Soma Zaidi...