Njia za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha.

Njia za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha.

Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini v

Njia za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha.

1. Kwanza kabisa tunajua kuwa maziwa ya Mama yanapaswa kuwa na virutubisho vyote vinavyohitajika kuna wakati mwingine virutubisho hivyo vinaweza kupunguza kwa sababu mbalimbali kama vile madawa, aina ya vyakula na njia mbalimbali za uzazi wa mpango ili kuepuka tatizo hili wanawake wanaonyonyesha wanapaswa kutumia njia zifuatazo.

 

2.Matumizi ya kitanzini.

Hii njia utumiwa na wanawake wanaonyonyesha kwa sababu haingiliani na uzalishaji wa maziwa, kitanzi hiki kimetengenezwa na madini ya kopa na uwekwa kwenye mlango wa kizazi na  kinaweza kukaa kwa mda wa miaka kumi na miwili, kwa hiyo uzuia mbegu za kiume kutokutana na mbegu za kike kwa hiyo mimba haiwezi kutungwa.

 

3.Pia wanaonyonyesha wanaweza kutumia njiti kwa sababu haingiliani na uzalishaji wa maziwa, huu njiti uwekwa mwilini juu ya mkono na uweza kuzuia mimba kwa kipindi cha miaka mitano, kwa hiyo kina homoni ambayo uzuia yai kupevuka kwa hiyo njia hizi inaweza kuwa na maudhi madogo madogo kama vile kutapika, kichefuchefu na kizungu Zungu na hivyo uisha kwenye miezi ya mwanzo na maisha uendelee kama kawaida.

 

4.Njia ya kutumia homoni ya progesterone peke yake iwe ya kuchoma au kutumia vidonge, hii ni njia ambayo uzuia yai lisipevuke na pia haingiliani na uzalishaji wa maziwa kwa hiyo mama anayenyonyesha anapaswa kutumia progesterone homoni peke yake asije akachanganya na oestrogen kwa sababu uingiliana na uzalishaji wa maziwa.

 

5.Pia Mama anaweza kutumia njia ya kunyonyesha kwa miezi sita ya mwanzoni baada ya hapo anaweza kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango, na pia kama familia haina mpango wa watoto wengine wanaweza kutumia njia ya kudumu ambapo wote wawili wanakata  mirija inayosafirisha mbegu na yai kwa kufanya hivyo hawawezi kupata watoto tena, kwa hiyo hizi ndio njia pekee kwa wanaonyesha na pia kondomu inaweza kutumika.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 13478

Share On:

Share follows: 5 | Unique share links followed: 1
Sponsored links
πŸ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰2 ai web app     πŸ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰5 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Fahamu kuhusiana na kubalehe kwa msichana na mvulana.

Kubalehe ni wakati mwili wa mtoto unapoanza kubadilika na kuwa wa mtu mzima (balehe) hivi karibuni. Kubalehe ambao huanza kabla ya umri wa miaka 8 kwa wasichana na kabla ya umri wa miaka 9 kwa wavulana.

Soma Zaidi...
Faida na hasara za kutumia uzazi wa mpango

Tunaposema uzazi wa mpango, tunamaanisha ile hali ya kuachanisha muda kutoka mtoto hadi mwingine. Inatakiwa angalau mtoto na mtoto wapishane miaka miwili. Uzazi wa mpango ni maamuzi kati ya mama na baba.

Soma Zaidi...
Dalili za upungufu wa homoni ya progesterone

Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu fangasi za ukeni

Posti hii inahusu zaidi fangasi za ukeni, hili ni tatizo kubwa ambalo linawakumba watoto, akina dada na wanawake kwa hiyo na vizuri kujua Dalili zake na kuweza kuchukua hatua mapema.

Soma Zaidi...
Siku za kupata mimba

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba

Soma Zaidi...