picha

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Kabla mali ya marehemu haijagawanywa kwa warihi wake, hapana budi kuzingatia yafuatayo:



(a)Haki zilizofungana na mali ya urithi:
Mali ya marehemu haitakuwa halali kwa warithi wake mpaka zitolewe haki zifuatazo:
(i)Madeni.
(ii)Zakat.
(iii)Gharama za makazi ya mkewe katika kipindi cha eda.
(iv)Usia ambao hauzidi theluthi moja (1/3) ya mali yote iliyobakia.



(b)Sharti Ia kurithi:
Kurithi kuna sharti tatu:
(i)Kufa yule mwenye kurithiwa (Si halali kurithi mali ya mtu aliye hai).
(ii)Kuwepo hai mrithi wakati akifa mrithiwa. Kwa mfano, kama wawili wanaorithiana mathalani baba na mtoto wote wamekufa. Aliyekufa nyuma (au aliyeshuhudia kifo cha mwenzie) atakuwa mrithi wa yule aliyetangulia kufa.
(iii)Kukosekana mambo yenye kumzuilia mtu kurithi.



(c)Mambo yanayomzuilia mtu kurithi
Mrithi huzuilika kurithi itakapopatikana na moja kati ya sababu zifuatazo:


(i)Kumuua amrithiye: Yaani mtu hatamrithi aliyemuua ijapokuwa kwa bahati mbaya.
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema Mwenye kuua hapati chochote katika mirathi. (Tirmidh, Ibn Majah).



(ii)Kuhitalifiana katika dini:
Muislamu hamrithi kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi na wala kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi hatamrithi Muislamu hata akiwa karibu naye kiasi gani katika nasaba.
Usama bin Zaid (r.a)ameeleza kuwa mtume wa Allah amesema: Muislamu hamrithi mshirikina wala mshirikina hamrithi Muislamu. (Bukhari na Muslim)
Pia Mtume (s.a.w) amesema katika Hadithi iliyosimuliwa na Abdullah bin Amri(r.a) kuwa: Watu wa dini mbili tofauti hawatarithiana. (Abu Dauwd, Ibn Majah, Tirmidh).



(iii)Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hana haki ya kumrithi baba aliyemzaa na baba hana haki katika mirathi yake, kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Amri bin Shuab(r.a) ameeleza kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake kuwa Mtume wa Allah amesema: "Atakayezini na mwanamke muungwana au na mjakazi, mtoto atakayepatikana humo hana haki naye. Hatomrithi na wala hatarithiwa naye ". (Tirmidh)



(d)Sababu za Kurithi:
Mtu hurithi kwa sababu moja katika hizi:
(i)Kuwa na nasaba na marehemu (baba, mama, mtoto, ndugu, n.k.). (ii)Kuoana kwa ndoa halali (yaani mume humrithi mke na mke humrithi mumewe).
(iii)Kuacha huru, yaani mwenye kumpa uhuru mtumwa humrithi huru wake.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 2195

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Vipi utapata uchamungu kupitia funga

Vipi lengo la funga litafikiwa na kumfanya mfungaji awe mchamungu.

Soma Zaidi...
kuletewa ujumbe

(c)Kuletewa Ujumbe na Malaika kutoka kwa Allah (s.

Soma Zaidi...
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU

Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji.

Soma Zaidi...
Tofauti kati ya zakat na sadaqat

Nguzo za Imani, tofauti kati ya sadaqat na zakat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat

Nguzo za uislamu, masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Njia za kudhibiti riba

Ufumbuzi wa tatizo la ribaRiba imeenea na kuzoeleka duniani kwa kiasi ambacho watu wengi wanadhani kuwa bila riba hakuna shughuli yoyote ya uchumi inayowezekana.

Soma Zaidi...
Taratibu za kuchaguwa mchumba katika uislamu

Hapa utajifunza hatuwa kwa hatuwa za kuchaguwa mchumba kulingana na sheria za kiislamu.

Soma Zaidi...