Dhana ya mirathi na kurithi katika zama za ujahiliya
Mirathi katika jamii za kijahiliKatika jamii nyingi za kijahili kama vile jamii ya Waarabu kabla ya Mtume Muhammad (s.
Mirathi katika jamii za kijahili
Katika jamii nyingi za kijahili kama vile jamii ya Waarabu kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w), watoto wadogo ambao hawajafikia baleghe, walemavu na wazee ambao hawakuwa na uwezo wa kupigana vita katika kuihami heshima ya familia na kabila kwa ujumla, hawakupata chochote katika mirathi. Aghalabu katika jamii zote za kijahili mwanamke akiwa binti au mke, au mama au katika uhusiano wowote ule kwa marehemu, hakuwa na haki yoyote ile katika urithi.
Badala yake wanawake wenyewe walifanywa mali ya kurithiwa kwa nguvu na ndugu wa marehemu au mtoto mkubwa wa kiume wa marehemu ambaye hakuzaliwa na huyo mama anayerithiwa. Waliwarithi kama wake au vinginevyo waliwaoza kwa wanaume wengine kwa nguvu kinyume cha ridhaa ya wajane hao. Kwa namna hii wanawake walirithiwa kama sehemu ya mali ya marehemu na waliuzwa na kununuliwa kama bidhaa. Uislamu umepiga marufuku tabia hii katika aya ifuautayo:
Enyi mlioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa jeuri. Wala msiwazuie (kuolewa na wanaume wengine) iii mpate kuwanyang 'anya baadhi ya vile mliiyowapa(Hapana ruhusa haya) isipokuwa wawe wamefanya uovu ulio wazi nakaeni nao kwawema " (4:19).
Wala msiwaoe wake waliowaoa baba zenu, ispokuwa yale yaliyokwisha pita. Bila shakajambo hili ni uovu na chukizo na ni njia mbaya. (4:22).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 web hosting 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Mgawanyo wa mirathi kutoka kwenye Quran
Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo.
Soma Zaidi...Jinsi ya kuswali swala ya kuoatwa kwa juwa ama swala ya kuoatwa kwa mwezi.
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya kupatwa yaani kupatwa kwa juwa na kupatwa kwa mwezi swalat kusuf na swalat khusuf
Soma Zaidi...Haki za kiuchumi za mwanamke katika uislamu
Haki za UchumiKuwa imara kiuchumi ni sababu mojawapo kubwa ya kumpa mtu hadhi katika jamii.
Soma Zaidi...Hizi ndio nyakati za swala tano na jinsi ya kuchunga nyakati za swala.
Posti hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkuchunga nyakatibza swala tano.
Soma Zaidi...Masharti ya swala
Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Soma Zaidi...