Dalili za mimba katika mwezi wa kwanza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba katika mwezi was kwanza
DALILI ZA MIMBA KATIKA MWEZI WA KWANZA (Ndani ya siku 30)Dalili hizi huweza kuonekana kwa urahisi kuliko hizo ambazo zimetajwa hapo juu. Ijapokuwa dalili hizi zinatokea ndani ya mwezi mmoja lakini zinaweza pia kutokea nje ya mwezi mmoja, yaani mpaka miezi mitatu. Sasa hebu tuzione dlili hizo:-
1.Kukosa hedthi.Kama ujauzioto ulishika mwanamke hataweza kupata siku zake. Hii ni dalili ambayowanawake wengi wamekuwa wakiamini kama ndio dalili pekee. Yes hii ni katika dalili kubwa ambazo wanawake wengi wameitaja kuwa ndio dalili yao ya kwanza. Unajuwa ni kwa nini? Ni kwa sababu ndio ya pekee wanayoweza kuigundua. Ukweli ni kuwa kukosa hedhi pekee sio dalili ya ujauzito, hedhi inaweza kukosekana kwa sababu kadhaa kama zifuatazo:-
A.Mabadiliko ya homoniB.UjauzitoC.MaradhiD.PIDE.VyakulaF.Stress na misongo ya mawazoG.Matumizi ya madawaH.Mabadiliko ya hali ya hewa.
Nini mwanamke afanye baada ya kukosa hedhi?.Yes hili ni swali zuri sana. Mwanamke aliyekosa hedhi kwanza aanze kufikiria kama alishiriki tendo la ndoa katika siku hatari ama laa. Kisha aangalie uwepo wa dalili nyingine kama nitakavyozitaja hapo chini. Kama hana dalili yeyote basui aangalie kama anapata maumivu sehemu yeyote, ama uwepo wa maradhi. Kama vyote hana ni vyema apime ujauzito. Kipimo cha mkojo kinaweza kuchelewa kutoa majibu, hivyo kama atapima wiki ya kwanz na asione kitu basi ni vyema akarudia tena wiki inayofata. Maelezo zaidi juu ya kutumia kipimo nitayataja hapo chini.
2.Maumivu ya matiti na chuchu, kujaa kwa matiti na mabadiliko ya rangi za chuchu.Dalili hii huwapata wanawake wengi, hata hivyo wapo ambao hawaipati kabisa. Hebu tuanze kuona kwa ufupi dalili hii. Mabadiliko ya rangi ya chuchu na eneo la kuzunguka chuchu. Hii ipoje ni kuwa mwanamke aliyebeba ujauzoto chuchu zake zinaweza kubadilika na kuweka ukiza na weusi. Inaweza kuwa chuchu pekee na na eneo la chini kuzunguka chuchu.
Kwa baadhi ya wanawake wao matiti yanauma na yanakuwa kama yamejawa na kaugumu flani. Wakati mwimgine inaweza kuwa titi moja ama yanaweza kuwa yote ama yakapeana zamu. Ila maumivu haya ni maumivu ambayo yanavumilia si makali kiasi cha kushindwa kufanya shughuli za kawaida. Kwa wanawake wengine maumivu haya hutokea pale anapoyaminya matiti yake.
Hata hivyo maumivu ya matiti pekee sio dalili ya moja kwa moja kuthibitisha ujauzito. Maumivu ya matiti yanaweza pia kusababishwa na maumivu ya kifua, shida katika homoni ama maradhi mengine. Hivyo bado itahitajika kupuma kupata uhakika.
3.Kukojoa mara kwa mara.Wiki kadhaa zimepita toka kuingia, homoni mbalimbali zimezalishwa ndani ya mwili,kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mama na mtoto. Homoni hizi zinapelekea mabadiliko mbalimbali ndani ya mwili wa mama, hivyo kusababisha mapigo ya moyo kuongezeka, mchujo wa damu kuwa mkubwa na uzalishwaji wa mkojo kuongezeka. Hapa mama mjamzito ataanza kuhisi mabadiliko katika kukojoa kojoa. Dalili hii kwa baadhi yao inachelewa kuonekana hadi miezi ya mbele.
4.Mapigo ya moyo kuongezeka.Hapa mwanamke anaweza kujihisi moyo kwenda mbio. Ukweli nikuwa kuna ongezeko la mapigo ya moyo kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ya mtoto aliyetumboni hayaathiriki. Dalili hii pia inaweza kuchelewa kuonekana ndani ya mwezi wa kwanza. Kwa baadhi ya wanawake watajihisi lamda ana presha lakini ukweli ni kuwa hii sio presa ni ongezeko tu la mapigo ya moyo.
5.Maumivu ya tumbo.Dalili hii inaweza kutokea hata katika wiki kadhaa za mwanzo. Ila mara nyingi hutokea ndani ya mwezi wa kwanza na ni endelevu. Yaani dalili hii inaweza kuendeea mpaka mtoto atakapozaliwa. Mwanamke awe makini sana na maumivu haya. Maana yanaweza kusababishwa pia na mambo mengine ikiwemo maradhi. Maumivu haya hayawezi kuwa makali kiasi cja kushindwa kufanya kazi za kawaida. Yanaweza kufanana na ya hedhi ama kuwa na uafadhali kidogo.
DALILI NYINGINE ZA UJAUZITO1.Uchovu wa mara kwa mara
2.Maumivu ya tumbo mara kwa mara
3.Kichefuchefu
4.Tumbo kukuwa.
5.Mtotockucheza
6.Kuongezeka kwa uzito
7.Kupata kiungulia mara kwa mara
8.Kukosa choo
9.Maumivu ya mgongo
10.Hasira za mara kwa mara
11.Maumivu maeneo ya nyonga
12.Kuharisha
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Changamoto za ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu changamoto za ujauzito na dalili zake endelevu
Soma Zaidi...je mtu kam anaona dalili za mimb ila akapima nakipim hakijamuonyesha kam ana mimb am hana je kuna uwezekan wakuw anayo
Dalili za mimba pekee haziwezi kuthibitisha uwepo wa mimba. Bila vipimo kwa. Muda sahihi huwezi kuwa. Na uhakika. Je na wewe unasumbuliwa na dalili za mimba na ukapona hakuna mimba? Makala hii ni kwa ajili yako. Swali
Soma Zaidi...Dalili za Mimba ya Siku 7 kwa Mwanamke
Kipindi cha siku saba baada ya kurutubishwa kwa yai (karibu wiki moja tangu kutunga kwa mimba) ni hatua ya mwanzo kabisa ambapo kijusi kinaanza kujipandikiza kwenye mji wa mimba. Ingawa mara nyingi ni mapema mno kwa vipimo vya mkojo kuonyesha matokeo chanya, mwili wa mwanamke unaweza kuanza kuonyesha dalili fiche za kibaolojia. Makala hii inaelezea kile kinachotokea mwilini mwako katika kipindi hiki cha siku saba.
Soma Zaidi...Sababu za kutoka mimba yenye miezi Saba na nane
Posti hii inahusu zaidi sababu za mtoto kuzaliwa akiwa na miezi Saba na nane kwa kawaida mtoto wa hivi anakuwa hajafikisha mda wake kwa hiyo uzaliwa akiwa na miezi saba na nane, kwa hiyo kuna sababu mbalimbali kama tutakavyoona
Soma Zaidi...Ay ni iv kipimo cha mimb uanz kutoa majb ndan ya mda gan wik mwez au iko vipi?
Kipimo cha Mlimba huweza kuonyesha mimba changa mapema sana. Pia ni rahisi kutumia na kinapatikana kwa bei nafuu. Je ungeoendavkujuwa ni muda gani kinatoa majibu sahihi?
Soma Zaidi...