21.
21.Suratul-Ikhlas (112:1-4) Sema, Yeye ni Allah aliye mmoja tu Allah ndiye anayestahiki 475 kukusudiwa (na viumbe vyote). Hakuzaa wala hakuzaliwa. Hakuna hata mmoja anayefanana naye." (112:1-4)
22.Suratul-Falaq (113:1-5) Sema: Ninajikinga kwa Mola wa ulimwengu wote.Na shari ya Alivyoviumba. Na shari ya giza la usiku liingiapo.Na shari ya wale wanaopulizia mafundoni.Na shari ya hasidi anapohusudu. (113:1-5)
23.Suratun-Naas (114:1-6) Sema: Ninajikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea watu. Mfalme wa watu. Muabudiwa wa watu. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma. Atiaye wasi wasi nyoyoni mwa watu. (Ambaye ni) katika majini na watu." (114:1-6)
24.Kumswalia Mtume Asubuhi na Jioni Mtume (s.a.w) amesema:Mwenye kuniombea rehema asubuhi mara kumi na jioni mara kumi, nitamuombea shufaa (masamaha) siku ya kiyama.
25.โAllahumma swali'alaa Muhammad wa'alaa aali Muhammad, kamaa swallayta 'alaa Ibraahiima wa'alaa aali Ibraahiim, Innaka hamidun majiidu, allahumma baarik-'alaa Muhammad wa-'alaa aali Muhammad, kamaa barak-ta 'alaa Ibraahiima wa-'alaa aalii Ibraahiima, Innaka hamidunmajiidu."
Ee Allah! Mrehemu Muhammad na jamaa zake (wafuasi wake) Muhammad kama ulivyo mrehemu Ibrahiim na jamaa zake (wafuasi wake) Ibrahiim, hakika wewe ni mwenye kusifika mtukufu. Ee Allah! Mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na jamaa zake Ibrahiim, Hakika wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu. Mtume (s.a.w) amesema: "Anayeniswalia mara moja, Allah (s.w) humswalia mara kumi." (Muslimu).
26.Pia Mtume (s.a.w) amesema: โBahili ni yule ninapotajwa, haniswalii (haniombei rehema na amani kwa Allah)." (Tirmidh) Kumswalia Mtume (s.a.w) kumeamrishwa kwa waumini kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: โHakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Mtume (wanamtakia rehema na amani). Basi, enyi mlioamini mswalieni (muombeeni Mtume) rehema na amani." (33:56)
27.Kuomba Msamaha na Kutubia Amesema Mtume (s.a.w): โNaapa kwa Mwenyezi Mungu hakika mimi ninamtaka msamaha Mwenyezi Mungu na ninatubia kwake katika kila siku zaidi ya mara sabini." (Al-Bukhari).
28.โAstagh-firu llaha waatuubu ilahi." (mara mia) โNamuomba msamaha Allah na ninatubia kwake." 29.Pia Mtume (s.a.w) amesema: "Yeyote anayesoma maneno yafuatayo, Mwenyezi Mungu atamsamehe hatakama anamakosa ya kukimbia vitani:
30.โAstagh-firu llaahal-'adhiimal-ladhii laaillaha illahuwalhayyul qayyuumu wa-atuubu ilayhi." โNamuomba msamaha Allah, Mtukufu ambaye hapana Mola ila yeye, aliye Hai, aliyesimama kwa dhati yake na ninatubia kwake."
31.Amesema Mtume (s.a.w): "Hakuna mja yeyote yule anayefanya dhambi kisha akatawadha vizuri na akaswali rakaa mbili, kisha akamtaka Mwenyezi Mungu msamaha ila atasamehewa". (Abu Daud na Tirmidh) 12. Dhikri ya kuleta baada ya kupatwa na janga au balaa โLaailaha illa llahul-'adhwiimul-haliimu, laa ilaha illa llahu r a b b u l - ' a r - s h i l ' a d hwi imi , L a a i l a h a i l l a l l a h u rabbussamaawaat warabbul-ardhwi,warabbul-'ar-shilkariimi.
โHapana Mola ila Allah, aliye mtukufu mpole, Hapana Mola ila Allah, Mola wa arshi tukufu, Hapana Mola ila Allah, Mola wa mbingu na ardhi na Mola wa arshi tukufu. โLaailaha illaa-anta Sub-hanaanaka inny kuntuminal Dhw- Dhwaalimiina." Hapana Mola ila Wewe, Utukufu ni wako, hakika mimi ni miongoni mwa waliodhulumu nafsi zao. 13.Unapokutana na adui au mtawala dhalimu โHasbunallahu wani'imal-wakiilu" โAllah anatutosheleza Naye ni mbora wa kutegemewa.
Umeionaje Makala hii.. ?
MAkala hii itakwenda kukufundisha jinsi ya kutoa salamu kwenye uislamu
Soma Zaidi...ADHKARI MBALIMBALI NA DUA Hapa tutajifunza dua mbalimbali ambazo ni adhkari.
Soma Zaidi...Hapa nitakuletea baadhi tu ya adhkari ambazo ni muhimu kwa muislamu
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Dua ni moja ya ibada ambazo zinamfanya mja awe karibu na Mweznyezi Mungu. Allah amesisitiza tumuombe dua kwa shida zetu zote, pia akaahidi kuwa atatujibu maombi yetu muda wowote tutakao muomba. Sasa ni zipi nyakati nzuri zaidi kuomb adua?
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ููุฑูููุฑูุฉู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุฃูููู ุฑูุฌูููุง ููุงูู ููููููุจูููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ุฃูููุตูููู.
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ู ูุณูุนููุฏู ุนูููุจูุฉู ุจููู ุนูู ูุฑูู ุงููุฃูููุตูุงุฑูููู ุงููุจูุฏูุฑูููู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ููุงูู: ููุงูู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนู?...
Soma Zaidi...