picha

DUA 85 - 93

SWALA YA MTUME 85.

DUA 85 - 93


SWALA YA MTUME
85.Kumswalia Mtume (s.a.w) ni nguzo ya swala inayofuatia baada ya kusoma Tahiyyatu. Kumswalia Mtume si faradhi katika swala tu bali pia ni faradhi kumswalia kila anapotajwa kwa jina lake. Msisitizo wa amri ya kumswalia Mtume unaonekana katika aya ifuatayo:

86.“Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume; na Malaika wake (wanamuombea dua). Basi; enyi Mlioamini msalieni (Mtume, muombeeni Rehema) na amani”. (33:56)

87.Pia katika maana ya hadithi nyingine Mtume (s.a.w) amesema kuwa bahili ni mtu ambaye atatajwa Mtume (s.a.w) kisha asimswalie.

88.Pia hadithi zifuatazo zinasisitiza umuhimu wa kumswalia Mtume (s.a.w) kila atajwapo na kila mtu apatapo wasaa. Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Bakhili ni yule anayesikia nikitajwa, lakini haniswalii. (hanitakii rehma). (Tirmidh).

89.Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Anayenitakia Rehma (anayeniswalia) mara moja, Allah humrehemu mara kumi”. (Muslim).

90.“Ibn Mas’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakayekuwa kipenzi changu katika watu, katika siku ya Kiama atakuwa ni yule aliye mbele kuliko wote katika kunitakia Rehma (kuniswalia). (Tirmidh).

91.Namna ya kumswalia Mtume (s.a.w) imeelezwa katika Hadithi nyingi lakini iliyomashuhuri katika hizo ni ile iliyosimuliwa na Abdur- Rahman bin Ubaidillah(r.a) na kupokelewa na Maimamu wote wa Hadithi kuwa Mtume (s,.a.w) ametufundisha tumswalie (tumtakie Rehma) kama ifuatavyo;

92.“Allahumma swalli ‘alaa muhammad wa’alaa aliy Muhammad kamaa swallaita ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik ‘alaa muhammad wa’alaa ali muhammad kamaa barakta ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahima innaka hamiidum-majid”

93.Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.


                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views 1473

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 ai web app     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

DUA ZA WAKATI WA SHIDA

DUA ZA WAKATI WA SHIDA 1.

Soma Zaidi...
DUA 94 - 114

DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 94.

Soma Zaidi...
Dua za kumuomba Allah wakati wa shida na tabu ama matatizo

Post hii inakwenda kukufundisha dua ambazo ni muhimu kuzisoma wakayi wa shida na taabu.

Soma Zaidi...
Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu

Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.

Soma Zaidi...
Faida za swala ya Mtume

Hapa utajifunza fadhila za kumswalia Mtume (s.a.w)

Soma Zaidi...
DUA ZA KUONDOA WASIWASI

DUA ZA KUONDOA MAUMIVU MWILINI Katika uislamu Allah amejaalia dawa katika kufuata sunnah.

Soma Zaidi...