Navigation Menu



Fahamu Ute unaotoka wakati wa ujauzito

Posti hii inahusu zaidi Ute unaotoka wakati wa ujauzito, kwa kawaida wakati wa ujauzito Kuna Ute ambao utoka na ni tofauti na kawaida pale mwanamke akiwa Hana mimba.

Fahamu Ute unaotoka wakati wa ujauzito.

1. Kwanza wakati wa ujauzito Kuna Ute ambao utoka na huwa ni mweupe kwa aina yake na ikitokea Ute huo ukawa na rangi tofauti na nyeupe kunakuwepo na maambukizi.

 

2. Ute huo uongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa homoni aina ya estrogen kwa sababu ya kufanya kazi mbalimbali kwenye mwili wa Mama wakati wa ujauzito kwa hiyo na Ute wakati wa ujauzito uongezeka zaidi.

 

3. Kwa upande wa akina Mama kama Kuna Ute wowote unaotoka wanapaswa kuwa makini Ili kuangalia ni Ute wa aje kwa sababu kama ni wa njano panakuwepo na maambukizi na hivyo ni vizuri kabisa kugundua na kuweza kupata matibabu.

 

4. Kwa sababu mabadiliko ya Ute usababishwa na hali yoyote iliyopo kwenye via vya uzazi kwa sababu kwenye via vya uzazi kama Kuna magonjwa kama vile kaswende na kisonono usababisha na rangi ya Ute kubadilika kwa hiyo kama Kuna aina yoyote ya mabadiliko ni vizuri kutafuta matibabu mapema na iwezekanavyo kwa sababu mtoto akipata maambukizi akiwa tumboni anaweza kupata shida ikiwepo kupoteza maisha.

 

5. Kwa upande wa akina Mama wajawazito hasa wanaochelewa kuanza clinic wanapaswa kuanza mara Moja Ili kuweza kupata vipimo mbalimbali kama vile vipimo vya magonjwa ya zinaa ikiwemo kaswende na Ukimwi, kwa kufanya hivyo hata kama mama hawezi kuangalia Ute wake hata kama una maambukizi anaweza kujua kama Kuna maambukizi kutokana na vipimo.

 

6. Kwa hiyo wajawazito wakiona Ute unaongezeka 

Wakati wa ujauzito wasishangae wajue kuwa ni kawaida kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni na hasa hasa Ute uongezeka wakati wa kukaribia kujifungua, kwa hiyo wasishangae ni kawaida tu na pakiwepo wasiwasi wowote ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya Ili kuweza kupata matibabu zaidi.

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 24005


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Dalili za kasoro ya moyo ya kuzaliwa kwa watu wazima
Ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao (kasoro ya moyo ya kuzaliwa) ni hali isiyo ya kawaida katika muundo wa moyo wako unaozaliwa nao. utu uzima. Ingawa maendeleo ya kimatibabu yameboreshwa, watu wazima wengi walio na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa wanaweza wasip Soma Zaidi...

Dalili ambazo mwanamke hapaswi kufumbia macho
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mwanamke hapaswi kufumbia macho. Soma Zaidi...

Damu, majimaji na uteute unaotoka kwenye uke wa Mjamzito, sababu zake na dalili zake
Unataka kujuwa sababu za mjamzito kutokwa na damu, utelezi ama majimaji kwenye uke wake. Na dalili gani zinaashiriwa na majimaji haya Soma Zaidi...

Nina vidonda kwenye uume wangu, je ni dalili ya nini?
Soma Zaidi...

Sababu za kuharibika kwa ujauzito na dalili zake
Dalili za kuharibika kwa ujauzito na dalili za kuharibika kwa ujauzo Soma Zaidi...

Jifunze kuhusu Protini, Fati, Wanga na kazi zao mwilini na vyakula vinavyopatikaniwa kwa wingi
Soma Zaidi...

Faida na hasara za Kufunga kizazi kwa Wanaume
Posti hii inazungumzia Faida, hasara, na madhara ya Kufunga kizazi kwa Wanaume. Soma Zaidi...

Siku za kupata ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata ujauzito Soma Zaidi...

Njia za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha.
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha kwa sababu kuna familia nyingi zinakosa watoto sio kwa sababu ni tasa ila kuna njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

sas na karibia mwezi nawashwa sehem Zang za sili kwenye shingo ya uume najikuta najikuna mpk natoka vidonda
Soma Zaidi...