KuzuilianaTumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10.
Kuzuiliana
Tumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10. Lakini wote hawa 25 wakikutana pamoja hawawezi kurithi wote bali baadhi yao huwazuilia wengine wasipate kitu au wasipate fungu kubwa. Katika kipengele hiki tunaonyesha wanaozuiliwa na wasiozuiliwa.
1.Mtoto mwanamume hazuiliwi na mtu.
2.Mjukuu huzuiliwa na mtoto mwanamume na kila mtoto wa kiume aliyeko mbali huzuiliwa na aliyoko karibu na marehemu. 3.baba hazuiliwi na mtu.
4.Babu wa upande wowote huzuiliwa na baba au babu wa karibu zaidi (kama vile baba yake baba humzuilia babu yake baba).
5.Ndugu wa kwa baba huzuiliwa na ndugu wa kwa baba na mama; na kila amzuiliaye yeye (huyo ndugu wa kwa baba na mama) vile vile huzuiliwa na dada wa kwa baba na mama akiwa pamoja na binti au binti wa mtoto wa kiume (mjukuu) au wote wawili.
6.Ndugu wa kwa mama huzuiliwa na mtoto au mtoto wa mtoto mwanamume au baba au babu.
7.Mume hazuiliwi na mtu wala
8.Mke hazuiliwi na mtu.
9.Binti hazuiliwi.
1O.Mama hazuiliwi.
11.Bibi huzuiliwa na mama.
Umeionaje Makala hii.. ?
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?
Soma Zaidi...Zoezi hili linamaswali mbalimbali kuhusiana na swala na masharti ya swala.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kuchunga au kutekeleza ahadi ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli.
Soma Zaidi...