Nafasi ya serikali katika ugawajiKatika suala la ugawaji, wajibu wa serikali ya Kiislamu upo katika maeneo makuu yafuatayo:(i)Kusimamia utoaji na ukusanyaji wa zaka. Serikali ndiyo yenye wajibu wa kuhakikisha kuwa kila anayepaswa kutoa Zaka anatoa na serikali inasimamia ukusanyaji wake.(ii)Kutoza na kukusanya kodi iwapo zaka haiku to s ha.(iii)Kutoza na kukusanya Jizya (aina ya kodi) kutoka kwa wasiokuwa Waislamu (dhimmi) wanaoishi katika dola ya Kiislamu.(iv)Serikali ya Kiislamu pia inao wajibu wa kuchukua hatua za kupunguza tafauti kati ya maskini na matajiri, kwa kugawa Zakat na kutoa huduma muhimu bure kwa maskini.