Dalili za kujifungua hatua kwa hatua

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa

DALILI ZA UJAUZITO BAADA YA TENDO LA NDOA

Je umeshawahi kujiuliza ni zipi zinaweza kuwa dalili za kwanza za ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa? Hakika hili ni swali zuri na hapa niyakujuza majibu yake. Ukweli ni kuwa ni vigumu kuona dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa kama hutakuwa makini. Yes inawezekana kuzijuwa ila inahitaji uangalizi wa umakini kabisa. Mwanamke mmoja alishaniambia kuwa yeye ndani ya masaa matano baada ya kufanya tendo la ndoa anaweza kujuwa kama amebeba mimba ama laa. Nilipojaribu kumuuliza alikataa kabisa kunieleza.

 

Je naweza kuziona dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa?

Kabla ya kulijibu swahi hili inapasa kujuwa mabadiliko ya mwili wako kabla ya ujauzito ama kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwanza zingatia mabo haya kabla ya kushiriki tendo la ndoa:-

1. Jeoto la mwili wako. Hakikisha unatambuwa vyema kama mwili wako joto lake lipo kiasi gani. Na hakikisha unaweza kutofautisha kati ya joto la homa na joto la kawaida.

2. Zingatia majimaji ya kwenye uke wako. Zingatia kama uke wako upo katika majimaji ama upo mkavu. Pia angalia rangi za mashavu ya uke.

3. Zingatia tarehe zako. Kabla ya kushiriki tebdo la ndoa hakikisha tarehe zako unazifahamu vyema, pamoja na siku zako za hatari ni lini.

 

Je nitazijuaje sasa hizo dalili baada ya kuzingatia mambo hayo?

Kujuwa kama umebeba mimba ama laa inaweza kuchukuwa hata wiki moja kuona mabadiliko kwenye mwili wako, mabadiliko haya yataweza kukuambia kwamba huwenda umebebe mimba. Ila pia kuna baadhi ya waanwake wanaweza kuyana mabadiliko hayo mapema kabisa. Ila tambuwa kuwa mabadiliko hayo yote yanaweza kuwa ni vyanzo vya sababu zingine na si ujauzito.

 

Mabadiliko hayo ni kama:-

1. Kuongezeka kwa joto la mwili. Kama ulizingatia vyema joto la mwili wako wakati ukiwa katika siku za hatari linakuwa kubwa kulinganisha ziku za nyuma. Baada ya kushiriki tendo la ndoa angalia je joto litapunguwa ama kuongezeka. Kama litapunguwa baada ya kupita siku za hatari huwenda bado hujabeba ujauzito. Lakini endapo utaona joto halipungui na huwenda likaongezeka hii huonyesha kuwa una mabadiliko kwenye mwili wako ambayo huwenda ni ujauzito. Jifunze pia kutofautisha kati ya homa na joto la kawaida.

1. Majimaji kwenye uke na njia ya kuelekea kwenye tumbo la mimba. Kikawaida wakati wa siku za hatari kiasi cha majimaji kwenye uke huongezeka, hii ni kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kuweza kubeba mimba. Zinapopita siku za hatari majimaji hupunguwa na hatimaye kurudi hali ya kawaida ya ukavu. Sasa endapo majimaji hayatapunguwa na vinginevyo yakawa yanabadilika na kuwa mazito kuliko hapo mwanzo hii huashiria huwenda amebeba ujauzito.

 

1. Ok sasa zingatia ziku zako za hatari.kama ulishiriki tendo la ndoa katika siku hatari kisha ukaanza kuona mabadiliko kama kutokwa na damu chache iliyo tofauti na hedhi, ama maumivu ya tumbo ya ghafla, ama kichwa kuhisi chepesi mabadiliko kama haya na mengineyo huashiria ujauzito.

1. Mabadiliko ya rangi kwenye chuchu na mashavu ya uke yanaweza kuwa n dalili ya ujauzito. Matiti kuuma ama kuwa magumu hii ni katika dalili wanayoiona wengi katka wanawake. Mashavu ya uke hubadilika kuwa na uweuzi ama uwekundu kutokana na mishipa ya damu kuja juu na kupitisha damu kwa wingi maeneo ya chini ili kuandaa ukuaji wa mimba

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-10-29     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1159

Post zifazofanana:-

Ugonjwa wa coma
Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la Kichwa, Kiharusi, Uvimbe kwenye ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi, Soma Zaidi...

Kulelewa kwa Mtume, maisha yake ya Utotoni na kunyonya kwake.
Historia na sura ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 06. Hapa utajifunza kuhusu historia ya Mtume akiwa mtoto. Soma Zaidi...

Dalili za mimba katika mwezi wa kwanza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba katika mwezi was kwanza Soma Zaidi...

Madhara ya mafuta mengi mwilimi
Post hii itakufundisha madhara ya kuwa na mafuta mengi mwilimi Soma Zaidi...

Uwepo wa asidi nyingi mwilini
Posti hii inahusu zaidi tatizo la kuwepo kwa asidi nyingi mwilini hali uwasumbua watu wengi na kufikia kiasi cha kusababisha madhara mengine mawilini ikiwamo pamoja na kansa ya koo, ili kujua kama una wingi wa asildi mwilini unapaswa kujua dalili kama ifu Soma Zaidi...

Mambo ambayo yanaweza kuongeza hatari ya Ugonjwa wa Homa ya ini yenye sumu.
Posti hii inazungumzia zaidi kuhusiana na Homa ya ini yenye sumu ni kuvimba kwa ini lako kutokana na kuguswa na vitu fulani ambavyo umeathiriwa navyo. Homa ya ini yenye sumu inaweza kusababishwa na pombe, kemikali, madawa ya kulevya au virutubisho vya lis Soma Zaidi...

Elimu juu ya afya ya uzazi
Makala hii itakwenda kukufundisha mambo mbalimbali na muhimu kuhusu afya ya uzazi Soma Zaidi...

Mafunzo yatokanayo na hijrah ya mtume na maswahaba wake
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Madhara ya kuchelewa kutibu tatizo la kiafya
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea endapo tatizo halijatibiwa. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula ukwaju
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamin B
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamin B Soma Zaidi...

Dalili za saratani kwa watoto.
Posti hii inahusu zaidi Dalili za saratani kwa watoto, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto na ikiwa mlezi au mzazi akiziona tu anaweza kutambua mara moja kwamba hii ni saratani au la na kama bado ana wasiwasi anaweza kupata msaada zaidi kutoka kwa wataa Soma Zaidi...