Hadithi ya tatu:ukarimu na kusaidiana
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
- Hadith ya Tatu: Ukarimu na Kusaidiana.
Kutoka kwa Abi Saidil-Khudhur (r.a) kasema: ilitokezea tumo safarini pamoja na Mtume (s.a.w); akaja mtu mmoja juu ya kipando chake, akawa anaangaza kulia na kushoto, Mtume (s.a.w) akasema;
“Mwenye kipando cha ziada na ampe msaada asiye na kipando, na mwenye chakula kilichozidi (matumizi yake) na ampe msaada mwenye kukihitaji (asiyenacho)”
Akataja aina mbali mbali za mali mpaka tukaona (tukajua) kwamba hatuna haki ya kuweka ziada (baada ya matumizi yetu).
(Ameipokea Muslim)
Mafunzo ya Hadith kwa Ufupi:
- Ni wajibu wa kila muislamu aliyenacho kumtilia hima kila anayehitaji msaada wa kibinaadamu.
- Ugawaji mbaya wa rasilimali na utajiri ndio sababu ya kuwepo matabaka ndani ya jamii.
- Uislamu umekataza kuhodhi bidhaa muhimu kwani kinyume cha sheria.
- Uislamu umetilia mkazo maisha bora kwa kila raia na kukataza kufanya israfu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 web hosting 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
UKITAKA KUOMBA BASI MUOMBE ALLAH, UKIMKUMBUKA WAKATI WA RAHA ATAKUKUMBUKA WAKATI WA DHIKI, SHIDA NA TAABU
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: "كُنْت خَلْفَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم يَوْمًا، فَقَالَ: ي...
Soma Zaidi...Darsa 5: Kujiepusha na tabia za unafiki na kutimiza ahadi
Katika Darsa hii tutajifnza kuhusu kujiepusha na tabia za unafiki na kitimiza ahadi.
Soma Zaidi...Darsa za Dua
Download kitabu hiki na upate kusoma zaidi ya dua 120, pamoja na darsa mbalimbali za dini ya kiislamu.
Soma Zaidi...