Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Kabla mali ya marehemu haijagawanywa kwa warihi wake, hapana budi kuzingatia yafuatayo:
(a)Haki zilizofungana na mali ya urithi:
Mali ya marehemu haitakuwa halali kwa warithi wake mpaka zitolewe haki zifuatazo:
(i)Madeni.
(ii)Zakat.
(iii)Gharama za makazi ya mkewe katika kipindi cha eda.
(iv)Usia ambao hauzidi theluthi moja (1/3) ya mali yote iliyobakia.
(b)Sharti Ia kurithi:
Kurithi kuna sharti tatu:
(i)Kufa yule mwenye kurithiwa (Si halali kurithi mali ya mtu aliye hai).
(ii)Kuwepo hai mrithi wakati akifa mrithiwa. Kwa mfano, kama wawili wanaorithiana mathalani baba na mtoto wote wamekufa. Aliyekufa nyuma (au aliyeshuhudia kifo cha mwenzie) atakuwa mrithi wa yule aliyetangulia kufa.
(iii)Kukosekana mambo yenye kumzuilia mtu kurithi.
(c)Mambo yanayomzuilia mtu kurithi
Mrithi huzuilika kurithi itakapopatikana na moja kati ya sababu zifuatazo:
(i)Kumuua amrithiye: Yaani mtu hatamrithi aliyemuua ijapokuwa kwa bahati mbaya.
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema Mwenye kuua hapati chochote katika mirathi. (Tirmidh, Ibn Majah).
(ii)Kuhitalifiana katika dini:
Muislamu hamrithi kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi na wala kafiri, mshirikina, mkristo au myahudi hatamrithi Muislamu hata akiwa karibu naye kiasi gani katika nasaba.
Usama bin Zaid (r.a)ameeleza kuwa mtume wa Allah amesema: Muislamu hamrithi mshirikina wala mshirikina hamrithi Muislamu. (Bukhari na Muslim)
Pia Mtume (s.a.w) amesema katika Hadithi iliyosimuliwa na Abdullah bin Amri(r.a) kuwa: Watu wa dini mbili tofauti hawatarithiana. (Abu Dauwd, Ibn Majah, Tirmidh).
(iii)Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa hana haki ya kumrithi baba aliyemzaa na baba hana haki katika mirathi yake, kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Amri bin Shuab(r.a) ameeleza kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake kuwa Mtume wa Allah amesema: "Atakayezini na mwanamke muungwana au na mjakazi, mtoto atakayepatikana humo hana haki naye. Hatomrithi na wala hatarithiwa naye ". (Tirmidh)
(d)Sababu za Kurithi:
Mtu hurithi kwa sababu moja katika hizi:
(i)Kuwa na nasaba na marehemu (baba, mama, mtoto, ndugu, n.k.). (ii)Kuoana kwa ndoa halali (yaani mume humrithi mke na mke humrithi mumewe).
(iii)Kuacha huru, yaani mwenye kumpa uhuru mtumwa humrithi huru wake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza faida za ndoa katika Jamii na kwa wanadamu kiafya, kiroho, kiuchumi
Soma Zaidi...Ugumba ni รขโฌลugonjwa wa mfumo wa uzazi unaofafanuliwa kwa kushindwa kupata ujauzito baada ya miezi 12 au zaidi ya kujamiiana bila kinga mara kwa mara. Utasaรย kutoweza kwa kiumbe hai kufanya uzazi wa ngono au kutoweza kupata mimba au kuchangia mimba.
Soma Zaidi...Kipengele hichi tutajifunza namna ya kusimamisha swala ukiwa safarini na vitani na nguzo zake.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Tumesha mzika maiti sasa imebakia mali yae nyumbani, watoto, wake na menginyeo.
Soma Zaidi...