Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuongeza damu
VYAKULA VYA KUONGEZA DAMU
Damu ni tishu iliyo katika kimiminika. Katika miili yetu damu ina kazi ya kusafirisha viinilishe na hewa ya oksijeni na kuondoa hewa chafu ya kabonidaiyoksaidi mwilini. Pia urekebishwaji wa joto na usafirishwaji wa homoni ndani ya mwili hutegemea damu. Kwa ufupi damu in akazi nyingi. Upungufu wowote wa damu mwilini unaweza kuleta athari nyingi mbaya za kiafya mwilini. Makala hii inakwenda kukueleza njia ya kuongeza damu kwa haraka.
Kazi za damu mwilini1.Kusafirisha viinilishe kutoka katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.2.Kusafirisha hewa ya oksijeni kutokakwenye mapafu kwenda maeneo mengine ya mwli.3.Kusafirisha hewa ya kabonikaiyoksaidi kutoka kwenye seli na kpeleka kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje4.Kudhibiti joto la mwili kwa kulipooza inapohitajika na kuliongeza inapohitajika5.Kusafirisha homoni kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
Vyakula vya kuongeza damu mwilini1.Nyama nyekundu kama nyama ya ng’ombe, mbuzi. Kondoo2.Maini3.Nyama ya figo4.Mboga za rangi ya kijani kama mchicha na apinachi5.Maharagwe6.Kunde7.Mayai8.Nafaka nyinginezo9.Njegere10.Koeosho na karanga11.Samaki12.Nyama ya ndege13.Karoti14.Matikiti15.Zabibu16.Viazi vitamu17.Matunda yenye uchachu kama machungwa, ndimu na limao.18.Polipili nyekundu
Dalili za kupungua kwa damu mwilini1.Uchovu wa hali ya juu2.Udhaifu wa mwili3.Ngozi kuwa na rangi ya njano au mauko4.Kupumua kwa shida5.Mapigo ya moyo kutokuwa ya kawaida6.Kizunguzungu na kichwa kuhisi chepesi7.Maumivu ya kifua8.Miguu na mikono kuwa ya ubaridi9.Maumivu ya kichwa
Sababu za upungufu wa damu mwilini1.Upungufu wa madini ya chuma mwilini2.Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini3.Maradhi kama HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu4.Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)5.Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.6.Kuwa na maradhi ya sickle cell
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin A
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za stafel/soursop
Soma Zaidi...kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake mwilini.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyama
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maini
Soma Zaidi...Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Soma Zaidi...vitamini B vipo katika makundi mengi kma aB1, B2, B3, B5, B6, B7 na B12. Makala hii itakwenda kukutajia kazi kuu za Vitamini B katika miili yetu
Soma Zaidi...