Namna ya kuongeza na mjamzito ili kupata taarifa zake na kutoa msaada

Namna ya kuongeza na mjamzito ili kupata taarifa zake na kutoa msaada

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kugundua tatizo lake na kutoa msaada pale penye uhitaji.

Namna ya kuongea na mjamzito.

1.Kwana kabisa hakikisha kama kuna mazingira ambayo yatafamfanya ajisikie vizuri na mazingira yawe na vitu vinavyohitajika na uhakikishe kubwa anaweza kukaa vizuri na kuweza kujisikia huru pale unapoongea naye.

 

2.Muulize kuhusu familia yake na watoto alionao kwa sasa na unapaswa kujua anataka kuwa na watoto wangapi, uliza kama anajua tarehe yake ya kujifungua kama hajui hakikisha anatoka kwako anajua tarehe maalum ya kujifungua.

 

3.Pia muuulize kama as mewahi kutumia uzazi wa mpango, na amepata faida gani au hasara zilizopata kutokana na uzazi wa mpango, kama hana taarifa yoyote kuhusu uzazi wa mpango mafundishe ba uhakikishe anajua jinsi ya kutumia uzazi wa mpango.

 

4.Ongea naye kuhusu dawa anazozitumia kwa sababu kuna wengine wanatumia dawa mbalimbali kama vile za kisukari, presha, degedege,na wengine dawa za kuongeza maisha, ongea naye na umpe ushauri kadri unavyoweza kuhusiana na matumizi ya dawa na matokeo yake.

 

5. Muuulize kuhusu matumizi ya vyakula mbalimbali kwa mfano ni vyakula gani anapendelea na kumshauri kuhusu mlo kamili kwa wajawazito hasa vyakula vya kuongeza damu na madini ya chuma anapaswa kuvitumia kwa wingi na pia anapaswa kuachana na vyakula ambavyo havina faida yoyote mwilini kama vile pemba na utumiaji wa mawe wakati wa ujauzito.

 

6.Pia ongea naye kuhusu matumizi ya vileo kama vile matumizi ya madawa ya kulevya, vileo vikali, uvutaji wa sigara, na vitu kama hivyo ambayo usababisha madhara makubwa kwa mtoto wakati akiwa tumboni, kama kuna matumizi yoyote ya vitu kama hivyo elimu inapaswa kutolewa ili kuzuia matumizi ya vileo 

 

7.Pia tunapaswa kujua kama Mama amepata chanjo zinazohitajika wakati wa ujauzito kama vile chanjo ya pepopunda ambayo umkinga mama na mtoto dhidi ya magonjwa ya kupooza na Magonjwa mbalimbali mbalimbali, kama hajapata hakikisha mama anapata chanjo hiyo 

 

8.Pia ongea na Mama kuhusu Maambukizi ya virusi vya ukimwi na matumizi ya madawa na pia kuhusu Magonjwa ya ngono na matumizi ya dawa, mama kama hana taarifa zozote kuhusu hayo anapaswa kupima na kupewa dawa kama kuna Maambukizi.

 

9.Pia Mama anapaswa kuwa na uhusiano mzuri na watu kwa sababu mimba inaweza kumfanya akabalika katika hali isiyo ya kawaida au pengine anaweza kuwa na hasira na watu basi Mama anapaswa kuambiwa wazi kuwa anapaswa kuwa chukuliwa watu Kawaida na kumhakikishia kuwa akijifungua kila kitu kitakuwa sawa.

 

10.Pia tunapaswa kujua hali ya uchumi wa Mama mjamzito kama anaweza kupata mahitaji ya kila siku ya kawaida na kama akifanikiwa wakati wa kujifungua kama ataweza kupata hela ya kununua mahitaji wakati wa kujifungua, kama hawezi tafuta jinsi ya kumsaidia na kumshauri akate bima ya shilingi elfu thelathini kwa watu sita na itaweza kumsaidia wakati wa kujifungua.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 1306

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Sababu za mbegu za kiume kuwa dhaifu

Posti hii inahusu zaidi sababu za mbegu za kiume kuwa dhaifu, hali hii uwatokea wanaume wengi kwa sababu mbalimbali za kimaisha ambazo ufanya mbegu za kiume kuwa dhaifu na kusababisha madhara makubwa zaidi kwa sababu wanaume wengi ushindwa kujiamini kwa h

Soma Zaidi...
Je endapo mama atafanya tendo la ndoa wiki moja kabla ya kuingia hedhi anaweza kupata ujauzito?

Zipo siku maalumu ambazo mwanamke hupata mimba. Siku hizi huzoeleka kwa jina la siku hatari. Je ungependa kufahamu mengi kuhusu siku hatari, endelea na makala hii.

Soma Zaidi...
Changamoto za kwenye ndoa kwa waliotoa mimba mara Kwa mara

Posti hii inahusu zaidi changamoto za kwenye ndoa kwa wale waliotoa mimba mara Kwa mara,hizi ni changamoto za wakati wa kufanya tendo na mme wake au mtu mwingine kwa ajili ya kupata mtoto.

Soma Zaidi...
Vitu vilivyopo kwenye maji ya Amniotic fluid (majimaji yanayomzungruka mtoto aliyekuwepo tumboni wakati wa ujauzito)

Post hii inahusu zaidi viti vilivyopo kwenye maji ya Amniotic fluid, ni jumla ya vitu vyote vilivyopo kwenye maji ya Amniotic fluid.

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia mimba zisiharibike.

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuzuia mimba zisiharibike, kwa sababu kila mama anayebeba mimba anategemea kupata mtoto kwa hiyo na sisi hamu yetu ni kuhakikisha kwamba mtoto anazaliwa kwa kuzuia mimba kuharibik

Soma Zaidi...