Yajuwe mandalizi ya Ibada ya hija

Yajuwe mandalizi ya Ibada ya hija

Maandalizi ya Safari ya Hija



Maandalizi ya Hija hayaanzii kwenye miezi ya Hija, bali huanzia mbali katika umri wa mtu. Tunafahamu kuwa utekelezaji wa Ibada ya Hija unahitaji kuwa na uwezo wa kifedha (kimali). Hivyo Muislamu wa kweli katika kuchuma na kutumia mali yake, hana budi kuzingatia suala la nguzo ya Zaka na nguzo ya Hija. Muislamu atakapoweka mbele yake wazo la kutoa Zaka na Kuhiji, daima atachunga mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) katika kuchuma kwake, kwani anafahamu wazi kuwa mali iliyochumwa kwa njia za haramu haifai kutolea Zaka au Kuhijia. Hebu tuzingatie hadithi ifuatayo:



Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Swala haikubaliwi bila ya Twahara, wala Sadaqa haikubaliwi kama inatolewa kutokana na mali iliyochumwa kwa njia za haramu. (Muslim).



Halikadhalika, kutokana na hadithi hii, Hija haitasihi endapo mtu atahiji kwa kutumia mali iliyopatikana kwa njia za haramu. Hivyo, fikra ya kuhiji, humzoesha Muumini kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu katika uchumi.



Pia fikra ya Hija humzoesha Muumini kutumia mali yake kwenye mambo muhimu tu ili kumuwezesha kuweka akiba kwa ajili ya Hija. Yaani fikra ya kutekeleza nguzo hii, humuepusha na ubadhirifu au utumiaji bila ya haja na bila ya ratiba.



Mtu anayekusudia kuhiji azidishe kutenda wema. Ajizatiti katika kusimamisha swala tano, kutoa Zaka, kufunga Ramadhani, kuwahurumia wanyonge kwa kuwapa misaada wanayohitajia na kusuhubiana vizuri na watu wote kwa ujumla. Amuombe msamaha kila aliyemkosea na amsamehe kila aliyemkosea. Pia mwenye kunuia Hija anatakiwa ajitahidi kujiepusha na maovu na azidishe kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa yote aliyokosea kwa kujua au kutojua na yaliyowazi au yaliyofichikana. Katika Qur-an Mwenyezi Mungu (s.w) anaagiza kwa wanaokusudia kuhiji:


“Na anayekusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu, wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija. Na kheri yoyote mnayoifanya Mw enyezi Mungu anajua …” (2:197)



Utaona mtu mwenye fikra ya kutekeleza ibada ya Hija daima atakuwa mwangalifu katika mwenendo wake wa kila siku. Atajitahidi kutekeleza maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) na kujiepusha na makatazo yake yote atajitahidi kuwatendea wema wanaadamu wenzake na kila mara atakuwa mwenye kujiandaa kuitika mwito wa Mola wake (Labbayka), kama vile mtu anayejiandaa kukutana na Mola wake kwa kifo, muda mfupi ujao.






                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1564

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 web hosting    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Mwenendo wa Mtu aliyetoa Shahada

Muislamu aliyetoa shahada ya kweli hanabudi kumfanya Mtume (s.

Soma Zaidi...
Taratibu za kutaliki katika uislamu.

Hapa utajifunza taratibu zinazofuatwa wakati wa kukusudia kumuacha mke. Pia utajifunza sababu za kiwepo kwa eda baada ya kuachwa mwanamke.

Soma Zaidi...
Mifano na namna ya kurithisha

Ugawaji wa mirathi-Mume ana nusu (1/2) = 1/2 -Mama ana sudusi.

Soma Zaidi...
Nini maana ya kusimamisha swala?

Je kusimamisha swala kuna maana gani kwenye uislamu?

Soma Zaidi...
udhaifu wa hoja za kuunga mkono kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango

Udhaifu wa Hoja za Kudhibiti Uzazi:Hoja nyingi zinazotolewa kuunga mkono udhibiti wa uzazi zimejengwa juu ya hali na mazingira ya maisha yaliyoletwa na utamaduni na maendeleo ya nchi za Ulaya na Marekani.

Soma Zaidi...
Haki za raia katika dola ya kiislamu

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...