Mafungu ya urithi yaliyotajwa katika haya sita yafutayo:
1.Nusu (1/2)
2.Robo (1/4)
3.Thuluthi. (1/3)
4.Thuluthi mbili (2/3) 5.Sudusi. (1/6)
6.Thumuni (1/8)

Mwenye kupewa mafungu
Katika warithi kuna wenye kupata mafungu maalum katika hayo mafungu sita; na kuna wasiokuwa na mafungu maalum ambao hupata kilichobakia baada ya wenye mafungu kuchukua mafungu yao au kupata mali yote ikiwa hapana wenye mafungu. Wasio na mafungu huitwa asaba.
Wenye mafungu maalum katika urithi ni watu kumi na na mbili (12) wafuatao:


I .Baba.
2.Babu.
3.Binti. 4.Binti wa mtoto mwanamume (mjukuu).
5.Ndugu wa kwa mama.
6. Dada wa kwa baba na mama.
7.Dada wa kwa baba.
8.Dada wa kwa mama.
9.Mama.
1O.Bibi.
11.Mume.
12. Mke.