Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Kwanza, serikali ya Kiislamu inao wajibu wa kuandaa mazingira mazuri ya kihuduma na kimawasiliano kuwawezesha raia kujiletea maendeleo na inao wajibu wa kuingilia kati ili kusimamia haki na kuzuia dhulma. Ni wakati gani kwa mfano ambapo serikali inaweza kuingilia kati. Allah ndiye aliyeziumba rasilimali zilizopo duniani na hivyo ni wajibu wa binaadamu kuzitumia rasilimali hizo kwa manufaa ya watu na kwa ufanisi. Hivyo serikali yaweza kuingilia kati iwapo rasilimali hizo zitatumiwa kuwadhulumu watu au hazitatumika kwa ufanisi.
Pili, baadhi ya kazi ni haramu katika Uislamu kwa sababu zimefungamana na mambo ya haramu, kama vile kamari, umalaya, uchawi, ulevi n.k. Ni wajibu wa serikali kuona kuwa mambo hayo hayapewi nafasi katika jamii.
Tatu, ni wajibu wa serikali pia kutoa fursa sawa kwa watu wote ya kuendeleza na kuvikuza vipaji vyao kwa kuwapa fursa sawa za elimu na mafunzo. Ni wajibu wa serikali kugharamia elimu kwa ajili ya manufaa ya watu wote. Elimu ni haki ya msingi kwa wanadamu wote.
Nne, ni wajibu pia wa serikali kuhakikisha kuwa hata katika zile kazi za halali kisheria zinafanywa kwa uadilifu pasi na dhulma yoyote. Yaani Serikali ihakikishe mathalani kuwa bidhaa zinazotolewa zimefikia ubora kwa wanaoizalisha, kuona kuwa uadilifu wa kitaalamu unadumishwa, kuona kuwa Wafanyakazi wanalipwa mishahara kwa haki.
Hata hivyo, Uislamu hauelemei upande mmoja tu wa kumtetea mfanyakazi peke yake wala kumtetea mwajiri peke yake. Wafanyakazi pia wakileta madai yasiyo ya haki ni juu ya serikali kuingilia kati.
Tano, ni wajibu wa serikali pia kuzuia mambo yanayoweza kudhuru watu, kwa mfano kama mtu akijenga kiwanda cha hatari katika makazi wanamoishi watu. Au hata mambo yanayoweza kuwatesa wanyama, kama kuwabebesha mizigo mizito sana hadi wanaanguka na kuvunjika miguu au kufa, au kuwafanyisha kazi kwa mateso makubwa na kutowapa chakula cha kutosha. Hali kadhalika serikali inaweza kwa mfano kuzuia magari au meli iliyopakia abiria au mizigo kuliko uwezo wake.
Sita, katika suala la usambazaji wa bidhaa, serikali inaweza kuingilia kati iwapo watu watahodhi vyakula na bidhaa nyingine muhimu kwa lengo la kupandisha bei.
Saba, ni wajibu wa serikali kujenga miundo mbinu (in-frastructures) na kuidhibiti, kwa mfano kujenga barabara, madaraja, reli, kusambaza maji ya bomba, kujenga mitambo ya umeme, simu n.k.
Wakati wa Ukhalifa wake, Ali (r.a) alimwambia Nahri, ambaye alikuwa mkuu wa jimbo la Misri; βUsifanye ukusanyaji wa kodi ya ardhi kuwa ndiyo kazi yako kubwa; kazi yako kubwa ni kuindeleza ardhi hiyo.β
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Dua za Mitume na Manabii π2 kitabu cha Simulizi π3 Kitabu cha Afya π4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π5 Kitau cha Fiqh π6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu
Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii.
Soma Zaidi...Ufafanuzi kuhudu mgogoro wa mwezi ni muda gani mtu aanze kufunga.
Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi.
Soma Zaidi...Mambo yanayodhaniwa kuwa yanaharibu funga lakini hayaharibu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jinsi ya kujitwaharisha Najisi hafifu na najisi ndogo
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi hafifu na najisi ndogo.
Soma Zaidi...Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir
Soma Zaidi...Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?
Soma Zaidi...