Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mapema, kwa sababu ya kuwepo kwa saratani ya matiti, kuna dalili ambazo zikijitokeza zinapaswa kutolewa taarifa mara moja bila kuchelewa kama ifuatavyo.
Mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mara moja.
1. Kuwepo kwa uvimbe kwenye matiti, kuwepo kwa fundi gumu kama mbegu ndani ya titi au kwapani, hizi ni Dalili za kuripoti mara moja pindi zinapotokea inawezekana kubwa Dalili ya saratani ya matiti au pengine ni ugonjwa wa kawaida unaohitaji tiba mara moja,
2. Pengine matiti yanaweza kuwa na joto la hali ya juu na Dalili za wekundu zinaweza kujitokeza kama si wekundu inaweza kuwa na rangi nyeusi kwenye matiti na kwa wakati mwingine kuna hali ya kubadilika kwa umbo la titi na kuwa kubwa kuliko kawaida au pengine na maumivu yanaongezeka kadri ya ukubwa wa titi linavyoongezeka.
3. Na dalili nyingine ni ngozi kujikunja au kubwa na vitundu na kuifanya iwe na ganda la chungwa kwa dalili hii hakuna maumivu yoyote yanayoweza kujitokeza bali ukilipapasa titi linakuwa gumu na labda Chuchu ndiyo inakuwa inawasha na kutoa maji na pengine hizo Chuchu na sehemu nyingine za titi kubonyea kwa ndani .
4. Dalili nyingine ni pamoja na Chuchu kwa na maumivu makali na pengine kama kutoa maji maji kama hali haikutibiwa inaweza kuleta matatizo makubwa ambayo kuja kuyatibu ni shida kubwa, kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa kama mama ananyonyesha na Dalili hizi zinajitokeza hapaswi kabisa kumnyonyesha mtoto anapaswa kutoa taarifa mara moja na kupata huduma hospitalini.
5. Kwa hiyo tunapaswa kuwa macho na makini kuhusu Dalili hizi hatari kwenye matiti, na tunapaswa kuelimisha jamii kujua wazi kubwa hizi zinaweza kuwa ni Dalili za saratani ya matiti, ila mwenye tatizo la namna hii anapaswa kupima na kujua kubwa ni saratani kweli kwa sababu kuna na magonjwa mengine yenye dalili kama hizi. Kwa hiyo saratani ya matiti ipo na inaweza kutibiwa hasa hasa mgonjwa akiwa mapema hospitalini.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Kitunguu thaumu ni katika viungo vya mboga na chakula.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango
Soma Zaidi...Posti hii itakwende kukueleza kuhusu faida za kula apple na umuhimu wake kiafya
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi juu ya madini ya zinki na faida zake katika mwili wa binadamu,
Soma Zaidi...