Navigation Menu



image

Suluhu na kupatanisha kati ya mke na mume

Suluhu na kupatanisha kati ya mke na mume

Suluhu Kati ya Mume na Mke



Wanaadamu wanapoishi pamoja, kutokana na udhaifu wa kibinaadamu kukwaana na kugombana ni jambo Ia kawaida. Hivyo mume na mke ambao wako karibu sana, hawana budi kuvumiliana kwa kiasi kikubwa. Mmoja akimwona mwenzie amekasirika hana budi kutulizana na kujifanya kama mjinga. Kila mmoja hana budi kujitahidi kwa jitihada zake zote kumtendea wema mwenzake na kumpa haki zake.


Vile vile kila mmoja hana budi kuwa tayari kusamehe haki ndogo ndogo alizonyimwa na mwenziwe. Mwenendo huu wa kuvumiliana na kusameheana hudumisha amani na upendo katika nyumba. Hatuna budi kukumbuka kuwa kuvumiliana na kusameheana, hakuleti tu furaha na amani katika nyumba na katika jamii kwa ujumla bali pia ni matendo ya kiucha-Mungu yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:



"... Na wasamehe na waachilie mbali (yaliyopita). Je, nyinyi hampendi Mwenyezi Mungu akusameheni? Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwingi wa rehema (basi nanyi sWkeni na sfa hizi) ". (24:22).


Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na ubaya huo; lakini anayesamehe na kusuluhisha ugomvi, ujira wake uko kwa Mwenyezi Mungu; bila shaka yeye hawapendi madhalimu.. (42:40)



Aya hizi zinatufahamisha kuwa kusamehe ni sababu ya mtu kusamehewa makosa yake na Mola wake na pia ni sababu ya kupata malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w). Hivyo ikitokea mume na mke wakahitilafiana na kugombana, hawana budi kujisuluhisha wenyewe kwa njia hii ya kusubiri na kusameheana kama Mwenyezi Mungu (s.w) anavyotushauri katika Qur-an:


Na kama mke akiona kwa mume wake kugombana gombana na kutengana tengana, basi si vibaya kwao wakitengeneza baina yao suluhu (njema wakastahimiliana bila kuachana) maana suihu ni kitu bora. Na nafsi zimewekewa ubakhili mbele (hakuna mtu anayetaka kumuachia mwingine haki yake). Na kama mkifanya mema (kuwafanyia wake zenu) na mkimcha Mwenyezi Mungu (msiwapunguzie haki zao, bila shaka Mwenyezi Mungu atakulipeni) kwani Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda. (4:128).


Ikitokea mume na mke wenyewe wameshindwa kujisuluhisha mpaka ugomvi ukajitokeza nje, Waislamu walio karibu nao kwa urafiki, ujirani, udugu, n.k. waingilie kati na kuwapatanisha ndugu zao kabla sumu ya shetani haijaenea katika nyumba. Msuluhishaji atumie busara kubwa na ajitahidi kwa kadiri ya uwezo wake katika kufanya kazi hiyo akijua kuwa hiyo ni kazi nyeti na yenye malipo makubwa sana mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) kama tunavyosoma katika Qur-an:


Hakuna kheri katika mengi wanayoshauriana kwa sin. Ispokuwa (mashauri ya) wale wanaoamnisha kutoa sadaqa au kufanya mema au kupatanisha baina ya watu. Na atakayefanya hivi kwa kutaka nadhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutampa ujina mkubwa. (4:114).



Msuluhishi huyu akishindwa, kabla mume hajakimbilia kutoa talaka au mke hajakimbilia kudai talaka, ni vyema Waislamu hawa wakashitakie ugomvi wao kwa kadhi. Kadhi atajitahidi kuwapa mawaidha mazuri na kumkumbusha kila mmoja haki zake na wajibu wake kwa mwingine, kisha baada ya kumsikiliza kila mmoja wao kuhusiana na ugomvi wao, hatatoa uamuzi pale pale bali ataomba muda wa kupekua zaidi kesi hiyo. Kadhi atachagua ndugu waadilifu kutoka kila upande watakaomsaidia kupeleleza kiini cha ugomvi na ni nani aliye mkosea mwenziwe.



Kisha Kadhi atamuita mume na mke na kuwapatanisha akisaidiana na jamaa wa kwa mume na mke. Kadhi atamsihi mkosa asirejee tena makosa yake na amtake mwenziwe msamaha na vile vile aombe msamaha kwa Mwenyezi Mungu (s.w). Pia aliyekosewa ataombwa amsamehe mwenzake ili naye Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake na kupata ujira mkubwa kutoka kwake. Wawili hawa wakiwa na nia ya kupatana, baada ya hatua hizi, Mwenyezi Mungu (s.w) ameahidi kuwapatanisha kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:



Na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basipelekeni mwamuzi mmoja katikajamaa za mwanamume na mmoja katika jamaa za mwanamke.Kama wakitaka map atano Mwenyezi Mungu atawapatanisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa habari za sin na habani za dhahini. (4:35).



Ni nani mbora wa kutekeleza ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu? Hivyo, mume na mke wasikimbilie talaka bali wajitahidi kutafuta suluhu baina yao kwa nia njema na kwa jitihada zao zote. Ndipo waachane endapo suluhu itashindikana kabisa. Na kutokana na ahadi hii, haitashindikana endapo watakuwa wacha Mungu.
Pia kabla ya kufikia hatua ya talaka, mume na mke wanaruhusiwa kutengana kwa muda wa miezi mine. Suluhu ikishindikana katika muda huo itabidi waachane kama tunavyojifunza katika Qur-an:


Kwa wale wanaoapa kwamba watajitenga na wake zao, (muda wao) ni kungojewa miezi mine. Na kama wakinejea, basi Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe, mwingi wa kunehemu.Na wakiazimia kuacha (basi) Mwenyezi Mungu ni mwenye kusikia, mwenye kujua. (2:226-22 7)




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 767


Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰5 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Namna ya kujitwaharisha mkojo wa Mtoto mdogo Najisi Hafifu
Soma Zaidi...

Mifano na namna ya kurithisha
Ugawaji wa mirathi-Mume ana nusu (1/2) = 1/2 -Mama ana sudusi. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuswali kuswali swala ya maiti
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya maiti, nguzo za swala ya maiti, sharti za swwla ya maiti na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Maswali juu ya Nguzo za uislamu
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

KUSOMA TAHIYATU NA KUMSWALIA MTUME KWENYE SWALA
11. Soma Zaidi...

Mwenendo wa Mtu aliyetoa Shahada
Muislamu aliyetoa shahada ya kweli hanabudiย kumfanya Mtume (s. Soma Zaidi...

Jukumu la serikali katika kuzuia dhuluma
Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutawadha kama aalivyotawadha Mtume Muhammad (s.a.w)
Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume Soma Zaidi...

Namna ya kuswali hatuwa kwa hatuwq
Post hii itakufundisha jinsi ya kuswali hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Lengo la kufunga ramadhani, na faida zake, nguzo za kufunga na sharti zake
Saumu (Funga). Soma Zaidi...

Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume. Soma Zaidi...

Ufumbuzi wa tatizo la riba.
Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba. Soma Zaidi...